Hoja binafsi kupinga ongezeko la bei ya mafuta

Hoja binafsi kupinga ongezeko la bei ya mafuta

Naunga mkono hoja
Jamani upole umetuponza
Ifike mahali tubadilike wa-tz
 
Watu wanaongea issue za maana wanakuja mabarubaru na magabachori kuanza kuharibu.

Back to topic:
Hivi zile tambo za Mkulo kupunguza kodi na tozo mbali-mbali ili kupunguza bei za mafuta zimeishia wapi? au ilikuwa ni danganya toto ili bajeti ipite?, mafuta ndio yanazidi kupaa, Tanzania bana, tunadanganywa eti shilingi imeshuka thamani, may be kweli, lakini kwa nini shilingi yetu inazidi kuporomoka wakati hatuna vita, hatuna njaa na tunaambiwa 'uchumi unakuwa'?.

Mheshimiwa JK mwezi huu nao utatuchinjia baharini tena kwa hotuba zako za mwisho wa mwezi?, tunapenda kusikia kiongozi wa nchi unasema nini kuhusu haya matatizo au J. Makamba yuko bize siku hizi na huna mtu wa kukuandikia hotuba?

Tunahitaji kuchukua hatua.

Kapotolo Ni kitugani tena Rais wetu anaweza kuliambia taifa kwa sasa katika mazingira haya. JAMANI WATANZANIA SAMAHANINI NAOMBA TUONDOE HULKA NA MISIMAMO YETU YA KICHAMA KWANZA.

TANZANIA INATEKETEA TARATIBU AMINI MSIAMINI HII NCHI INALIWA NA YAISHA SASA. SERIKALI INAKOSA UMAKINI USIMAMIZI WA NCHIYETU HUKO WAPI SASA. NANI ATATUSEMEA KAMA RAIS ANAKUWA KIMYA NAMNA HII. ANASHINDWA KUTOA MWONGOZO NINI KIFANYIKE ANAKAA IKULU ANAFANYA NINI KAMA ANASHINDWA KUTOA MWONGOZO. INASIKITISHA SIO KUONGEA MAMBO YA SIASA LA ILA HALI SI SHWARI WATANZANIA.
MIMI NALIA SANA NA NEC NEC NEC NEC MMETUPOTEZA WATANZANIA BASI
 
Vp mmeshawasiiliana na Chama cha demokrasia na maadamano Tanzania kuratibu mgomo huo?

Barubaru

Nakuheshimu sana bro.
Kulingana na avatar yako inaonyesha wewe ni muislamu saafi na ukizingatia kuwa huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhan ulipashwa uchangie hoja kwa kutumia AKILI na siyo MAKALIO!!!

Get me? Karibu sana.
 
Kwa pamoja tutaweza tukiwa pamoja na chama cha manafiki,Mungu ibariki TZ,Mungu Mbariki Slaa
 
