Baada ya hapo jana Askofu Gwajima kutoa ushauri na maoni juu ya mambo mbali mbali yanayoendelea nchini, wameibuka wanafiki machawa na wasema ovyo humu Jf kutaka kuushawishi umma kuwa katika hoja za Gwajima kuna ukabila na udini.
Jambo hili ni hatari na baya mno kwa amani, umoja na Mshikamano wa Taifa letu
Aidha mitazamo ya aina hii ikiachwa iendelee inafifisha kama si kuondoa kabisa haki ya raia kutoa maoni.
Katika ujumbe wake kwa Serikali, hakuna mahali popote aliposema watu wasiende kupiga kura, hakuna mahali popote aliposema kwa vile nchi hii Kiongozi wake ni Muislamu, Wakristo wasiende kupiga kura, hakuna!
Alichojaribu kuonyesha ni kwamba makando kando yaliyopo baina ya Serikali na baadhi ya Taasisi za dini ikiwa ni pamoja na Kanisa lake yasipopatiwa ufumbuzi, waumini wake wanaweza wasipigie CCM kura? Kuna kosa gani hapo?
Gwajima kasema wapo wanaolia na kuomboleza kwa ajili ya ndugu zao waliopotea hawajulikani walipo, wengine wameuawa, wengine wamepigwa. Haya mambo hayapo? Anaposema yakomeshwe na kwamba yasipokomeshwa wahanga wanaweza wasipigie kura Chama chake, Kuna kosa gani hapo??
Gwajima anaposema tunaenda kwenye Uchaguzi wengine wamo gerezani, Chama chao kwa sababu hizi na zile Chama chao kipo kama halipo, anapotoa rai kuwepo kwa maridhiano ya kitaifa ili kujenga heshima ya Chama, umoja Mshikamano wa kitaifa Hilo ndilo kosa??
Hakuna udini wala ukabila kutokana na hoja za Gwajima ispokuwa Kuna watu kwa sababu zao wanaleta vioja na uzushi kuwa Kuna elements za ukabila na udini kwenye hoja za Gwajima.
Wengine wanasema Gwajima hana haki ya kusema haya eti kwa vile hata wakati wa JPM Makanisa yalifungwa na watu walitekwa na.kuuawa, alikuwepo na hakusema. Hizi si hoja baali vioja tupu.
Sawa, hakusema wakati huo lakini Sasa kasema. Hilo ni kosa? Wewe ambaye ulikuwepo wakati ule yanatendeka hayo hukusema, na Sasa yanatendeka husemi tena unakosoa wanaoyasema, nani mwenye akili??
Tuache unafiki, mnafiki ni mbaya kuliko mchawi, viongozi wetu siyo Malaika wanakosea kama sisi sote. Tunapokataa ukweli huu, tunajidanganya na kujazana ujinga!