Hoja binafsi kupinga ongezeko la bei ya mafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja binafsi kupinga ongezeko la bei ya mafuta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Aug 15, 2011.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Kufuatia tangazo la EWURA la kupandisha bei ya mafuta kwa aina zote yaani Petroli,Dizeli na Mafuta ya taa kuanzia leo naomba Mbunge yeyote makini kutoka upinzani hasa CDM apeleke HOJAS BINAFSI YA KUPINGA ONGEZEKO LA BEI YA MAFUTA kuanzia leo kama ilivyotangazwa na EWURA jana. EWURA hawahawa walituambia kuna stock ya mafuta ya kutosha siku 60(2 months),iweje mara tu baada ya kutangaza bei jana usiku tayari bei zimepanda ASUBUHI? Ni mfanya biashara gani amesha enda jana usiku kununua mafuta kwa bei iliyotangazwa jana usiku????
  HUU NI WIZI WA MCHANA KWEUPE! Wauza mafuta wanatuchezea. Tusikubali.

  Inasikitisha na inashangaza kuona kwamba baada ya mgomo wa Wafanyibiashara ya mafuta kufuatia bei elekezi ya PUNGUZO kutoka EWURA ndani ya wiki mbili bei imepanda tena na kuzidi hata ile bei iliyokuwepo kabla ya mgomo wa Wafanyi biashara wa mafuta.

  Kwanza kabla ya hapo EWURA walitutangazia kuwa SERIKALI IMEPUNGUZA KODI ZA UNUNUAJI MAFUTA KWA MAKAMPUNI YANAYOAGIZA MAFUTA kutoka nje kwa almost 40%.Hili ni punguzo kubwa sana kibiashara. Hata kama Shilingi ya Tanzania inaporomoka kila wiki na bei ya soko la Mafuta duniani inaongezeka kila wiki bado BEI INGELIKUWA inakuwa contained kwenye ile 40%.

  Haiwezekani bei ya mafuta ibadilike kila siku kwa visingizio cha KUPOROMOKA KWA TZ SHILINGI na KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA KWENYE SOKO LA DUNIA!!Je,hii bei ya mafuta soko la dunia inaihusu Tanzania peke yake? Mbona hatusikiii kwa majirani zetu kama Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi n.k kuwa Bei zao zinapanda kila kukicha?Tunajua hata wao majirani zetu pesa zao haziko stable sana dhidi ya Dollar ya Marekani. Tuchukue mfano wa Uganda ambao thamani yao ya Shilingi iko chini ukilinganisha na Shilingi ya Tanzania. Mbona hatusikii na wao kila siku wakiteremsha na kupandisha bei za mafuta kwa visingizio vya thamani ya shilingi na bei ya soko la dunia?

  Bado EWURA imetaka kuwadanganya Wadanganyika kuwa gharama na punguzo zilizofanywa na Serikali zitabebwa na Serikali! Ukweli wa jambo hili uko wapi???Kwanini EWURA na Serikali ya CCM wanawabebesha Watanzania mizigo wasiyo weza kuibeba???Serikali inashindwa nini kubeba gharama hizo na badala yake wanatupa mzigo huo kwa walalahoi???

  Nahitimisha kwa kusema kuwa kwa hili la KUONGEZA BEI YA MAFUTA kama serikali haichukui hatua za makusudi za KUPUNGUZA BEI HIYO kwa kuondoa KODI ZISIZO ZA LAZIMA kwa wafanyi biashara basi SASA IWE NI ZAMU YA WATANZANIA KUANDAMANA KUPINGA ONGEZEKO LA BEI YA MAFUTA.

  Watanzania tusipende kutawaliwa kama makondoo. Ni wakati wa Watanzania kuonyesha mshikamano sasa kwa kuingia mitaani kwa maandamano na kugoma kununua mafuta kutoka vituo vya wauza mafuta halafu tuone nini kitatokea. Inawezekanaje bei ya mafuta soko la dunia ipande jana na leo tayari muuza mafuta auze kwa bei ya soko la dunia???Ni saa ngapi huyu muuza mafuta ameingiza mafuta mapya yenye bei ya soko la dunia???

  MASEBU NA EWURA YAKO ONDOKENI HATUWATAKIIIIII !!!!!!!!!!!!!
   
 2. Yakuza

  Yakuza Senior Member

  #2
  Aug 15, 2011
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Well said, big up!!!
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  jamani ni sisi tu ni waoga...dawa ya serikali hii ni migomo/ maandamano angalia wafanyabiashara waligoma hatimae kimeelewaka sasa sisi watanzania tunabaki kulalamika tu vitendo hakuna, hoja ni jambo jema wasiwasi wangu mtoa hoja ataambiwa kaa chini na akikaidi nje baadae tutamwita mhuni...
   
 4. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni kweli hii nchi Watanzania tunapelekwapelekwa, Mheshimiwa baba wa Taifa alipata kusema "Wapo viongozi katika vyombo vya umma ambao wanahitaji mapinduzi makubwa ya fikra na tabia, wakishindwa kufanya hivyo wenyewe, basi watarekebishwa na wananchi".

