Hoja za kidini "zateka" maoni ya katiba mpya !

MNYISANZU

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
7,048
1,102
* Waislam wataka wimbo wa Taifa ubadilishwe kwani ni wa Kikristo na pia siku za mapumziko zibadilishwe ! * Wakristo nao hawataki mahakama ya kadhi, OIC na uvaaji wa hijab mashuleni. Source: Habari Leo [ Lead story ]. Je, kwa hali hii, ni upi mustakabali wa taifa letu?
 
Duuu ila ndugu zetu ni noumaaa yani hadi mwimbo wa taifa upo kikristo ingawa ni kweli una'sound kama kwaya za kikristo sasa wanataka uwekwe kikaswida au?
 
Duuu ila ndugu zetu ni noumaaa yani hadi mwimbo wa taifa upo kikristo ingawa ni kweli una'sound kama kwaya za kikristo sasa wanataka uwekwe kikaswida au?
Kipi kifanyike ili ku-balance mambo?
 
Mbona wimbo wetu wa taifa unaendana na nyimbo/wimbo wa mataifa mengine mengi tu ya Afrika?
Ina maana katika hizo nchi nyengine hakuna waislam?
 
Mbona kuhusu wakristo wanaoshabiki vimini hamusemi? Coz mtoa mada kasema watoa maoni wanatoa hijab zipigwe maarufuku. Lakin hii hamuiyoni bali mumeona wimbo. Semeni basi kama kuna wakristo wanataka hijab maarufuku ili wavae vimini.
 
Kikwete anavuna alichopanda, UDINI

tatizo ni kubwa zaidi ya tunavyodhani.
Halikuanza wakati wa jk wala mkapa, tangu wakati wa mkoloni ndo lilipoanza.
Tunachoona sasa ni matokeo ya mwanzo tu,
kama taifa tusipochukua hatua madhubuti za maksudi tusitegemee mabadiliko.
 
* Waislam wataka wimbo wa Taifa ubadilishwe kwani ni wa Kikristo

Ha ha haa ili uwe kam hivi sio?

Arabic
كلنـا للوطـن للعـلى للعـلم
ملء عين الزّمن سـيفنا والقـلم
سهلنا والجبـل منبت للرجـال
قولنا والعمـل في سبيل الكمال
كلنا للوطن للعلى للعلم
كلّنا للوطن
شيخنـا والفتـى عنـد صـوت الوطن
أسـد غـاب متى سـاورتنا الفــتن
شــرقنـا قلبـه أبــداً لبـنان
صانه ربه لمدى الأزمان
كلنا للوطن للعلى للعلم
كلنا للوطن
بحـره بــرّه درّة الشرقين
رِفـدُه بــرّهُ مالئ القطبين
إسمـه عـزّه منذ كان الجدود
مجــدُهُ أرزُهُ رمزُهُ للخلود
كلّنا للوطن للعلى للعلم
كلّنا للوطن

Transliteration


Kullunā lil-waṭan, lil-ʻula lil-ʻalam
Milʼu ʻayn az-zaman, saifuna wal-qalam
Sahlunā wal-jabal, manbitun lir-rijāl
Qawlunā wal-ʻamal fī sabīl-el-kamāl
Kullunā lil-waṭan, lil-ʻulā lil-ʻalam,
Kullunā lil-waṭan
Šayḫunā wal-fatā, ʻinda ṣawṭ-il-waṭan
ʼUsdu ġhaben matā, sāwaratn-āl-fitan
Šarqunā qalbuhu, ʼabadan Lubnān
Ṣānahu rabbuhu, li-madā-l-azmān
Kullunā lil-waṭan, lil-ʻula lil-ʻalam,
Kullunā lil-waṭan
Baḥruhu barruhu, durratush-sharqayn
Rifduhu birruhu, māliʼu l-qutbayn
ʼIsmuhu ʻizzuhu, munzu kāna-l-judūd
Majduhu ʼarzuhu, ramzuhu lil-ḫulūd
Kullunā lil-waṭan, lilʻula lil-ʻalam
Kullunā lil-waṭan

English Translation


All of us! For our Country, for our Flag and Glory!
Our valor and our writings are the envy of the ages.
Our mountain and our valley, they bring forth stalwart men.
And to Perfection we devote our words and labor.
All of us! For our Country, for our Flag and Glory!
All of us! For our Country
Our Elders and our children, they await our Country's call,
And on the Day of Crisis they are as Lions of the Jungle.
The heart of our East is ever Lebanon,
May God preserve him until the end of time.
All of us! For our Country, for our Flag and Glory!
All of us! For our Country
The Gems of the East are his land and sea.
Throughout the world his good deeds flow from pole to pole.
And his name is his glory since time began.
The cedars are his pride, his immortality's symbol.
All of us! For our Country, for our Flag and Glory!
All of us! For our Country
 
Mbona kuhusu wakristo wanaoshabiki vimini hamusemi? Coz mtoa mada kasema watoa maoni wanatoa hijab zipigwe maarufuku. Lakin hii hamuiyoni bali mumeona wimbo. Semeni basi kama kuna wakristo wanataka hijab maarufuku ili wavae vimini.

nyani haoni kundule mkuu,
we hujui?
Hapa mada itakuwa ni wimbo wa taifa na siku za mapumziko, yakwao hawayasemi.

