Hoja binafsi: Ninaomba Bunge lifute vyama vingi tubaki na chama kimoja cha CCM

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Tangu tumeingia katika mfumo wa vyama vingi tangu 1995 hadi leo hii sijaona umuhimu wa vyama vingi kwa watanzania ni bora tubakie katika chama kimoja kuliko kuwa na vyama vingi.

Tangu tuingie katika huu mfumo wa vyama Vingi hadi Leo huu mfumo umekuwa mchungu sana kwa watu ambao wanaonekana kuunga mkono upinzani na hata wafuasi wa upinzani wamekuwa wakipitia katika hali ngumu na mapito magumu ambayo huwezi kueleza

Hivyo katika bunge lijalo ninamuomba spika ndugai na tulia ackson naibu spika pamoja na mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja wingi wa wabunge wa ccm mfute sheria ya uwepo wa vyama vingi na mvifutee kabisa vyama vingi ibakie CCM peke yake na tuwe na bunge la CCM.

Sisi wafuasi wa upinzani tumeshakubali kushidwa mambo ya uchaguzi sijui mbunge, sujui diwani sijui Rais mchaguane wenyewe kwa wenyewe hamna shida na hizo pesa za kuendesha chaguzi ziende katika maendeleo .

Inatosha sasa hapa tulipofikia inatoshaaa tuliyoyaona katika mfumo wa vyama vingi inatosha sasa enough its enough madhara tuliyoyaona inatosha sasa tunataka tuishi kwa amani na furaha.
 
Ninaunga mkono hoja yako Mkuu, tena naongezea.........natamani Mbowe na wenzake watutangazie Leo kuwa kutokana na yanayoendelea Nchini basi hatuna haja ya kuwa na vyama Vingi, hivyo kuanzia siku yoyote Chadema tunaifuta kwa msajili Wa vyama, baada ya hapo afuate Zitto na ACT, RUNGWE, CUF ile ya halali CCM iachwe inyooshe wananchi wake itakavyo..........
 
Tena mwaka 2020 sina hakika kama kuna mbunge wa upinzani atakaye rudi bungeni. Labda tu kwa Wale mapandikizi ya ccm yaliyopo upinzani
 
Kuuwa vyama ni dalili ya kushindwa siasa za ushindani,lakini ni bora kuachana na mchezo wa siasa za vyama kuliko kuuwana kama kuku.Lakini tatizo kubwa kwa nini tunashindwa kuvumiliana na kuheshimiana?

Sasa nami nafikiri ili haki itendeke yaani tukose wote,tumkabidhi nchi Malkia Elizabeth nchi yake hadi tutie akili miaka 70.Hayo majigambo yatakwisha tutaitana waTanganyika na sio Watanzania.Labda tutajua hata lugha ya kutunga sheria.
 
Kwa style ile ile ya nyerere alivyouliza wananchi kama wanahitaji vyama vingi ingefanyika tena kura za maoni ili tukatae hivi vyama vingi......bora kuwe na chama kimoja ili tujue moja
 
Kama mmeanza kufumbuka macho basi mmekomaa kisiasa.

Kuna watu hawatakuelewa,huwezi kufanya biashara eneo la soko ambalo limepigwa marufuku
 
Back
Top Bottom