Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 21,493
- 38,326
Heshima sana wanajamvi,
Leo nimeona wacha nitoe pongezi hata kama pongezi zenyewe si za dhati
Ziara ya waziri Lugola Mkoani Arusha imeleta neema na furaha kubwa ingawa hatujui kama furaha yetu itadumu kwa muda gani.
Wadau katika sekta ya utalii walitoa malalamiko yao kuhusiana na bughuza za maaskari wa usalama barabarani na wewe bila kupoteza muda ukatoa maagizo hata kama maagizo yako yalilenga magari ya watalii na sisi watalii wa ndani tumejikuta tukifaidika kwa namna moja na maagizo yako.
Kwa hakika askari wa usalama wa barabarani wamekuwa kero kubwa si kwa mji wa Arusha tu bali Tanzania nzima.Imekuwa kama laana siku hizi kumiliki gari au kuendesha gari Tanzania.
Binafsi nimekumbana na kero ya trafiki mara nyingi.Mfano kila siku asubuhi nikienda azini nasimamishwa na trafiki ESAMI maswali ni yale yale hakuna jipya lete leseni yako mara haukusimama zebra mara gari yako ina dent........Naondoka nikifika fire nasimamishwa tena maswali yasiyokuwa na kichwa wala miguu.Nikifika Metropole nasimamishwa tena yaani ni shida na taabu tupu.
Kila mwezi nafanya safari zangu Dar na Tanga nikitokea Arusha huko ni kivumbi na jasho matrafiki wako kwaajili ya kukusanya fedha si kudhibiti ajali.Imebidi nijifunze kuendesha usiku ili kukwepa bughuza.
Ukweli mchungu uonevu wa askari wa usalama barabarani ni matokeo ya matamko ya viongozi ambao hawajui kupitia kauli zao raia wa kawaida wanapata taabu kweli kweli.
Hongera Lugola ingawa kero ya matrafiki haikujiunda yenyewe,ilizalishwa,ikamea na kupaliliwa na viongozi sasa imekuwa janga kubwa kweli kweli wanaopaswa kulaumiwa ni viongozi ambao leo tunawasifu ingawa si kwa dhati.