Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,143
Wewe Mkuu Bongolander umeipitia Rasimu? Inataja Marais wangapi?Unahitaji kupitia tena rasimu
Wewe Mkuu Bongolander umeipitia Rasimu? Inataja Marais wangapi?
Wewe Mkuu Bongolander umeipitia Rasimu? Inataja Marais wangapi?
Ni kweli Mkuu Bongolander.Lakini,hata Serikali zilizopo sasa ikisemwa zigawanywe zitatoka Serikali ngapi? Idadi ya waunda-serikali itawekwa na Katiba husika ya Tanzania Bara na Zanzibar. Halafu, hakutakuwa na matumizi yatakayozidi mapato ya Serikali.Hofu inatoka wapi kabla ya kuijadili KATIBA?Mkuu suala hapa sio nani kuwa rais, suala ni serikali. Kama mkuu wa serikali ataitwa Waziri, gavana au mkuu, haina maana kuwa hiyo sio serikali.
suala ni mamlaka, madaraka, nguvu , raslimali nk za hizo serikali. Hata kama wakiita jimbo la Tanganyika na mkuu wake akaitwa mkuu wa mkoa jimbo la Tanganyika, kama likiwa na bunge, makahama, jeshi na raslimali nyingine nyingi ambazo Rais wa Jamhuri ya Tanzania atazitegemea....basi kiongozi wa hilo jimbo atakuwa na nguvu kuliko rais.
Suala ni serikali tatu, sio marais watatu.
Mkuu wangu swala la serikali 3 halina Ubishi. Ni lazima kila serikali itakuwa na kingozi wake sasa umuite Rais, sijui waziri kiongozi, au Waziri mkuu (Premier), senator bado nafasi hizo tatu (kiongozi wa Znz, Kiongozi wa Bara na Kiongozi wa muungano)zinahitajika na watavuta mshahara sawa na marais iwe kwa jina lolote.Hoja hii iliyo katika Rasimu ya Pili ya Katiba iliyokabidhiwa kwa Rais Kikwete na Rais Shein na kutetewa ipasavyo na Jaji Warioba inapotoshwa sana. Inaandamwa na propaganda.Mojawapo ni kuwa na Marais watatu! Nani amesema (au Rasimu gani iliyopendekeza Marais watatu)? Huu ni upotoshaji.
Rasimu ya Jaji Warioba inahusika na suala moja kuu:Serikali ya Muungano. Ni Tanzania tu na si Zanzibar wala Tanganyika. Kwakuwa Rasimu inazungumzia namna Serikali ya Muungano itakavyokuwa,ndiyo maana Serikali za Zanzibar na Tanganyika (iliyoitwa Tanzania Bara) zinadokezwa. Mantiki hapa ni kuwa Tanzania itakuwa moja lakini yenye Serikali tatu. Moja ni zao la muungano (Serikali ya Muungano).Ya pili ni Serikali ya Tanzania Bara (kama mshiriki wa muungano) na Serikali ya Zanzibar(mshiriki mwingine wa muungano).
Kinachozaa propaganda zote hizi dhidi ya serikali tatu ni Urais. Vipo vyama na watu wenye 'airtime' kwenye vyombo vya habari na Serikalini waliojaa mawazo ya 'Urais' tu. Wakilala-urais;wakiamka-urais. Wanapotosha hoja kwa kusema kuwa Tanzania itakuwa na Marais watatu. Si lazima kuwa na Marais watatu. Mbona Ujerumani yenye Serikali za Majimbo 16 haina Marais 17? Marekani kuna utawala wa aina hiyo hiyo lakini Rais mmoja.
Hakuna hata Ibara moja ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba inayopendekeza muundo wa Serikali za Tanzania Bara na Zanzibar. Wasingeweza kupendekeza hivyo kwakuwa hiyo haikuwa kazi yao.Wao walikuwa kimuungano. Mfumo na ukubwa wa Serikali za Tanzania Bara na Zanzibar vimeachwa kwa wahusika wenyewe. Watafanya hivyo na watakavyo iwapo Rasimu ya Muungano itapitishwa kama inavyopendekeza.
