Wabunge wa ccm ni kama wamekariri nini cha kusema bungeni.. Kila anayesimama kuchangia bajeti kuu anaongelea mojawapo ya hoja zifuatazo:-
(a) kodi ya kiinua mgongo cha wabunge.
(b)VAT kwa watalii
(c) kumpongeza naibu spika kwa kukalia kiti mfululizo.
(d) ufinyu wa bajeti ya CAG.
Mada yangu inahusu hoja kwamba bajeti ya CAG ni finyu.
Kazi ya CAG ni kukagua na hatimaye kubinisha matumizi ya fedha za umma kama yalikwenda vizuri ama vibaya. Ni kazi nyeti sana. Na ikumbukwe walitengewa bajeti ya sh bil 70 lkn serikali imeona ofisi ya CAG ipewe bil 44. Hoja hii iliibuliwa na Zitto kwa mara ya kwanza na sasa imedakwa na ccm ndiyo imekuwa wimbo midomoni mwao. Na kuna wabumge wanapo iongelea unaona kabisa hakuna wanachokijua.
Wanaamini kuwa alichokiona Zitto (ambaye uwezo wake wa kufikiri ni sawa na wabunge 100 wa ccm) kitakuwa sawa. Hawakuni bongo zao hata kidogo.
Serikali ya awamu ya tano imekuja na mtazamo wa kuondoa ufisadi na kurejesha maadili/uadilifu katika utumishi wa umma.
Lakini pia tunaona makusanyo mengi yaliyokuwa yakifanywa na halimashauri sasa yatafanywa na serikali kuu mfano kodi ya majengo, mabango, n.k
Malipo ya miradi mbalimbali ya ujenzi hayatafanywa na halmashauri bali watapeleka vyeti vya kuthibitisha kuwa mradi Fulani uliopo halmashauri X umekamilika. Wuzara itatuma watu wake kwenda kujiridhisha na hatimaye kutoa fedha za malipo.
Kwa kuzingatia mikakati hiyo hapo juu na ukweli kwamba serikali ya awamu ya tano inalenga kubana matumizi ni dhahiri kuwa kazi kubwa ya CAG itafanyikia wizarani.
Vijana wake waliopo ktk halmashauri watafanya ukaguzi wa miradi na kuzilinganisha na thamani ya fedha iliyolipwa. Tofauti kabisa ilivyokuwa hapo awali.
Jambo kubwa LA kusisitiza hapa ni kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya ofisi hii (bil 44) zote ziende. CAG atafute namna ya kubana matumizi ili pesa hii ambayo ni karibu ya asilimia 70 afanyie kazi kwa ufanisi.
Wabunge wa ccm msituhadae mngekuwa na nia ya dhati ya kumuongezea CAG fedha msingekuwa mnakataa kukatwa kodi kwenye kiinua mgongo. Mbona huyu mwalimu wa shule ya msingi anakatwa?
Ktk awamu ya nne CAG amekagua na kubqinisha madudu mengi sana ktk matumizi ya serikali. Halmashauri nyingi zikawa zinapata hati chafu kila mwaka. Sikuonq tija. Ufisadi ulizidi kushamiri huku ukaguzi ukifanywa na CAG. Nadhani hoja hapa iwe ni kuzuia ifisadi na ubadhilifu. Tuwe wakali kwa kila atakayefuja fedha za umma ili miaka ijayo ofisi hii I we inapewa fedha mara moja kila baada ya miaka 5. Lkn baada ya ukaguzi kufanyika na ikabainika ufujaji wa Mali ya umma hatua kali zichukuliwe.
Nawasilisha.