Ndugu zangu, Ni ukweli, kuwa hali za maisha ya kiuchumi ya watu wetu zinazidi kuwa ngumu. Na inaonekana, kuwa ndio moja ya sababu iliyopelekea Serikali kupitia EWURA kuingilia kati bei za mafuta. Ni dhamira njema ya Serikali ingawa kuna umuhimu pia wa kujadili matokeo ya dhamira hiyo. Tufanye hivyo ili labda iwe fundisho kwa baadae. Maana, Watanzania tumesoma kwenye media, kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kupanda tena kwa bei za mafuta kati ya asilimia 5 na 6 kuanzia leo. EWURA inasema, kuwa kupanda kwa bei hizo kunatokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuendelea kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na dola ya Marekani. Na Watanzania tunapozwa kwa kuambiwa, kuwa bei ya sasa ya mafuta ina unafuu kutokana na kutumika kwa kanuni mpya ya ukokotoaji wa bei, na iwapo ingetumika kanuni ya zamani, petroli kwa Dar es Salaam ingeuzwa kwa sh. 2,298.33, dizeli 2,213.36 na mafuta ya taa kwa sh. 2,188.89. Na tunaambiwa, kuwa kwa mujibu wa sheria ya mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. Na kwamba EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta kwa lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta. Tafsiri yangu; Kwanza tunaona hapa, kuwa wiki iliyopita bei iliteremshwa kwa asilimia 9. Na wiki hii imepanda kwa asilimia 6. Hapa hakuna tofauti kubwa . Kingine ni ukweli kuwa EWURA inakiri kuwa bei imepanda kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta duniani na kushuka kwa shilingi ya Tanzania. Ukweli huu una maana kuwa bei ya mafuta inaweza kupanda tena kama bei ya mafuta ya dunia itazidi kupanda na shilingi yetu itazidi kushuka. Na mfumuko wa bei hii leo unaripotiwa kufikia asimilimia 13, unapanda. Pamoja na ukweli kuwa mimi ni ‘Mchumi wa porini tu’- Bush- Economist, lakini, naona kuna makosa yamefanyika juu ya namna EWURA ilivyoshughulikia kinachoitwa sasa ‘ Mgogoro kati ya Wadau wa Mafuta na Serikali kupitia EWURA”. Ni mgogoro, maana hata lugha iliyokuwa ikitumika na labda inaendelea kutumika ni ya ‘ Kimapambano’. Ni ukweli, kuwa katika juma moja tu la ‘ mgogoro’ huu wa mafuta uchumi wetu umepata pigo. Inasemwa; chagua vita vyako. Nenda kapigane vita vyenye lazima na huku ukiwa umejizatiti kushinda. Kama ama hakuna lazima ya kuingia vitani au hujajizatiti kushinda, basi, busara ni kuepuka vita hiyo. Maana, si kazi kubwa kutabiri matokeo yake. Kwetu kama nchi haukuwa wakati muafaka wa kuingia kwenye ‘ Vita’ na wafanyabiashara ya mafuta. Kwa hali ya sasa ni heri kuingia ‘ vitani’ na wafanyabiashara wa matikiti Kariakoo kuliko wafanyabiashara ya mafuta bandarini Kurasini. Suala la mafuta linahusu soko. Na dubwana hili soko liko ‘ sensitive’ sana. Kuna wakati gari la wagonjwa lilionekana likiingia Ikulu ya Mandela. Siku hiyo hiyo sarafu ya Rand ikashuka thamani dhidi ya dola. Kisa? Soko lilishtuka; kama Mandela mgonjwa na anakufa huenda South Africa ikaingia kwenye machafuko na uchumi ukavurugika. Ndio, soko lilishtuka tu! Baadae ikafahamika, kuwa Mzee Madiba alikuwa na tatizo dogo tu la kiafya, basi, sarafu ya Rand ikapanda tena thamani kwenye soko. Na sisi kama nchi, Soko linatufuatilia kila dakika. Soko likisikia Serikali ya Tanzania inashikana mashati na watu wa mafuta, basi, linashtuka. Na kwa upande wetu inaonekana soko limeshtuka kweli. Inahusu economics stability of a country. Kuna wawekezaji wanaoweza kusitasita kuhamishia mitaji yao kwetu wanaposikia Serikali ina mgogoro na wafanyabiashara wa bidhaa nyeti kama hii ya mafuta. Naam, mafuta ni kila kitu inapohusu uchumi. Tunadhani, hatua zote za majadiliano kati ya Serikali/ EWURA na wafanyabiashara zingefanyika kabla ya EWURA kuanza kuwatunishia misuli wafanyabiashara ya mafuta. Na katika hali ya sasa hakuna suala la who won the battle? Itangulizwe busara tu. Ndio, itumike diplomasia ya kiuchumi itakayozileta kwenye meza moja pande zinazotofautiana. Haya ni mambo ya kuyamaliza mezani kwa mazungumzo. Tusikimbile kwenye ’ kamata kamata’ na ’ fungia fungia’ ya Wafanyabiashara ya Mafuta. After all inahusu biashara, na biashara ni maelewano. Wafanyabiashara wa mafuta wanatuhitaji na sisi tunawahitaji. Ni ukweli, kuwa tunahitajiana. Na mazungumzo ya upatinishi yaanzie na ukweli huo. Ni hayo tu. Maggid, Iringa, Agosti, 16, 2011 MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
 
