Honest and humble man needed

Mkuu kuna Thread ulizianzisha Humu Ukiomba Ushauri juu ya Mume wako wa Ndoa Kulewa sana na Kuchelewa kurudi naomba niziandike vizuri kuzilink nimeshindwa.

  1. Mrejesho- hii uliiandika 2015
  2. Ushauri-Mwanaume Anakunywa Pombe mpaka hawezi kufanya tendo la Ndoa.
  3. Hivi inakuwaje hii Wanaume Jamani
  4. Wanaume kuweni wa wazi kwa wake zenu.
Mama Katika Thread zako inaonekana ulifika Mahala ukakubaliana na Maisha ya Mumeo na hukupenda kabisa kugombana naye kwa kuwa kila jitihada zote ulizofanya ni kama vile ulikuwa unachochea kuni. Yaani Kama ni Uhuru Ulimpa vya kutosha Pia Kama ni Kuitunza Familia alikuwa Vizuri Pia.

Mpendwa naomba utusaidie uliamua kubwaga Manyanga au unatafuta wa Pembeni?

Asante na Mungu akubariki sana.
Daaaaaaah..... Anaiendeleza thread yake leo....
 
Anayebadilisha Mtu ni Mungu halafu kumbuka huyo Mungu unayedai kumuabudu anachukia kuachana. Na ukisoma Biblia haikupi mamlaka ya kuolewa tena unapotengana na mumeo ni kifo tu kinawatenganisha. Kuna laana unapoachana na mke/mume wa ujana wako. Mungu habadiliki jamani hata mimi nilikuwa mlevi lakini hakuna mahali mke aliniacha Mungu ndiye aliyenibadilisha. Kumbuka ndoa yenu ni hadi kifo jump in jump out hutopata utakacho kwakuwa Mungu amekiweka kwa mumeo. Soma

Malaki 2:13-16
[13]Tena mnatenda haya nayo; mnaifunikiza madhabahu ya BWANA kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia.
[14]Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu BWANA amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.
[15]Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana.
[16]Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema BWANA wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.
Zingatia hayo mama zingatia sana usije kujuta mbeleni

Kwa iyo mkuu unajarib kumwambia MTOA Uzi kuwa unafaa,ama na unamwogopa Mungu,..!?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom