Hongera Jeshi la Magereza na Mbunge wa Segerea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Jeshi la Magereza na Mbunge wa Segerea

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by HomeSweetHome, Apr 11, 2011.

 1. H

  HomeSweetHome Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwako Mkuu wa Jeshi la Magereza-Segerea,

  Ninakupongeza kwa kuamua kutufungia njia ya tabata segerea kulekea bunyokwa, kisukuru B na baadhi ya vitongoji vyake bila kutoa hata notice. Nakupongeza kwa kuwa na ujasiri wa kuvumila wapita njia, magari na raia wema wote kwa muda wa zaidi miaka 10. Ninakupongeza kwa kuwa umeona ni busara kuwafungia njia zaidi ya wananchi ya familia 2000 zenye watu zaidi ya 8000 tuliokuwa tunapita katika njia hiyo.

  Ni matumaini yangu kuwa huna mpango wa kufungua tena njia hiyo kwa kuwa sasa umeamua kupanda uzio wa katani katika njia hiyo na kuonesha dalili kuwa huna hata chembe ya huruma kwa idadi kubwa ya wananchi waishio maeneo ya huko. Umeonesha uzalendo mkubwa kwa serikali unayoitumikia kwa kupata mshahara wa walipa kodi ambao ndio wananchi uliowafungia barabara.

  Ninakupongea kwa kuwa fikra zako za kutufungia barabara zimekuja wakati mbaya ambapo serikali unayoitumikia umekalia kuti kavu hivyo kukabiliwa na presha ya kung'olewa madarakani ifikapo mwaka 2015. Na sasa umeamua kumuwekea mazingira magumu mbunge wa jimbo la segerea, kwa kuwa naye mpaka sasa anaendelea kutumbua fedha za walipa kodi huku akisahau kuwa kazi yake ya kutuwakilisha bungeni ni pamoja na kulinda na kutetea haki za wananchi waliomtuma.

  Ewe mheshimiwa mbunge, nakupongeza kwa kuwa kazi yako ya ubunge 'uwakilishi wa sauti' ya wananchi waliokutuma imekushinda na kuamua kutolea ufafanuzi suala letu la kufungiwa barabara bila NOTICE. Nakupongeza kwa kuwa usitarajie tena kushinda ubunge na kuwakilisha wananchi ambao huwezi kuwasemea pamoja na kuwa u sehemu ya serikali.

  Mhe. endelea kukaa kimya hivyo hivyo na sisi wananchi tutazungumza na wewe lugha rahisi na nyepesi kwa kutumia VIKARATASI tu ifikapo mwaka 2015. Tunakusikitikia kwa kuwa tutakesha kulinda hivyo vikaratasi kuhakikisha hauibi tena kura kama ulivyomfanyia Bw. Frdy Mpdzoe mwaka 2015. Tunakuhakikishia kuwa safari hii hautaenda tena mahakamani kujibu tuhuma za wizi wa kura na badala yake utafarijiwa na familia yako ambayo wamekuwa wakikufariji miaka yote kwa kupenya kwa uchakachuaji.

  ni hayo tu kwa leo, natamani tuonane uso kwa uso ili ukiniona sura yangu ujue kweli ninamaanisha ninachokisema.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,596
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  Omba ruhusa kazini FACE HIM!! huwa hata hawasomi humu,

  Poleni na please dont just speak, face him tell him plainly!

  Juzi tulimuita mbunge mmoja na kumweka kiti moto, huwa wadogo sana ukiwa-confront,

  otherwise dumisha mila ya kitanzania ya kulalamika

  Wewe na hizo familia you are coward, na mtalia tu kwa mtindo huu!
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,514
  Likes Received: 5,641
  Trophy Points: 280
  wakenya huwa hawalalamiki! Wale wakazi wa tegeta hawakulalamika walipiga la mgambo tu! Nafikiri kupunguza malalamiko this is one of ways!
   
 4. J

  Jonas Mpango Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa, nakushukuru kwa kuliona hilo. Sasa tumeishazuiwa njia. Ila gereza liliikuta njia. kwa kawaida ukikuta njia, inabidi watu uwape nyingine kabla ya kufunga ya mwanzo. Nadhani tujitahidi kutengeneza pale kwenye vilima kwani vinateleza wakati wa mvua. Bajaj zetu itabidi kuziacha Segerea Stand wakati wa Mvua. Kamati zetu za mitaa za Kisukuru na Bonyokwa itabidi zifanye kazi. Hiyo idadi ya wakazi uliyokadiria ni ndogo mno, ni zaidi ya mara mbili ya kako.Asante.
   
 5. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Segerea kuna mbunge? Mbona mahakama haijamtangaza?
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Huyu mbunge aliyebebwa ndo leo mnamlilia! ULIMWINGIZA WEWE MKUU USILIE SANA MLISHINDWA KULINDA KURA ZENU VUMILIENI MATATIZO!
   
 7. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Aaggg. Niliposoma kichwa habari ilikuwa nisifungue hii thread kwa sababu tu ya kumsifia mwizi (mbunge) lakini, lo. Asante sana. Mbunge mwizi kama huyu usitazamie atazungumza tena na watu. Na kulingana na upepo wa mabadiliko ya cabinet yanayokuja (offcourse lazima januari awe forein minister) nitashangaa akibaki kwenye baraza la mawaziri.
   
Loading...