Fungua macho yako ndugu,
Umesahau kauli ya mch msigwa bungeni kuhusu serekali ya znz kuwabana watu ktk mavazi hasa mwezi wa ramadhani?
 
Habari yenyewe hii hapa
UHURU uliotolewa wa kutoa maoni yoyote ili kuunda Katiba ijayo kwa manufaa ya Watanzania wote, umetekwa na viongozi wa makanisa na misikiti, ambao wametuma waumini wao kutoa maoni ya kutetea misimamo ya dini husika iingie au isiingie katika Katiba.


Hali hiyo imejidhihirisha wiki iliyopita mkoani Ruvuma na hasa katika Wilaya ya Songea mjini, ambapo Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya, ilijikuta ikisikiliza maoni ya aina moja yakijirudia zaidi ya mara kumi katika kila mkutano huku watoaji wa maoni hayo wakionesha kutumwa kuwakilisha maoni waliyotumwa.


Hata hivyo wakati wakisisitiza kuwa Serikali haina dini, waumini hao walijikuta wakitoa maoni kutaka Serikali isiyo na dini itambue dini zao na kutii matakwa yao yanayopinga kinachodaiwa ni maslahi ya dini nyingine.


Matakwa ya Waislamu Waislamu katika matakwa yao, walisisitiza Serikali pamoja na kutokuwa na dini, iajiri watumishi kwa uwiano sawa kwa kuzingatia dini na kugawa maeneo vikiwemo viwanja na majumba yasiyotumika kwa usawa huo huo.


Mbali na kusisitiza madai ya siku nyingi ya Waislamu ya kutaka Mahakama ya Kadhi na Tanzania kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC), pia walipendekeza kufutwa kwa Wimbo wa Taifa na siku ya Ijumaa kuwa ya mapumziko kama Jumapili na Jumamosi, au itafutwe siku nyingine ya mapumziko lakini siyo Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.


Kumejitokeza pia madai ya kutaka usawa katika siku za sikukuu za dini, yaani Idd El Fitri na Idd Al Haj zipewe siku za mapumziko zaidi ya tano kwa kila sikukuu na kutambuliwa kwa Mwaka Mpya wa Kiislamu. Katika kutetea hoja hiyo, mkazi wa Kata ya Lizaboni, Haji Nditi (44), alipendekeza siku za kupumzika za Serikali ziwe katikati ya wiki.


Nditi alisema pendekezo lake, linalenga kuondoa ubaguzi wa siku za kuabudu kwa madai kuwa Ijumaa ambayo ni Siku ya kuabudu kwa Waislamu, imebaguliwa kwa kuwa siku ya kazi wakati Jumamosi na Jumapili, zimependelewa kuwa za mapumziko.


Hata hivyo mmoja wa Waislamu ambaye hakutaka kutajwa jina, akizungumza na gazeti hili, alifafanua kuwa hoja hiyo si kwa mujibu wa Korani, kwa kuwa kitabu hicho kitakatifu, kimeagiza baada ya Ibada, Waislamu watawanyike kwenda kutafuta riziki.


Mkazi wa Mji Mwema, Salehe Seif alisema Mahakama ya Kadhi inapaswa kutambuliwa na Katiba ili ipate nguvu ya utendaji, ikiwemo kukamata Waislamu wanaokaidi amri zake.


Alisema pia si busara Muislamu kufungishwa ndoa na Abdalah (Shehe msikitini) na kuvunjwa kwa ndoa hiyo, kufanywe na Paulina (Hakimu mahakamani).


Mkazi wa Kata ya Makumbusho, Ally Kumchoma (52), alisema kuwa Kadhi asipotambuliwa na Katiba, akitoa hukumu inaweza isitekelezwe kwa kuwa hatambuliki kiserikali na anaweza hata kushitakiwa.


Kuhusu kujiunga na OIC, Seif alisema kutasaidia Waislamu na wasio Waislamu kupata mikopo bila riba ambayo ni neema kwa wote.


