Hoja za Dk. Slaa zipimwe

Hoja za Dk. Slaa zipimwe

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
JUZI, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, alijitokeza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya takriban mwezi mmoja hivi wa ukimya, na kuibuka na zile alizodai kuwa ni vielelezo (ushahidi) juu ya tuhuma mbalimbali zinazomkabili Edward Lowassa.

Katika mtindo ule ule uliozoeleka wakati akiwa Mbunge wa Karatu, Dk. Slaa alizungumza kwa ufasaha na kwa kujiamini huku akisapotiwa na nyaraka zake mwenyewe za kuthibitisha tuhuma hizo dhidi ya mgombea urais wa Ukawa.
Aliyoyazungumza si mageni sana masikioni mwa Watanzania wengi, ila ni msisitizo tu wa kile kilichokuwa kikidaiwa cha kutokuwapo ushahidi wa tuhuma kadhaa zilizokuwa zikielekezwa kwa Lowassa zinazoweza kusababisha kushitakiwa kwake au kumpotezea sifa za kuwa Rais bora wa Tanzania.

Kwa mwanasiasa aliyedumu kwa zaidi ya miaka 10 kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa chama kikubwa kama Chadema, anayeheshimika ndani na nje ya nchi, kusimama hadharani na kuzungumza mambo mazito kama hayo, haistahili kumpuuza hata kidogo.

Iwe ametumika, ametumiwa au amejituma bado hoja zake zinapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari nzito na kuzijadili kwa kina ili kupata majawabu sahihi kwa kuwa yeye si Mtanzania wa kawaida sana kwani amekuwa kwenye uongozi wa juu ndani ya siasa kwa miaka mingi sana na kwa vyovyote vile kuna anayoyafahamu.

Hatutaki kuamini hata kidogo kwamba chuki binafsi kati ya watu hawa wawili, Dk. Slaa na Lowassa, ni miongoni mwa mambo yaliyomsukuma kuzungumza kama alivyozungumza juzi au uchu wa madaraka na ukubwa ndio uliosababisha hayo yote kuwekwa hadharani.

Hoja ni je, yana ukweli kiasi gani? Kama ni ya uongo, ni kwa nini aliyatoa hadharani? Kwa nini asishitakiwe kwa kuhatarisha amani? Na kama yana ukweli, utaathiri vipi mustakabali wa kisiasa na kijamii wa taifa letu?

Haja za Dk. Slaa na maswali haya ndivyo vinavyotufanya kuwataka wahusika (Lowassa na wenzake) watoe majawabu, wajisafishe ili kuondoa shaka mioyoni mwa Watanzania na kudhihirisha uadilifu wao kwa taifa.

Raia Tanzania Tahariri
 
Huyo Slaa aliyesaliti hata watoto wa kiuno chake?..! STUPID
 
Alichonifurahisha jana Star Tv ni kusema Maghufuli arejeshe kwanza nyumba ya serikali aliyompa mwanamke wake,hakika huo ni ufisadi uliotukuka.Akiingia ikulu atahonga mpaka pesa za BOT
 
Hoja ya Dr. Slaa kuhusu Lowasa kujisafisha ni nzuri sana, tatizo huo Muda wa kujisafisha haupo na kufanya hivyo kutatuchelewesha kufanya mabadiriko.
Tuko na hoja moja ya msingi sana nayo ni kufanya mabadiriko, haijalishi nani anagombea kupitia ukawa hata ingekuwa ni jiwe lisoweza hata kuongea bado lingetosha kukidhi kiu ya watu wengi "mabadiliko".
Tumefundishwa kuwa mabadiriko hayakwepeki hivyo ni suala la muda tuu, tuanze kuanzia Haiti na fika zetu kukubali mabadiriko, yakifika tusiwe wagumu kuyakubali ili hisije kuwa shida.
 
Alichonifurahisha jana Star Tv ni kusema Maghufuli arejeshe kwanza nyumba ya serikali aliyompa mwanamke wake,hakika huo ni ufisadi uliotukuka.Akiingia ikulu atahonga mpaka pesa za BOT

Angekuwa anawapiga Wagombea wote tungemwelewa,sasa ameelekeza mashambulizi kwa mtu mmoja kwa tuhuma za mwaka 47 ambazo amepewa nyaraka na Serikali bila Shaka,mtu wa kawaida huwezi kupata documents za Scotland Yard au contents za kitu alichojaza mtu tume ya maadili! Dr Mihogo inabidi akamatwe kwa kuwa na nyaraka kama hizo,anatishia nazo watu,waliompa kwanini hawapeleki huo ushaidi Mahakamani?!! je za kwao wanaomtumia Wamempa Huyo Dr Mihogo? Tundu lisu alishamjibu hahitaji majibu zaidi.
 
