Hongera chama pinzani

Sharo hiphop

JF-Expert Member
May 17, 2011
660
99
Chama cha wananchi cuf, kimetanganza mkakati wa kufanya maandamano kupinga uhalifu wa polisi tz. Naona hii ni hatua mmojawapo ya kupinga ubabe wa polisi usio na maana kwani mara nyingi wamekuwa wanafanya kazi hasa za kupinga mambo mbalimbali kama maandamano ya vyama vya siasa, wanafunzi n.k mpaka wanaboa, nahisi hawa jamaa mara nyingi ni kama wanatumwa na ccm! Hongera cuf....
Ewe mwana jf, unayaona haya maandamano kivipi?

Naomba kuwasilisha.
 
Hawa polisi wanaishi katika mazingira magumu sana, wanashindwa kuilaumu serikali hasira zao wanamalizia kwa wananchi
 
Yale ya Tarime wengine walidhani chadema wanayakuza haya saa CUF nao haooo, hapo mjue hili jeshi la polisi kuna walakini mkubwa sana ndani yake! hatua lazime zichukuliwe haraka sana lkn kuwaachia askari kama akina MASSAWE waendelee kukaa kwenye jeshi hilo ni sawa na kuwapa wendawazimu silaha!!
 
Hapo naunga mkono asilimia mia, lakini Cuf walijaribu nao pia kwa kumtumia Ismail Jussa kuchochea fujo za chuki dhidi ya Bara, wanawaita wakoloni weusi, kwa Ismail Jussa na mwenzake Mnyaa wote wawili wamepewa kazi mpya baada ya hiyo ya kuvunja Muungano kushindikana, moja wameweza la kuvuruga history ya Zanzibar ili waarabu waliokuwa wanauza watumwa waonekane mashujaa katika history ya Zanzibar na kumwita Nyerere Joka lililojaribu kuimeza Zanzibar, hiyo ni kazi yenyewe ya Cuf, mengine ni mbwembwe tu
 
Hii ni sawa na UVCCM kutaka bodi ya mikopo ivunjwe, mwaka huu tutasikia mengi, serikali inapigana kila idara
 
Hawa polisi wanaishi katika mazingira magumu sana, wanashindwa kuilaumu serikali hasira zao wanamalizia kwa wananchi


Kuna mtu amewalazimisha kuwa mapolisi? wameamua wenyewe na inabidi hali waliyonayo wakubaliane nayo tu, tena wana unafuu sana sababu wanaweza kula rushwa, lakini ukiangalia kwa mtu kama mwalimu, ana nafasi gani ya kula rushwa? kwa ufupi ni kwamba wao wamefunzwa kuwa wakatili and they are reacting in the same way. cha muhimu ni huko chuoni waangalie njia mbadala na za kisasa za kuwapatia mafunzo hawa jamaa .

kuhusu chama cha CUF nadhani wanadandia treni kwa mbele baada ya kuona CHADEMA wanafanya kazi ya nguvu.
 
Back
Top Bottom