Hakuna hata Ibara moja ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba iliyopendekeza aina ya viongozi wa Serikali za Tanzania Bara na Zanzibar;kama ziongozwe na Marais,Mawaziri Wakuu,Wafalme au Wakuu wa Mikoa. Hii hoja ya Marasi watatu inatokea wapi zaidi ya kuwa upotoshaji wa Rasimu?
Wengi wetu tunajua,tunatambua na kuthamini kazi ya Tume ya Jaji Warioba. Imewasikiliza watanzania na kuandika maoni yao juu ya Katiba yao katika Rasimu. Wao wameandika tu maoni ya watanzania. Yeyote atakayejaribu,kulazimisha au kushawishi kuchakachuliwa kwa maoni hayo,hatabaki salama. Huo ndio ukweli. Kadiri muda unavyokwenda,ndivyo tunavyoendelea kuwaona wapotoshaji na kujiandaa kuwashughulikia.
Time will tell!
Mkuu wangu swala la serikali 3 halina Ubishi. Ni lazima kila serikali itakuwa na kingozi wake sasa umuite Rais, sijui waziri kiongozi, au Waziri mkuu (Premier), senator bado nafasi hizo tatu (kiongozi wa Znz, Kiongozi wa Bara na Kiongozi wa muungano)zinahitajika na watavuta mshahara sawa na marais iwe kwa jina lolote.
Kwa hiyo iwe rasimu imeacha ama vyovyote bado haiwezekani kuundwa serikali ikakosa mkuu wa nchi hiyo! ni logic tu mkuu wangu. Na pia ufahamu kila serikali itakuwa na mawaziri na wabunge wa kujaza serikali zote 3 haihitaji sayansi kutambua hilo maana tunaunda serikali inayofanana na serikali za nchi nyinginezo. Hivyo tutakuwa na mawaziri wa Tanganyika (bara) na wabunge wake wa majimbo kama ilivyo leo Zanzibar halafu tuna mawaziri na wabunge wa bunge Jamhuri (muungano). Hatuwezi kuwa na serikali 3 isokuwa na vyombo hivyo!
sawa lakini viongozi watatu wa serikali hizo tatu watakuwepo au sio?Mkuu Mkandara,hoja yangu kuu ni kuwa si lazima katika uwepo wa Serikali tatu kuwepo Marais watatu
Sahihi Mkuu,ndivyo itakavyokuwa.Lakini,ukubwa wa Serikali husika na matumizi yake ni maamuzi ya waunda Katiba za Serikali hizosawa lakini viongozi watatu wa serikali hizo tatu watakuwepo au sio?
wewe kama mwananchi iwe wa Bara au visiwani unafikiri uundwaji wa serikali hizi utafanywa kama unavyopenda iwe? au hao hao watarajiwa wenye nafasi zao (viongozi) watajipangia madaraka!Sahihi Mkuu,ndivyo itakavyokuwa.Lakini,ukubwa wa Serikali husika na matumizi yake ni maamuzi ya waunda Katiba za Serikali hizo
Ni hawa hawa wa SIRI na DHAHIRIwewe kama mwananchi iwe wa Bara au visiwani unafikiri uundwaji wa serikali hizi utafanywa kama unavyopenda iwe? au hao hao watarajiwa wenye nafasi zao (viongozi) watajipangia madaraka!
Kifupi nini nafasi yako ktk uundwaji wa serikali hizo?
Hii ndio sababu mimi napinga serikali 3 kwa sababu nawajua viongozi tulokuwa nao, wao wanafikiria maslahi yao na kuwapa serikali 3 ni kuwapa fursa sisi wenyewe kujipangia madaraka na ulaji.Ni hawa hawa wa SIRI na DHAHIRI