Homa ya Dengue

Homa ya Dengue

kunguni wa ulaya

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
4,131
Reaction score
6,143
Habari za jioni wakuu,

Napenda tukumbushane tu kuwa mliopo Dar es Salaam, kuna homa ya dengue

Kuna watu kadhaa naishi nao majirani na wengine tunafanya nao kazi imethibitika kuambukizwa na homa ya Dengue.

Hivyo ukisikia maumivu ya Viungo na kichwa ni bora uwahi mapema hospitali ukapate vipimo kuliko kuanza kutumia dawa.

Maana inasemekana baadhi ya vidonge haviruhusiwi kumezwa na mgonjwa wa dengue.

Mamlaka husika pia itapendeza kama wakitoa tahadhari na elimu stahiki kwa umma!
 
wanajikausha wako bize na msafara wa Rais watu wanakufa huku na dengue! shubamit
 
Mbona naibu waziri wa afya alishatangaza kitambo mkuu. Labda ulikuwa Congo.
 
Mwenyewe nilikuwa siamini hadi jana nilipokutana na jamaa yangu mmoja amekata weight mbaya kabisa akaniambia huu ugonjwa ulimlaza.

Siyo la kubeza hili.
 
Maambukizi yake ni kwanjia gani?
Itarahisisha namna ya kujikinga.
 
Back
Top Bottom