Randy orton
JF-Expert Member
- Apr 29, 2019
- 1,338
- 3,541
Sidhani kama kuna mtu mwenye akili timamu anayepinga uwepo wa matangazo kwenye jezi ila wengi wanaopinga wanapinga kwa hoja zifuatazo.
1. Mpangilio wa matangazo, matangazo kwenye jezi ya simba yamekaa hovyo hovyo sana, mengine mgongoni, mengine kwenye kola, mpaka yanapoteza mvuto wa jezi na sidhani kama walikosa muundo mzuri wa kuweka matangazo hayo kwa kuwa end product ni kama bango.
2. Mdhamini mmoja kujirudia mara nyingi, Kampuni moja inajirudia zaidi ya mara tano!! , Utajisikiaje ukivaa jezi ya arsenal halafu fly emrirates ipo mara 6!!
3. Mdhamini mkuu wa Simba anajulikana kuwa ni Sportpesa, kiasi anachokitoa kwaajili ya udhamini kinajulikana, huyu mdhamini mwingine anatoa shilingi ngapi ukilinganisha na idadi anayotokea kwenye jezi ya Simba.?
4. Wakati mwingine sio tu hela watu wanaangalia class, Simba imeshakuwa brand kubwa sana Tanzania, kuna vitu vidogo vidogo vinaweza kushusha hadhi ya kitu hata kama kuna hela inaingia, hivi club kubwa kama Manchester United inayomilikiwa na familia ya Glazer wanashindwa nini kutangaza jina na makampuni yao kwenye jezi, au Chelsea ya Roman Abramovich mbona hatuioni ikitangaza matangazo ya kampuni za mafuta za Roman Abramovich?
Jibu ni kwamba Roman Abramovich na Familia ya Glazer hawashindwi kujaza mitangazo kwenye hizo jezi, isitoshe wao ndio wamiliki kwa kiasi kikubwa, ila kinacholindwa ni hadhi ya hizo clubs ndio maana unawaona wadhamini kama Team Viewer wakijinafasi peke yao kama wadhamini wakuu na wadhamini wadogo wakionekana kwenye sehemu nyingine za jezi vizuri bila kuharibu haiba ya jezi
Itaendelea.