Kuna sababu nyingi za kutaka hii serikali ibadilishwe.
Ila hii ya bei ya mafuta ni ulimbukeni wetu tu,hatuzalishi mafuta,tunanunua na bei ya mafuta hubadilika sio kila wiki tu,sometimes everyday! sasa kama EWURA wanapanga bei bi-weekly sioni tatizo lolote.Tangu waanze kutumia formula mpya angalau consumers wanapata bei inayoreflect world markets.Mafuta yamepanda by 1.94% ambayo ni shs 40,jumlisha thamani ya shilingi kupungua kwa 47 shs unapata 87shs.
87=2030=2107shs.
Kwa hii formula,every two weeks kutakuwa na bei mpya ya mafuta,nchi nyiiingi duniani ndivyo zinavyo calculate bei ya mafuta(kutokana na soko la dunia),ikishuka yatashuka and vice versa......huu unazi sometimes unatuaibisha watanzania,mafuta siyo maembe!
 
Kuna sababu nyingi za kutaka hii serikali ibadilishwe.
Ila hii ya bei ya mafuta ni ulimbukeni wetu tu,hatuzalishi mafuta,tunanunua na bei ya mafuta hubadilika sio kila wiki tu,sometimes everyday! sasa kama EWURA wanapanga bei bi-weekly sioni tatizo lolote.Tangu waanze kutumia formula mpya angalau consumers wanapata bei inayoreflect world markets.Mafuta yamepanda by 1.94% ambayo ni shs 40,jumlisha thamani ya shilingi kupungua kwa 47 shs unapata 87shs.
87=2030=2107shs.
Kwa hii formula,every two weeks kutakuwa na bei mpya ya mafuta,nchi nyiiingi duniani ndivyo zinavyo calculate bei ya mafuta(kutokana na soko la dunia),ikishuka yatashuka and vice versa......huu unazi sometimes unatuaibisha watanzania,mafuta siyo maembe!
Vp mambo ya Stock? maana bei ikishuka wao wanaomba stock iishe bei ikipanda hakuna cha stock wala nini? hili linchi bana?
 
Barubaru<br />
<br />
Nakuheshimu sana bro. <br />
Kulingana na avatar yako inaonyesha wewe ni muislamu saafi na ukizingatia kuwa huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhan ulipashwa uchangie hoja kwa kutumia AKILI na siyo MAKALIO!!!<br />
<br />
Get me? Karibu sana.
<br />
<br />
YOU TELL HIM FACT MEN
 
Shida jamani ni serikali yetu. Hata kama thamani ya shilingi imeporomoka na bei ya mafuta imepanda katika soko la dunia, bado serikali ina jukukmu la kulinda raia wake kutoka katika mfumuko wa bei. Kama EWURA ama serikali ilitaka bei ya mafuta iteremke dawa ilikuwa kupunguza kodi inayotozwa na si kuleta visingizio kibao. Kazi imewashinda kwa hiyo dawa ni moja tu, watolewe kwa nguvu ya umma.

Nimesoma kwenye gazeti la Sema Usikike kuwa CDM kulipuka tena. Jamani wa TZ tuache mzaha, maandamo ya safari hii yawe mwanzo wa kuundoa utawala huu dhalimu. Tuondoe woga na ukondoo, Tanzania sasa imeiva kwa mapinduzi, hebu tuwe sehemu ya historia ya kuleta mapinduzi.
 
Ni kweli kabisa watanzania wenzetu wamekosa maono kiasi hiki? wanapunguza bei ya mafuta kabla wiki haijaisha wanaongeza bei zaidi. ilikuwa na maana gani kutuweka katika ukame wa mafuta kwa kipindi cha siku zote zile.

Kama ni kushuka kwa shilingi wachumi walikuwa na kazi gani na kwanini wasitasmini hilo mapema?
Hivi wanatufanya sisi hatuoni au wajinga sana au hatuwezifanya chochote hivyo wanatupeleka tu.

Basi tufute ewura kwasababu inaongeza matumizi kwa kuwalipa mishahara na posho watu ambao hawana kazi yoyote...
 
Ewe Mwenyezi Mungu zidisha maisha yawe magumu kwa hali zote umeme juu mafuta juu sukari juu sembe juu mafuta ya kula juu.kwasababu tuna macho lakini hatuoni,tuna masikio lakini hatusikii ni kulogwa????????siku inakuja tutatia akili Mwl.alifanikisha azma yake ya kutawala wajinga.
 
