Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,251
- 44,586
- Thread starter
-
- #241
Hayo makundi Mzee Mwanakijiji kayaona kwa chadema peke yake na ndiyo sababu kubwa anayosema kwamba hawataweza kushinda uchaguzi ama hawatakiwi kushinda uchaguzi(not ready to lead),sikujuwa sababu ya yote hayo ni Membe.
MZEE MWANAKIJIJI, umeamua ku swing kivyako siku mbili hizi, umepima malaria? huyu ni bora tukamchukue HEADBOY wa BENJAMINI MKAPA atatufaa kuliko pendekezo lako. kwanini uhangaike kuwawazia hao walioko ccm wakati jamii ya watanzania wame wachoka? huoni walivyo taka kutuingiza kwenye vita vya kidini? huoni walivyo iyumbisha serikali mpaka watu hawajui wafanye nini? huoni wanavyo baguana wao kwa wao? huoni wanavyo halalisha rushwa mpaka PCCB hawajui wasimamie nini maana walio iasisi ndio watoaji na wapokeaji wakubwa wa rushwa.huko hakuna msafi, wamebaki wanao penda ngumi mkononi, udini, visasi, ubaguzi na kila baya ulijualo.Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"
CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.
Ni kweli?
Mzee Mwanakijiji,
Sintopendekeza mtu isipokuwa kwa manufaa ya taifa na japokuwa Membe ni kichwa, muweza ukiachana na habari za Ufisadi wake maana huko CCM hakuna msafi kihivyo. Wayahudi walilaaniwa tena na Mungu mwenyewe lakini bado wanaitawala dunia.
Hivyo pamoja na utetezi wako bado nakuhakikishia kwamba CCM wataweza tu kushindana ikiwa watamsimamisha Asha Rose Migiro na hii itatokana na WANAWAKE kutumia kauli mbiu ya TUKIWEZESHWA TUNAWEZA. Itakuwa sio swala la chama bali wanawake against the rest...Na amini maneno yangu watu hawatatazama tena nyuma wala kutazama uwezo wa AshaRose isipokuwa ni mageuzi ambayo kwao yatawalemaza akili..
Kwa upande wa ushindani na hasa Chadema wanatakiwa kuanza mapema sana kumtafuta na kumwandaa mgombea japo kwa siri lakini nawatahadharisha mapema - KAZI IPO 2015 wajipange mapema na vizuri sana laa sivyo itakuwa aibu maana elimu ya Uraia haijazama vichwani mwa wananchi hivyo SHIDA na MATATIZO yanatangulia Mapenzi yao..
Ni ukweli Usiopingika kuwa Mhe. Membe ndo Rais Ajaye Tanzania, ndio atamrithi JK maana historia inamlinda kila awaye Waziri Mambo ya Nje ndo Rais Ajaye toka 1995
Ni ukweli Usiopingika kuwa Mhe. Membe ndo Rais Ajaye Tanzania, ndio atamrithi JK maana historia inamlinda kila awaye Waziri Mambo ya Nje ndo Rais Ajaye toka 1995
Ni ukweli Usiopingika kuwa Mhe. Membe ndo Rais Ajaye Tanzania, ndio atamrithi JK maana historia inamlinda kila awaye Waziri Mambo ya Nje ndo Rais Ajaye toka 1995