Customer care inategemea na tawi! mlimani city wapo vizuri. Nadhani nitafanya survey kwenye matawi mengine pia. Hivyo nitakuwa na nafasi ya kuchangia vema. Kwa sasa itoshe kusema ni benki nzuri.
Nimetoa mada ya kupongeza ,baadhi ya wachangiaji wamenirushia madongo .Tuwe critical thinkers. Tuchambue kwa tafiti na kusoma kama hapa tulitakiwa tupitie financial reports za CRDB dhidi ya Bank hizo nyingine.
CRDB ni benki ya hovyo na hivi ninavyoongea nimeagiza hisa zangu ziuzwe ,sitaki tena.Benki ambayo haiwezi kutoa taarifa sahihi kwa wateja wake hiyo ni benki gani? CRDB ukiomba mkopo kuupata ni kudra za mwenyezi mungu.Kuna upumbavu mwingi crdb na akaunti naenda kuifunga.
Mojawapo ya taasisi nchini inayofanya vizuri kutokana na uongozi ni CRDB tokea ilipoanzishwa imekuwa na mafanikio makubwa na haswa kipindi ikiwa chini ya uongozi wa ndg kimei hadi Sasa ikiwa chini ya ndg Nsekeka.
Hii ni changamoto kwa taasisi nyingine katika sekta za kuhudumia wananchi ziige hii ya CRDB. Sina haja ya kutaja hizo taasisi wengi tunazijua na wenyewe wanajijua.