Hongera bi. Addy lyamuya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera bi. Addy lyamuya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, Jun 20, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  James Magai


  HAKIMU Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Addy Lyamuya, amesema miongoni mwa kesi ambazo hatazisahau katika maisha yake, ni pamoja na Babu Seya na ya majambazi waliovamia familia moja jijini na kubaka watu wote

  Hakimu Lyamuya aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kutunukiwa cheti cha uwakiliwa wa kujitegemea, katika hafla iliyofanyika Mahakama Kuu ya Tanzania.

  Babu Seya ambaye jina lake halisi ni Nguza Viking na watoto wake Papi Kocha, Viking Francis, Nguza Viking walihukumiwa kifungo cha maisha, baada ya kupatikana na hatua ya kuwabaka wanafunzi kadhaa wa Shule ya Msingi Mapambano, iliyoko Sinza wilayani Kinondoni.

  Akizungumzia kesi hiyo, Hakimu Lyamuya alisema kinachomfanya asiisahau ni kitendo cha kuwahusisha watu wa familia moja jambo ambalo alisema katika hali ya kawaida halitarajiwi kutokea.

  "Kesi hiyo ilikuwa 'Unique' (ya kipekee) maana iliwahusisha watu wa familia moja. Hii ilikuwa halikuwa la kawaida ingekuwa imewahusisha watu tofauti tofauti sawa," alsema Lyamuya ambaye alitoa adhabu hiyo kwa familia ya Nguza.

  "Ingawa watu hawakuamini lakini ndivyo ilivyotokea," alisisitiza.

  Kuhusu kesi ya majambazi, Lyamuya alisema majambazi hao waliivamia familia ya mfanyabiashara mmoja na kisha kuwabaka hadharani, watu wote wa familia hiyo.

  Alisema hataisahau kesi hiyo hasa kwa kitendo cha Mahakama ya Rufaa, kukubaliana na uamuzi alioutoa.

  Alisema katika kesi hiyo aliyoiamua akiwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, aliwahukumu watuhumiwa hao kifungo cha maisha jela.

  Alisema baadaye watu hao walikata rufaa lakini Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa zilikubaliana na uamuzi wake kuwa ulikuwa sahihi.

  Mbali na Hakimu Lyamuya, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali (IGP) Said Mwema pia alitarajiwa kutunukiwa cheti cha uwakili lakini hakuhudhuria sherehe hizo.

  Hata hivyo Msajili wa Mahakama Kuu, Eliaman Mbise alisema hakuwa na taarifa za kutokufika kwa mkuu huyo wa polisi.

  Akimkaribisha Jaji Mkuu, Agustino Ramadhani kuwatunuku vyeti mawakili hao, Mbise alisema kukubaliwa kwa mawakili hao wapya, kutaongeza idadi ya mawakili kutoka 1,138 hadi kufikia 1,168.

  Rais wa Chama cha Wanasheria nchini (TLP), Dk Fauz Twaib, alisema kabla ya kukubaliwa kuwa mawakili wa kujitegemea, mawakili hao walifanyiwa usaili na Baraza la Elimu ya Sheria nchini ambalo mwenyekiti wake ni Jaji Kiongozi na kuridhika kuwa wana uelewa wa kutosha wa sheria za nchi.
  Dk. Twaib alisema baadaye Jaji Mkuu naye aliwafanyia usajili na kuridhika kuwa wanastahili kutumukiwa vyeti hivyo.

  MWANANCHI.
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Hongereni sana wahitimu mje msaidie jamii yetu hasa uelewa wa haki zetu za msingi...ili tujiamini ndani ya nchi yetu.
   
 3. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Shule ya msingi Mashujaa na sio Mapambano...
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu Addy Lyamuya hakuwahi kuwa na matatizo ya rushwa wakati fulani?? au nimefuka?
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hapana Mkuu, huyo alikuwa hakimu mwingine wa Temeke anaitwa Jamila Nzota, ameshakula mvua 11
   
Loading...