Hoja kuwa Mwanamke ni dhaifu ni kweli?

Hoja kuwa Mwanamke ni dhaifu ni kweli?

Quetzal

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
6,412
Reaction score
10,926
Habari,

Nimekuwa nikisikia sana kuwa Mwanamke ni dhaifu. Akizungumziwa mwanamke udhaifu nao lazima uwepo hapo.

Je, udhaifu huu ni upi? Mbona nikimuangalia wanawake wengi tu siwaoni kama dhaifu.

Je, udhaifu wa mwanamke upo katika nyanja gani?

Nawasilisha.
 
Hili swala hutegemea Sana malezi kwani Hata wanaume wengi Ni dhaifu. Ingawa wengi Wana elimu kubwa, Wanawake wa mwambao wa pwani Na Kanda ya ziwa Ni dhaifu katika nyanja nyingi za maisha kutokana malezi, ukilinganisha na wale wa Arusha, KILIMANJARO na Mbeya.
 
Huwezi kuwa Imara ikiwa ulitoka kwenye sehemu ya kitu fulani ukapatikana wewe.
 
Mwanamke sio dhaifu tukianza kubishana kwa hoja za maandishi.

Ila kwenye ulimwengu wa uhalisia mwanamke akilinganishwa na mwanaume, mwanamke ni dhaifu.
Fafanua.
 
Elezea kidogo mkuu
Mungu Alimuumba Mwanamume kwanza akamuona yu mpweke, akamuumbia mtu wa kufanana naye ili asiwe MPWEKE, akamfanya Mwanamke kutoka kwenye Nyama na Mifupa ya Mwanamume yaani Adam. Anakuwaje Imara!?
 
Mungu Alimuumba Mwanamume kwanza akamuona yu mpweke, akamuumbia mtu wa kufanana naye ili asiwe MPWEKE, akamfanya Mwanamke kutoka kwenye Nyama na Mifupa ya Mwanamume yaani Adam. Anakuwaje Imara!?
Lakini binafsi utofauti mkubwa ninaouona Kati ya mwanaume na mwanamke Ni physical strength tu. Mengine tunafanana, la sivyo Basi kusingekuwa na Tanzania one mwanamke
 
Hili swala hutegemea Sana malezi kwani Hata wanaume wengi Ni dhaifu. Ingawa wengi Wana elimu kubwa, Wanawake wa mwambao wa pwani Na Kanda ya ziwa Ni dhaifu katika nyanja nyingi za maisha kutokana malezi, ukilinganisha na wale wa Arusha, KILIMANJARO na Mbeya.
Kwaiyo udhaifu wa mwanamke unahusianishwa na ukanda aliotokea. Na sio asili ya kuzaliwa?
 
Lakini binafsi utofauti mkubwa ninaouona Kati ya mwanaume na mwanamke Ni physical strength tu. Mengine tunafanana, la sivyo Basi kusingekuwa na Tanzania one mwanamke
Sijasema hawana Akili, kama mstari wako wa mwisho ulivyotanabaisha. Ila kimsingi Mwanamke atabaki kuwa Mwanamke na Mwanaume atabaki kuwa hivyo. Nature ishafanya Distinction na hakuna namna ya kuifanyia Ulinganifu
 
1Petro3:7-Kadhalika ninyi waume,kaeni na wake zenu kwa akili;na kumpa mke heshima,kama chombo kisicho na nguvu;na kama warithi pamoja wa neema ya uzima,kusudi kuomba kwenu kusizuliwe:mambo yote yameanzia huku kwenye neno la Mungu,tuendelee...
 
mwanamke ni dhaifu coz alikua wa kwanza kudanganywa na pia wa kwanza kudanganya kwa mujibu wa maandiko
 
HUO NDIO UDHAIFU WENYEWE...

KUTOUTAMBUA NA KUKUBALIANA NA UDHAIFU ULIO NAO MWANAMKE NDIO UDHAIFU WENYEWE HUO...
Natafuta kujua...tu na kusikiliza wadau wanasemaje... Nimesikia Sana viongozi wa Dini wakisema wanawake ni dhaifu... T

Nikawa najiuliza udhaifu huu ukoje...ndo nachotaka kujua..
 
HUO NDIO UDHAIFU WENYEWE...

KUTOUTAMBUA NA KUKUBALIANA NA UDHAIFU ULIO NAO MWANAMKE NDIO UDHAIFU WENYEWE HUO...
Ulitakiwa unipe Dalili...Sio kuandika.kwa herefu kuubwa...hoja isioeleweka.
 
Inawezekana wanawake sio dhaifu (as how they claiming) lakini Udhaifu wao wanauthibitisha wenyewe kwa kulazimisha kufanya vitu ambavyo anafanya mwanaume ili kushindana.

Naamini kuna vitu vingi mwanaume hawezi kuvifanya ila mwanamke anaweza kuvifanya kwa ukamilifu na ubora. So ili wasionwe ni dhaifu wangewekeza muda wao zaidi kufanya hvyo vitu kwa ustadi na ubora zaidi ili kuthibitisha umma kwamba wao sio dhaifu. Lakini kama wataendelea kufanya vitu vifanyavyo na wanume ili kushindana na bado wataendelea kuonekana hivo
Remember Mbunifu ndio hupandishwa cheo..!!
Naweza kua sahihi au siko sahihi
 
mwanamke ni dhaifu coz alikua wa kwanza kudanganywa na pia wa kwanza kudanganya kwa mujibu wa maandiko
Kwaiyo kuwa muongo Ni udhaifu?..je huyu aliedanganyika yeye hakua dhaifu kudanganywa?

Ina maana wote wasemao uongo Ni dhaifu?
 
Sijasema hawana Akili, kama mstari wako wa mwisho ulivyotanabaisha. Ila kimsingi Mwanamke atabaki kuwa Mwanamke na Mwanaume atabaki kuwa hivyo. Nature ishafanya Distinction na hakuna namna ya kuifanyia Ulinganifu
Ok
 
Back
Top Bottom