Hizi hadithi hazitaisha leo wala kesho kupanda kwa gharama za mafuta kinacho jili ni kupanda kwa bei za bidhaa someone has to pay the extra cost za wafanyabiashara za uchukuzi na kama tuna viwanda vinavyotumia mafuta kujiendesha.

Hapa realistically kuangaika na EWURA ni kupigia mbuzi gitaa lawamaa hizi zilitakiwa ziende straight to Mr.Mkullo. EWURA ni nani na wanapata wapi nguvu za kupanga bei ya bidhaa sokoni au hizi taasisi zinatumia formula gani kwenye kupanga ushuru bila kuwaumiza watanzania.

Ndio tunarudi pale pale Mkullo is a problem the guy hana mbinu za kumanipulate internal growth kwa hivyo macho yao yameamia bandarini na kukomoa watanzania wachache hili kuongoza pato la taifa, ushuru wa tanzania katika bidhaa zingine zinazoingia is somewhat pathetic and putting off to potential investors.

Its about time wale jamaa waliondaka the five years plan wakae mstari wa mbele apparently they do understand the core of our problem lakini vinginevyo watu wataendelea kuumia na maisha kuwa magumu chini ya huyu jamaa na raisi wetu kwanza asiye jua hata sababu za umaskini wetu.
 
Ni mfanya biashara gani amesha enda jana usiku kununua mafuta kwa bei iliyotangazwa jana usiku????
HUU NI WIZI WA MCHANA KWEUPE! Wauza mafuta wanatuchezea. Tusikubali.
wacha kuota wewe!!
Wafanyabiashara wanakuchezea kivipi wakati Bei imepandishwa na EWURA??!!
Kwanza kabla ya hapo EWURA walitutangazia kuwa SERIKALI IMEPUNGUZA KODI ZA UNUNUAJI MAFUTA KWA MAKAMPUNI YANAYOAGIZA MAFUTA kutoka nje kwa almost 40%.
Hakuna punguzo kama hilo, kodi ilipungua kutoka aprox. Tshs 500 na kua aprox. Tshs 400 (-20%)

Mbona hatusikiii kwa majirani zetu kama Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi n.k kuwa Bei zao zinapanda kila kukicha?Tunajua hata wao majirani zetu pesa zao haziko stable sana dhidi ya Dollar ya Marekani. Tuchukue mfano wa Uganda ambao thamani yao ya Shilingi iko chini ukilinganisha na Shilingi ya Tanzania. Mbona hatusikii na wao kila siku wakiteremsha na kupandisha bei za mafuta kwa visingizio vya thamani ya shiling
Kenya wamepanisha bei

Watanzania tusipende kutawaliwa kama makondoo. Ni wakati wa Watanzania kuonyesha mshikamano sasa kwa kuingia mitaani kwa maandamano na kugoma kununua mafuta kutoka vituo vya wauza mafuta halafu tuone nini kitatokea. Inawezekanaje bei ya mafuta soko la dunia ipande jana na leo tayari muuza mafuta auze kwa bei ya soko la dunia???Ni saa ngapi huyu muuza mafuta ameingiza mafuta mapya yenye bei ya soko la dunia???
MASEBU NA EWURA YAKO ONDOKENI HATUWATAKIIIIII !!!!!!!!!!!!!
La msingi ni kua Ewura imekua ikifanya kazi kisiasa zaidi kuliko kitaalamu.
Nachelea kusema kwamba walikua wanatafuta Credit za kumpa Ngeleja ili bajeti yake ipite.
Nitaendelea kupingana na wengi kwa kuamini kwamba waagizaji mafuta walikua wana haki ya kuendelea kuuza kwa bei ya mwanzo ili kimalizia stock zao kwanza.
Ndio maana EWURA kwa kuliona hilo wameamua kurudisha bei palepale, kwani kama ni Credit za kupitishia bajeti, Ngeleja ashazila za kutosha tu na makofi juu kutoka kwa wabunge
 