We dont have time to waste on Slaa, No one will change our minds , It is not a rocket science to understand his position athe is just like a renegade soldier
 
We dont have time to waste on Slaa, No one will change our minds , You dont need a rocket science to understand his position at the moment , he just like a renegade soldier
 
JUZI, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, alijitokeza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya takriban mwezi mmoja hivi wa ukimya, na kuibuka na zile alizodai kuwa ni vielelezo (ushahidi) juu ya tuhuma mbalimbali zinazomkabili Edward Lowassa.

Katika mtindo ule ule uliozoeleka wakati akiwa Mbunge wa Karatu, Dk. Slaa alizungumza kwa ufasaha na kwa kujiamini huku akisapotiwa na nyaraka zake mwenyewe za kuthibitisha tuhuma hizo dhidi ya mgombea urais wa Ukawa.
Aliyoyazungumza si mageni sana masikioni mwa Watanzania wengi, ila ni msisitizo tu wa kile kilichokuwa kikidaiwa cha kutokuwapo ushahidi wa tuhuma kadhaa zilizokuwa zikielekezwa kwa Lowassa zinazoweza kusababisha kushitakiwa kwake au kumpotezea sifa za kuwa Rais bora wa Tanzania.

Kwa mwanasiasa aliyedumu kwa zaidi ya miaka 10 kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa chama kikubwa kama Chadema, anayeheshimika ndani na nje ya nchi, kusimama hadharani na kuzungumza mambo mazito kama hayo, haistahili kumpuuza hata kidogo.

Iwe ametumika, ametumiwa au amejituma bado hoja zake zinapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari nzito na kuzijadili kwa kina ili kupata majawabu sahihi kwa kuwa yeye si Mtanzania wa kawaida sana kwani amekuwa kwenye uongozi wa juu ndani ya siasa kwa miaka mingi sana na kwa vyovyote vile kuna anayoyafahamu.

Hatutaki kuamini hata kidogo kwamba chuki binafsi kati ya watu hawa wawili, Dk. Slaa na Lowassa, ni miongoni mwa mambo yaliyomsukuma kuzungumza kama alivyozungumza juzi au uchu wa madaraka na ukubwa ndio uliosababisha hayo yote kuwekwa hadharani.

Hoja ni je, yana ukweli kiasi gani? Kama ni ya uongo, ni kwa nini aliyatoa hadharani? Kwa nini asishitakiwe kwa kuhatarisha amani? Na kama yana ukweli, utaathiri vipi mustakabali wa kisiasa na kijamii wa taifa letu?

Haja za Dk. Slaa na maswali haya ndivyo vinavyotufanya kuwataka wahusika (Lowassa na wenzake) watoe majawabu, wajisafishe ili kuondoa shaka mioyoni mwa Watanzania na kudhihirisha uadilifu wao kwa taifa.

Raia Tanzania Tahariri

Hoja za dk. Slaa ni nzito siyo tu hazijibiki lakini pia hazina uwezo wa kujibiwa na watu wa ziro waliozoea siasa za mtaroni na uongo

Slaa ni mtu makini sana. Alijua kuwa lowasa hasafishiki hata kwa msasa wa chuma
 
...mkuu unamaanisha apimwe akili au ubongo ? em fafanua kidogo....
 
No time at all.We wasted time a lot with him now...no..Since he cannot cath with us anymore..
 
Hoja za dk. Slaa ni nzito siyo tu hazijibiki lakini pia hazina uwezo wa kujibiwa na watu wa ziro waliozoea siasa za mtaroni na uongo

Slaa ni mtu makini sana. Alijua kuwa lowasa hasafishiki hata kwa msasa wa chuma

Kama alikuwa na hoja kama hizo angejiuzuru kabla LOWASA hajaja Chadema, angeeleweka na kujibiwa! tumia kichwa kwaajili ya kufikiria kama thinker tank,usilete mihemko humu
 
Hoja za dk. Slaa ni nzito siyo tu hazijibiki lakini pia hazina uwezo wa kujibiwa na watu wa ziro waliozoea siasa za mtaroni na uongo

Slaa ni mtu makini sana. Alijua kuwa lowasa hasafishiki hata kwa msasa wa chuma

Kama ulimsikiliza Dr jana mahojiano na Star tv akasema matamanio ya urais yalishateka nafsi yake. Na alisema hilo limechangia yale anayoyasema. Sasa nani asiyejua kuwa kinachoendelea ni ile dhana ya waswahili "heri tukose wote"?

Halafu katika press ile ya kwanza alishafananisha chama au mfumo aliotokea Lowassa na choo. Na sasa anataka tuamini kuwa mtu ambaye bado yumo chooni humo anaweza kuwa safi kuliko aliyekwishatoka humo?

Tafakari!!
 
Back
Top Bottom