Mkazi wa Kata ya Makumbusho, Yahaya Mpingi (52) alipendekeza Mwaka Mpya wa Kiislamu utambulike na kuwe na mapumziko kama mwaka mpya uliozoeleka na kutaka Serikali iajiri Wakristo nusu na Waislamu nusu.


Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu cha St Augustino, Jasmin Ulambo (22), alipendekeza vazi la Hijab liheshimiwe na katika Sensa ya Watu na Makazi, kipengele cha dini kiwepo.


Mkazi wa Kata ya Majengo, Nahodha Mpaka (76), alipendekeza Serikali isiingilie uhuru wa kuabudu na kutoa mfano wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), kwamba limeundwa na Serikali kudhibiti Waislamu. Hamisi Njovu (36), mkazi wa Kata ya Majengo, alipendekeza OIC Tanzania ijiunge lasivyo ijitoe Vatican.


Hata hivyo hakufafanua kwa nini Tanzania imuondoe Balozi wa Vatican ambayo ni nchi ya kidini na isimuondoe Balozi wa Iran ambayo pia ni nchi ya kidini. Njovu pia alipendekeza Wimbo wa Taifa ufutwe kwa madai kuwa ni wa dini moja.


Alipoulizwa na Profesa Baregu afafanue, alisema Mungu Ibariki Tanzania, ni wimbo unaotumika makanisani wakati wakianza ibada.


Alitaka pia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utambue wake wanne na watoto wanaotokana na wake hao kwa kuwa Waislamu wameamrishwa kuoa wake zaidi ya mmoja. Mkazi wa Kata ya Bomba Mbili, Abdul Ramadhani (74), alisema Sikukuu ya Pasaka, ina siku sita, yaani Jumatano ya Majivu, Alhamisi Kuu, Ijumaa Kuu, Jumamosi, Jumapili na Jumatatu ya Pasaka ambazo Wakristo hupumzika.


Alisema Waislamu katika Idd, wamekuwa wakipewa siku moja au mbili na kutaka kuwe na usawa. Hoja za Wakristo Wananchi wengi waliotoa maoni walitaka uhuru wa kuabudu kama ulivyo katika Katiba ya sasa, ubaki hivyo hivyo na kupinga kufutwa kwa Wimbo wa Taifa, Tanzania kujiunga OIC na Mahakama ya Kadhi kuingizwa katika Katiba.


Pia walipinga vazi la Hijab kuvaliwa katika ofisi za Serikali, ajira kwa kuzingatia vigezo vya dini na kupendekeza uchaguzi usifanyike siku za ibada ikiwemo Ijumaa, huku wakifafanua kuwa umekuwa ukifanyika mara nyingi Jumapili.


Hata hivyo hawakufafanua kwa nini wanapinga uchaguzi siku hiyo, wakati ibada za Wakristo Jumapili hufanyia nyingi katika nyakati tofauti kuruhusu watu kuchagua muda wa kuingia ibadani na muda wa kwenda kazini.


Ayubu Bilal wa Kata ya Majengo, alisema machinjio yameshikwa na dini moja na visu vimeandikwa Bismillah na kupendekeza upande mwingine wa visu uandikwe Kwa jina la Baba, la Mwana na Roho Mtakatifu.


Hata hivyo tofauti na ilivyo kwa Waislamu, Wakristo hawana mwiko wa kuchinja na hata akichinja Muislamu, Mkristo atakula nyama bila wasiwasi.


Mkazi mwingine wa kata hiyo, Charles Wambura, aliyeanza na salamu ya Bwana Yesu ni Mkombozi wa Dunia, apewe sifa, alipinga suala la OIC, alisema haipaswi kuhusisha nchi, hasa kwa sababu ya misaada, badala yake ijulikane na upande wa pili wa hasara kabla ya kuamua. Naye Daniel Sanga (27), alipendekeza Mahakama ya Kadhi isiingizwe katika Katiba na Tanzania isijiunge na OIC.


Katika Kata ya Majengo, baadhi ya wanawake walichukua fomu za kutoa maoni ya Katiba kwa maandishi na kumpa mtu mmoja, aliyeandika kwa niaba yao maoni yaliyofanana, jambo ambalo Tume ililishtukia na kuziweka sehemu moja ili zitambuliwe kama maoni ya mtu mmoja.


Tume, katika timu iliyokuwa na wajumbe watatu; Profesa Baregu, Al Shaimar Kwegyir na Alli Saleh, ilikamilisha kazi ya kukusanya maoni mkoani Ruvuma mwishoni mwa wiki ambapo Jumatatu ya wiki ijayo, itaanza kazi hiyo katika mikoa mingine.

My take :: Kwa kiasi kikubwa watu wengi inaonekana wako-misinformed, hebu angalia baadhi ya sehemu nilizo-highlight.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom