Hongera CHADEMA - fanyeni zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera CHADEMA - fanyeni zaidi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Sep 16, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 16, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nilipata faraja sana niliposikia an kusoma kwenye magazeti na mitandao kadhaa kwamba chama cha democrasia na maendeleo sasa kimeamua kuanzisha utaratibu wa kukusanya michango yake kwa kupitia mitandao ya simu za mikononi .

  Sikuweza kutoa mchango wangu wowote kwa kipindi hicho kwa sababu nilijua hichi kitu wamekiiga kutoka kwa taasisi ya elimu Tanzania ambayo mpaka leo hii ina utaratibu huo wa kusaidia watu wenye ulemavu nchini .

  Pia utaratibu kama huu uliwahi kutumiwa na mgombea uraisi wa marekani wakati huo ndugu barak obama , aliweza kukusanya pesa nyingi sana tofauti ni kwamba yeye alitumia mtandao wa internet katika kufanikisha hilo mtu aliyetengeneza system hiyo ya ukusanyaji wa pesa anazungumza kiswahili chadema wangeweza kuwasiliana nae angeweza kuwapa miongozo zaidi

  Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha kisiasa lakini nimefurahia kwa sababu huko ni kukua kwa ICT katika sehemu mbali mbali ambapo inatumika , hongereni sana chadema lakini pamoja hongera hizi kuna baadhi ya vitu nimeona niwaambie .

  Huduma yoyote ambayo inaanzishwa haswa inayohusiana na vitu binafsi ( privacy ) lazima kuwe na mkataba Fulani kati mwenye huduma na yule ambaye anatumia huduma hiyo , je kuna mwanachama wowote wa chadema aliyepata kusoma maelezo zaidi kuhusu huduma hii kama akipata matatizo yoyote pindi anapochagia pesa huko mbeleni ? una hakikishiwa vipi usalama wako na familia yako .

  Huko nyuma tumewahi kusikia tetesi kuhusu watu waliokamatwa au kufanyiwa hujuma kwa kuchangia vyama au taasisi zingine ambazo zinaonyesha upinzani Fulani dhidi ya makundi mengine kwa hili chama kitahakikishaje mawasiliano yake hayaingiliwi na watu wengine yaani kulinda wale wote wanaochangia ? kwa kutumia njia hii ni rahisi sana kufuatilia wanachama kwa sababu siku hizi Tanzania namba zinasajiliwa kwa makampuni vyombo vya sheria vinaweza kuomba mawasiliano haya inapobidi .

  Tumeona nchi kama IRAN serikali ya nchi ile ilivyoweza kudhibiti mawasiliano ya wapinzani pindi walipotaka kuandamana au hata kuandamana na siku si nyingi tumeona gabon vyombo vyao vilivyoweza kudhibiti wanaharakati pamoja na wapinzani wao hili somo naona kwetu bado halijafika .

  Pia sheria zetu za nchi zinasemaje kuhusu viwango vya michango kwa vyama vya siasa haswa vinavyohusiana na mitandao ya simu , kwetu pia hatuna sheria maalumu zinazohusiana na mitandao kama zipo mimi sizijui hapo ningeweza kuongea zaidi .

  Ingawa hii huduma ya kuchangia haifanyi kazi kama ilivyokusudiwa mpaka sasa kwa sababu wenyewe wanasema bado wanatengeneza databank kama , hii ni maajabu sana kwanini walikimbilia kutangaza kwenye vyombo vya habari kuhusu huduma hii wakati walijua haiko sawa – hii ni picha kamili ya upinzani pamoja na wengine wa chama tawala – ni picha kamili ya jamii ya kitanzania .

  Bora mheshimiwa raisi alisema atajibu maswali live kwa njia ya barua pepe pamoja na simu akafanikiwa kufanya hivyo , nina wasi wasi chadema wangejaribu hili wangeweza kuja kutuambia barua pepe zao zilijaa sana , maswali ni mengi mno .

  Mwisho ni kuwakumbusha CHADEMA kuhusu kufanya mabadiliko ya mara kwa mara kwenye tovuti yao , nimeona mfano zitto kabwe ana blogu katika tovuti ya chadema lakini updates zake hazipo kama hotuba anazotoa mara kwa mara pamoja an mengine anayoandika hivi ni vitu muhimu sana kuna watu hawapati taarifa hizi sehemu zingine , Mfano zitto anatakiwa mada zake azianzishe kwenye blogu yake kwanza ndio ziweze kuhamia sehemu zingine hii ni njia nzuri sana ya kuweka wanachama karibu .

  Mimi sio mwanachadema niko kwenye Fani Ya ICT imegusa kwenye vitu tunavyofanyia kazi na kujadili kila siku , nimeona nichangie hilo kidogo .

  NAWATAKIA MAFANIKIO .
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 764
  Trophy Points: 280
  Hawa wachaga hakuna haja kuwapongeza kuhusu kukusanya hela hiyo ni jadi yao, hawahitaji hata hata hizo lecture zako.
   
 3. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Shy pamoja na pongezi kwa hiyo NGO yakina Ndesamburo & Co lakini hakuna mtu makini atakayechangia fedha kwa ajili ya kuvurumisha Chopper angani kwa minajili ya kuwavuta wanavijiji ambao hawajawahi kuiona.
   
 4. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Shy umenifurahisha, pamoja na kuwakumbusha bado unawaeleza CHADEMA wanaweza kukutumia.

  Tokea wamalize uchaguzi wao wako kimya hata kwenye chaguzi serikali za mitaa siwasikii kabisa acha tuwape muda kwani usimwamshe aliyelala!
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  unapozindua ujenzi wa barabara au shule au mradi fulani si kwamba tayari ni barabara na magari yanapita. Pale CHADEMA ni kama waliweka jiwe la msingi kwa hiyo ujenzi wa mtandao huo wa simu na database ya wanachama uanendelea. Kwa hiyo wakuu msiwe na haraka, haya mambo yanahitaji fedha si bure.Shy, unasema bora JK alisema ataongea na wananchi live na akafanya, lakini bora angesema apelekewe maswali atayajibu kuliko majibu ya hovyo hovyo aliyoyatoa. CHADEMA hawataki kuanza bila mpangilio halafu baada ya wiki waseme database imecorupt.Nadhani ni mwanzo mzuri tuwape muda.
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  wewe tu, sisi tutachangia tu japo kidogo, wewe umezoea kuchangia lile lori la mzee komba na kwaya yake na huoni hata aibu!!ah!!!
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145

  Sasa wewe mbondei unapata hela za bure za ufisadi hata huwezi kuwaza utapataje pesa, wenzio wanafikiria na ndo hivyo wanakuacha.
   
Loading...