Hoja siyo kujiunganishia umeme, hoja ni sababu ya kujiunganishia

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Hakuna suala linalonikera kama kuona baadhi ya Watanzania wakikamatwa kwa kosa la kujiunganishia umeme.

Nimeshangazwa na kusikitishwa sana na habari kutoka ITV ambayo inaonyesha wananchi wa Arusha wakikamatwa kwa sababu wamejiunganishia umeme bila ridhaa ya TANESCO.

Kadhia ya Arusha kwa baadhi ya wananchi kujiunganishia umeme ni tip of the iceberg kuhusu ukubwa wa tatizo nchini hasa ikichukuliwa kuwa kuna viongozi wa dini na serikali ambao wamejiunganishia umeme bila ridhaa ya TANESCO. TANESCO hawajiulizi kwa nini mpaka viongozi wa dini wameamua kuiba umeme?

Gazeti la The Citizen la Desemba 27, 2015 lilihabarisha kuwa, TANESCO mkoa wa Arusha pekee ilipoteza kiasi cha shilingi milioni 200 kutoka Januari 2015 mpaka Desemba 2015 kutokana na wananchi kujiunganishia umeme bila ridhaa ya TANESCO. Kwa Dar es Salaam ni zaidi ya shilingi milioni 700.

Kwa sasa tuna shirika la umeme nchini ambalo badala ya kuhangaika na chanzo cha tatizo, linahangaika na matokeo ya tatizo. Tatizo la TANESCO halina tofauti na tatizo la Mamlaka ya Majisafi na Majitaka nchini.

TANESCO hawajiulizi na kupata majibu ya sababu ya wananchi kujiunganishia umeme bali wanatumia nguvu kubwa na rasilimali (resources) nyingi kutafuta wananchi wanaojiunganishia umeme.

Huhitaji kwenda kusomea Ph.D kufahamu faida kubwa ya TANESCO kuwaunganishia wananchi umeme bila malipo (bure) kuliko hasara yake hasa ikichukuliwa kuwa TANESCO ina ukiritimba (monopoly) nchini katika kuuza umeme kwa watumiaji. Kwa kigezo hiki wananchi wengi wataunganisha umeme na matokeo yake TANESCO itakusanya pesa nyingi zaidi kutokana na malipo ya matumizi ya umeme.

Tatizo la msingi kwa Watanzania siyo gharama ya kutumia umeme bali ni gharama ya kuunganishiwa umeme.

Huhitaji kuwa na Ph.D kufahamu kuwa mtu akiunganishiwa umeme hawezi kukubali kuishi bila umeme ndani ya nyumba au kazini kwa muda mrefu kwa sababu LUKU haina salio. Kuunganishiwa umeme haina tofauti sana na mtu aliyeingia kwenye mkopo ambapo anatakiwa kisheria kulipa kila mwezi kiasi cha pesa kwa mtoa mkopo ambapo kushindwa kufanya hivyo ni kukaribisha matatizo kwenye dhamana.

Badala ya nguvu nyingi kuzitumia kusaka wananchi waliojiunganishia umeme, TANESCO wanatakiwa wazitumie nguvu hizo kuwaunganishia umeme bure wananchi na kwa kufanya hivyo, wananchi wengi wataunganisha umeme na matokeo yake, TANESCO watapata mapato mengi huku wananchi wengi wakiachana na tabia ya kuiba umeme.

Mbaya zaidi, hata wananchi wanaotaka kulipa ili kuunganishiwa umeme na TANESCO inabidi watoe rushwa au wasubiri kwa muda mrefu na kutokana na mazingira hayo, wananchi wanafikia uamuzi wa kujiunganishia bila ruhusa ya TANESCO.

TANESCO lazima ibadilike na kama imeshindwa kubadilika, basi mazingira yataibadilisha!

VIDEO:
 
Una vituko.

Tanesco ni kampuni inayofanya biashara, iunganishie umeme bure watu malighafi za kuunganishia watu itazitoa wapi maana haizalishi waya wala mita wala nguzo.

Huna sababu ya kutetea watu wanaojiunganishia umeme, mwizi ni mwizi tu hata awe shehe au padri au mchungaji, kujiunganishia umeme bila ridhaa ya tanesco ni uhujumu uchumi na ni kinyume cha sheria ya umeme ya mwaka 2008.

Kuna watu wameunganishiwa umeme kwa bei ya chini, REA au wameunganishiwa kwa bei ya kawaida lakini bado wanaiba umeme..

Hao viongozi wa dini waliojiunganishia umeme ni wezi kama wezi wengine., kwa maisha ya sasa kitu kinachowakera watu wengi ni ankara za umeme, umeme ni wa lazima lakini umeongeza gharama za maisha kwa hiyo watu hutafta mbinu ya kupunguza hayo makali kwa kuiba umeme.

Miaka michache iliyopita nakumbuka tanesco ilitangaza kukamata baadhi ya vigogo wa serilaki wakiiba umeme. Kuiba umeme iwe umejiunganishia mwenyewe au umeunganishiwa na tanesco ni kinyume cha sheria.
 
Back
Top Bottom