Leo nimefarijika sana baada ya Kamanda wa Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZTO), ACP Awadhi Haji kusimamia Sheria na kumwamuru askari wa Usalama Barabarani WP Beatrice alipe faini ilipobainika kuwa alitaka kumbikia kosa la kupita kwenye taa nyekundu Dereva wa Gazeti la JAMHURI.
WP Beatrice alilazimisha kuwa Dereva Leonce Mujuruzi amepita taa nyekundu wakati alipita taa ya kijani baadaye akabadili kauli na kusema yeye alikuwa anaongoza magari hivyo Dereva Leonce hakupaswa kufuata ishara ya taa bali maelekezo ya WP Beatrice.
Katika kikao tulichofanya Ofisi ya ZTO Awadhi leo Aprili 28, 2017 Dar es Salaam, Afande Awadhi amesema amebaini ukweli kuwa WP Beatrice hakufuata utaratibu anaopaswa kufuata askari anaponkamata Dereva kwa kosa analomtuhumi nalo Barabarani.
Nitaandika kwa kina sakata hili kwenye safu yangu ya SITANII Jumanne ijayo katika Gazeti la JAMHURI, ila kwa ufupi amesema askari akimkamata Dereva anapaswa kufanya yafuatayo:-
1. Askari akimkamata Dereva anaangalia aina ya kosa. Adhabu ya kwanza ni ONYO.
2. Adhabu ya pili imegawanyika sehemu mbili. Dereva akikiri kosa, anapigwa faini. Akikataa anapelekwa Mahakamani pande mbili zisikilizwe na haki itendeke.
Katika shauri lililokuwa mbele yetu, WP Beatrice hakumpa fursa Dereva wetu Leonce ya ama onyo au kuchagua kati ya faini au kupelekwa Mahakamani.
In charge wa Police Msimbazi Inspekta Bihemo, alikuwa ameelekeza Dereva Leonce awekwe ndani na kufunguliwa mashtaka kwa kutokana na Leonce kulalamika kuwa WP Beatrice amemwonea.
ACP Awadhi amesema hayupo kutetea Polisi au Raia. Mwenye makosa anawajibika kwa makosa yake. Amebaini WP Beatrice amekiuka wajibu wake hivyo akamwagiza alipe faini aliyokuwa amemwandikia Leonce.
Nitaandika kwa kina kwenye safu yangu ila nampongeza ACP Awadhi. Sisi kama JAMHURI tumekuwa tukipokea malalamiko juu ya uonevu wa askari. Si kwamba hatukuwa na Sh 30,000 za kulipa faini, ila tumejiuliza kama askari ana uwezo wa kutubambikia kesi sisi, inakuwaje kwa wasio na kuwasemea?
Ilitubidi tusimame kutetea haki. Tunamshujuru ACP Awadhi kwa kutetea na kusimamia haki bila uonevu. Tunaamini WP Beatrice na Inspekta Bihemo kuanzia sasa watafanya kazi kwa weledi na kitenda haki kwa kila mmoja.
Asante ACP Awadhi na Mungu akubariki uendelee kusimamia haki, leo, kesho na baadaye.
Balile