Hongera kwa kuolewa

Hongera kwa kuolewa

mcndomba maprosoo

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2013
Posts
225
Reaction score
94
Tumsifu Yesu Kristu!
Hongera sana ndugu yangu. You are really beautiful Onyinye! Sometime ur like Ifunanya! Nimeona nipate wasaha huu kukuandikia ili kukutakia heri na fanaka katika harusi yako nafanya hivi nikitambua kuwa sitapata nafasi ya kuhudhuria katika sherehe hiyo si unajua tena ndiyo kwanza muhura wa masomo hapa ndo umeanza!

Hata hivyo nakupongeza sana, hakika wewe ni mwanamke hodari maana nawaona wale waliokuwa wakikudharau wakianza kukusalimia kwa heshima japo wapo wachache ambao hawana soni hao nao usihangaike nao si unajua duniani kuna watu wengi lakini binadamu ndio wachache cha msingi hapa endelea kuwa "hodari na moyo wa ushujaa kwa kuwa BWANA Mungu wako yuko pamoja nawe kila uendako", Yoshua 1:5-6,9; Isaya 41:10-12, 43:2). Mchuchu wako kaja lakini kaumia sana nimebaki kumtuliza moyo labda anxiety zitapungua.

Pamoja na hayo yote nakumbuka siku moja BWANA Yesu aliwahikuwaambia wanafunzi wake kuwa wasifurahi kwa kuwa mapepo yanawatii lakini furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa mbinguni, hapa ndipo ulipo ujumbe wangu kwako kwamba siku zote wasiokuwa kwenye ndoa wanatamani kuishi katika ndoa lakini walio kwenye umoja huo wanatamani kutoka unadhani kwanini? Ndoa si rahisi kama kumgonga mwanachuo na SUP, tena ndoa si masihala na nyepesi kama wengi wanavyodhani, pamoja na ugumu wote mwanamke ndiye anayepewa jukumu kubwa la kuamua ndoa iwe ngumu ama nyepesi kwani imeandikwa, "kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe", Mithali 14: 1 na hapa ndipo palipo msingi wa ndoa yako, kwa kiingereza inasomeka hivi, "EVERY WISE WOMAN buildeth her house; BUT THE FOOLISH plucketh it down with her own hands".

Kumbe wewe ndiwe utakayeamua kuwa wise woman ama foolish woman kazi ni kwako. Sulemani hakuishia hapo, "mke mwema ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani, moyo wa mumewe humwamini wala hata kosa kupata mapato…,apataye mke apata kitu chema naye naye ajipatia kibali kwa BWANA,… mke mwema ni taji ya mumewe…bali mke mwenye busara mtu hupewa na BWANA.. ", Mithali 12:4, 18:22, 19:14, 31:10-12.

Wanawake wengi wanajivunia uzuri walionao hebu angalia hili, "kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, ndivyo alivyo mwanamke mzuri asiye na akili", Mithali 11:22. Katika ndoa uzuri si dili ila namna ya kuwa naakili ya kuwa ‘wise woman' ndiyo dili na wala si kujivunia madigrii hayana maana kwa wakati huu ni sawa na kusikiliza simulizi za Alfu Lela Ulela ama zile za wagigikoko. Paulo anaongeza kuwa, "wake wawe wastahivu…mke asikose kumstahi mumwewe", Efeso 5:31, 1Tim 3:11. Hata kama kunashida kubwa kiasi gani mashindano ya mdomo si mazuri jifanye mjinga mwana, "jawabu la upole hugeuza hasira, bali neno liumizalo huchochea ghadhabu,…katika kosa la mdomo kuna mtego wa mabaya bali mwenye haki atatoka katika taabu…mtu atashiba mema kwa matunda ya kichwa chake na atarudishiwa matendo ya mikono yake", Mithali 12:13-14, 15:1.

Hongera sana, hepuka kubadili badili line!
 
Kurasa za kutosha mpaka zinaboa.
Fupisha hivi; NAKUPONGEZA KWA KUKARIBIA KUOLEWA, MIMI SITAFIKA KWA SABABU YA SHULE ILA MCHANGO WANGU NTAKUTUMIA KWA M_PESA. ZINGATIA KUMPENDA MME WAKO WALA USISIKILIZE MANENO YA WATU. PIA, MFANYE MUNGU NDO AWE KIONGOZI WENU. HONGERA
 
mahubiri mpaka yanachosha,lol ila hata kanisani kuna wanaohubiri mpaka unasinzia nahisi na wewe ni mmoja wao lol
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom