Hoja ya kumfuta Nape Nnauye uanachama CCM

Hoja ya kumfuta Nape Nnauye uanachama CCM

Mkara-tu

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2018
Posts
224
Reaction score
221
nape.jpg


Uamuzi wa mtu kuwa mwanachama wa chama cha siasa ni utashi wa mtu. Vile vile ni jambo jema kukusoana ndani na nje ya chama as long as ni constructive criticism.

Hapana shaka Nape Nnauye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Rais Magufuli tangu aondolewe kwenye nafasi ya uwaziri, amabaye pia ni mwenyekiti wa chama chake. Pasipo mashaka yoyote, sehemu kubwa ya ukosoaji wa Bw. Nape hauna tija kwa chama chake, ingawa anapenda kukisemea chama chake kama msingi wa ukosoaji wake.

Sihitaji kutaja maeneo mbali mbali ambayo Nape Nnauye ametoa matamko yanayo lenga kupingana na Rais Magufuli. Hii imepelekea baadhi ya watu au wanachama wa CCM kutoa maoni au hisia zao kwamba Bw. Nape Nnauye afukuzwe uanachama wa CCM. Nadhani matamanio haya ya kufukuzwa uanachama siyo sahihi.

Kimsingi, mimi naamini uteuzi wa Bw. Nape Nnauye kuwa katika baraza la mawaziri ya Serikali ya Rais Magufuli hapo awali haukuwa uamuzi wa Rais Magufuli.

Ninahisi ilikuwa ni shinikizo la kichama, kwasababu ya nafasi aliyokuwa nayo Nape wakati wa kampeini za uchaguzi mkuu. Yeye mwenyewe alidai kwamba amepigania uteuzi wa Rais Magufuli at the time. I have no doubt Bw. Nape Nnauye is not kind of a guy intellectual enough kuwepo kwenye teuzi za mwanzo za Rais Magufuli.

Ieleweke kwamba CCM ina tabia ya kutoa fadhila kwa watoto wa viongozi mashuhuri wa chama waliopita hata kama hawana ubora wa uongozi kama baba zao. In this case, Nape is good example. This has to stop.

Kwa wale wanaoelewa mchango wa Mzee Moses Nnauye katika taifa kama askari na kama kada wa chama wanakumbuka. Nape Nnauye huyu wa sasa anadhani kwenda kwenye majukwaa na kusema lolote analosema ndiyo uongozi, ndiyo siasa, ndiyo msimamo wa chama hata kama it lacks common sense at best. Ni mzuri wa kelele kuliko busara. Inaonekana wazi kwamba anatanguliza chuki kwa utenguzi wake kwenye nafasi ya uwaziri kuliko mantiki za hoja zake.

In the meantime Bw. Nape Nnauye ana platform ya kutumia nafasi yake ya ubunge kumkosoa Rais ili kuwa relevant in the eyes of the public. Badala ya watu kufikiria kumfukuza uanachama, CCM ijipange kumtoa kwenye hiyo platform kwa kumtafuta the right candidate atakayewawakilisha wananchi wa Mtama na ajenda za CCM kitaifa.


Then, things will fall apart.
 
Mkampime mkojo miinzi ya bwana , mkuu apingwi sababu hakosei
 
Huyu mwenyekiti na Nape wanatofautiana nini kichama kukijua na kukifia chama?
 
Nimesoma sioni hoja yoyote zaidi ya ujazo wa maneno meengiiii ya upofu na yanayoshindwa kusimamavki madhubuti katika hoja yako. Ushauri hoja hujibiwa kwa hoja...nape katoa hoja kama mtu was kusini na mwana CCM anaeelewa maana ya ilani ya chama chake walioiuza kwa wananchi....
 
CCM haigopi mtu ndio uzuri huo...inaweza ikakuacha ukiuke taratibu unavyotaka ila mwisho wa siku utanyooshwa kwenye kamati husika.

NANI ALIYESUMBUA KAMA LOWASSA?
 
Dosari za hoja za Nape ni kuvuliwa uwaziri hata aongee point gani kwa nchi hii kuwaelewa ccm si kazi sana.

Wakosoe tu utawaona
 
Kama ccm itawakataa wakosoaji wa vyama vya upinzani. Halafu tena ikawakataa hata wakosoaji wake yenyewe. Sipati picha litakuwa lichama la namna gani. Ngoja tuendelee kulisubiri hili picha la kihindi.
 
Back
Top Bottom