hongera Halmashauri ya Mpanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hongera Halmashauri ya Mpanda

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by ngoshwe, Aug 10, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nimevutiwa na jinsi Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ilivyojipanga kwa maonesho ya Nane nane hasa kwa kuwa na mfumo wenye kuwezesha mnyororo wa thamani (value chain) kwenye kilimo. Japo ipo mbali na mji mkuu wa nchi, Halmashauri hii iliyopo mkoa wa Katavi imeweza kuandaa vituo vya kuendeleza wakulima katika skimu ya kilimo ya Mwamapuli,kuna soko na kituo cha habari, trekta, miundo mbinu ya umwagiliaji, Saccos, kisima cha kuvunia maji nk. Pia wameweza kuandaa kitabu "kiongozi cha Mkulima" ambacho kinamsaidia mkulima badala ya kutegemea zaidi mtaalamu wa Ugani ambae kwa sasa ni vigumu kumfikia kila mkulima kwa wakati. Halmashauri zote nchini zingekuwa makini na kuiga yale yanayofanywa na wengine hakika kilimo kingeboreka kwa kuongeza tija, thamani na bei nzuri kwa maana ya kutekeleza Kilimo Kwanza.
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hongera sana, sasa tunataka kuona hayo kwenye maisaha ya kila siku ya mkulima...
   
Loading...