Hakuna umuhimu wa mamlaka kama EWURA kwa sasa.Hii ni wakala tu wa kuwalinda wafanyabiashara na kujikusanyia mapato kwa ajili ya wachache. Uthbitisho wa hili ni maamuzi na matendo yake na usumbufu kwa wananchi kwa sakata lililopita ambapo EWURA imesalimu amri kwa wafanyabiashara huku ikitoa sababu za uongo.
Baada ya wafanyabiashara kugomea bei iliyoshushwa EWURA iliwahakikishia kuipandisha baada ya muda mfupi na ndyo maana makampuni yaligoma kutoa mafuta kwenye bohari wakisubiria bei mpya pamoja na kuombwa na EWURA wawe wanatoa mafuta kidogo kidogo wasionekane wamegoma.
EWURA haiwezi kuyadhibiti makampuni ya mafuta kwa sababu inayategemea kujiendesha. Ustawi wa EWURA unategemea malipo ya makampuni hao. Siyo rahisi hakimu amuadhibu mkosaji halafu hapo hapo amuombe hela ya ya kuendesha mahakama.
EWURA haina msaada wowote kwa wananchi wanaotumia nishati pamoja na maji, zaidi sana ni mzigo kwa kuongeza gharama kupitia tozo.
Serikali inatakiwa iangalie upya uanzishwaji wa mamlaka au wakala zinazoongeza urasimu na gharama kwa wananchi kwani zinapingana na dhana nzima ya kupiga vita umaskini.
Tutumie wataalamu wetu katika kuzalisha zaidi kuliko kuwatumia kuongeza urasimu.
Kwa hali ilivyo sasa katika Tanzania, wananchi wa kipato cha chini wanatakiwa kuanza mapambano ya kujikomboa kama walivyoanza enzi za kudai uhuru. Siyo rahisi tena wapate utetezi wa kuinua hali zao za maisha kupitia mfumo uliopo.
Viongozi walio wengi wanajifikiria wenyewe, familia zao pamoja na marafiki zao.
Wananchi wa vipato vya chini na vya kati mfumo wa utawala hauwajali na uzalendo hakuna tena na matokeo yake ni kuanzishwa kwa wakala za serikali zinazozidi kumyonya mwananchi wa kawaida ili kuwafaidisha viongozi wachache pamoja na wageni.
Kuondoa hali hii, wananchi wa kawaida wanatakiwa kuelewa kuwa viongozi na wanaofaidi mfumo huu ni wachache na hivyo kuwashughulikia ni rahisi sana. Tukiamua kubadilisha hali hii inawezekana tena kwa ufanisi na muda mfupi kutokana na wingi wetu.
Viongozi wanatumia ujinga wa wananchi walalahoi kuwanyonya na kuwadhibiti. Vyombo vya dola vinavyotumika vinaundwa na walalahoi wanaonyonywa kwa asilimia kubwa na wao wanahitaji kushiriki kujikomboa.
Polisi, jeshi la wananchi na hata mgambo wengi ni walalahoi kabisa ambao hawafaidiki na mfumo uliopo na hiyo tukiamua kurekebisha mfumo huu usiowasaidia wananchi walio wengi inawezekana, ni swala la kuamua ili kupata mustakabali mwema kwa watoto wetu na vizazi vijavyo.
Mashujaa tunaowakumbuka siku hizi walijitoa kwa ajili ya wengi na yatubidi kujenga mawazo kwa wananchi kujitoa kwa ajili ya vizazi vijavyo kwa kuwa ukombozi lazima uwe endelevu.
Viongozi wengi wamejisahau wakifikiri kuwa uhuru ulilenga kukomboa wao wenyewe, familia zao na marafiki wachache, lakini ukweli ni kwamba maana ya uhuru ni ukombozi kwa wananchi wote ambao ni zaidi ya milioni 40 kwa sasa na vizazi vijavyo.
Sababu nyingi zitatolewa zisizoweza kuthibitishwa ili tu kuhalalisha unyonyaji huu, mbona hawasemi shilingi imeshuka kiasi gani dhidi ya dola, na bei imepanda kiasi gani kwenye soko la dunia kwa kipindi hicho? Mafuta yaliyokuwa yamehifadhiwa hapa nchini yanhusika vipi na bei mpya?
Tunafanya makosa makubwa kukubaliana kirahisi na maamuzi ya kipuuzi kwa kisingizio tu kuwa ni kulingana na sheria.
 
Back
Top Bottom