  Kulingana na maneno haya ya baba wa taifa, wananchi sasa hatuna budi kufanya maamuzi sisi wenyewe. Tumechoshwa na utawala huu.
   
 5. P

  Polisario Member

  #5
  Aug 15, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani JK nchi imekushinda achia ngazi au anataka hadi ufe!
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  madaraka matamu sana hawezi kuachia hivi hivi mpaka muonyeshe mmemchoka siyo kwa maneno kwenye keyboard tu...
   
 7. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  No fear destination darkness!!!
  Naomba mungu maisha ya mtanzania yazidi kuwa mabaya ili watanzani wafanye maamuzi magumu.wafanyabiashara waweza kuwa chachu ya mapinduzi?!
  Wauza mafuta,TABOA,wauza sukari na mahindi pandisheni bei za bidhaa mpaka kieleweke na akili zetu zikae sawa!
   
 8. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli ndugu yangu mtoa hoja na wadau wengine waliochangia Hapa Tanzania tunakazi sio ndogo. amini usiamini sisi watanzania ni wezi wote si bure. NAWAMBIA WATANZANIA WOTE NI WEZI HATA MIMI PIA MWIZI. Kwanini nasema hivyo hatuwezi kukaa kimya vitu vinapanda kiholela holela kisha unaona watu wanakaa kimya kama vile nijambo dogo sana. kama kweli tungekuwa tunatafuta kwa majasho yetu leo tungekuwa bara barani jamani amini msiamini huu ndio ukweli. angalia nchi za wenzetu wanahali ya kudhubutu sisi tunakuwa kama mafala tuuuuuu. samahani kama nitakuwa nimetukana ila inasikitisha sana jamani.
  JAMANI NANI KATULOGA NANI KASHIKA MAAMUZI YETU WATANZANIA . SITAKI HALI YA AMANI IPOTEE ILA HAKI ITENDEKE HIVI HATA HAWATUNAOWAOGOPA YAANI POLISI NAO MAISHA KWAO SI MAGUMU JAMANI TUSHIKAMANE SI KWANIA YA KUTOWESHA AMANI ILA KUITENGENEZA NCHI YETU.

  TAMBUA KUWA HALI HII ITATUPELEKA KATIKA VITA KAMA AITATAFUTIWA UFUMBUZI MAPEMA
   
 9. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #9
  Aug 15, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Mtoto mara nyingi akikulia katika mazingira ya kukosolewa kosolewa hujifunza kulaumu.
  Mtoto mara nyingi akikulia kwa mzazi mwenye kupenda kulaumu huiga tabia hiyo ya kulaumu
  bila kuchukua hatua. Kwanini Watanzania tusichukue hatua sasa badala ya kuendelea kulaumu?
  Kama baba (kiongozi wa nchi) ameonekana kuwa mtu wa kulaumu tu, tusimuige bali tuoneshe
  kwa vitendo kile kinachopaswa kufanywa badala ya kuishia kulaumu...

  Huu ni mtazamo wangu.
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Vp mmeshawasiiliana na Chama cha demokrasia na maadamano Tanzania kuratibu mgomo huo?
   
 11. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mbona EWURA kichwa maji sana, sasa walileta mgomo wa nini majuzi na kujifanya kuifungia BP mbona wao ndio wameonekana wapuuzi wasiojuwa wanalofanya.

  Nilitaka kushangaa Ma-tycoon waliochangia fedha nyingi katika kampeni ya kijana wao na kuupata urais kama wangeangushwa wakati fedha zao walizochanga zinarudishwa bei ya mafuta kuwa juu.

  Kuhusu hoja binafsi waambie CCM ndio mliowapa Wabunge wakati wa uchaguzi.
   
 12. M

  Marcossy A.M Verified User

  #12
  Aug 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Uwanja mweupe..... Nani alianza akalazimika kwenda kinyume? mbona Nyerere na wenziwe waliweza: huu uoga wa wapi? Muda ulikuwa bado. SASA NDO UMEFIKA. KARIBUNI8...
   
 13. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  ni kweli maana hawa Ewura wanaelewa baadhi ya facts juu ya kinachoendelea lakini tumekumbatia mfumo mbaya wa kuendesha mambo na ukichanganya na 'ujinga/upole/ukarimu' wa Watanzania wanaamua kwenda hivyo hivyo, kwa hakika hali haiwezi kubadilika hadi tu abandon hizi keyboards ili kuwa mfano na kuingia barabarani!
  Niliangalia kipindi cha 'Kipima Joto' ITV juzi ndio nikakata tamaa. Zakharia Hans Pope anajaribu kwaeleza hali halisi (state of nature) lakini kuna watu wawili wa Ewura (tena mwingine Engineer wanaongea mambo ya sijui 'sera', 'elekezi', 'mwongozo' na mambo yasiyo na uhalisia wowote!
  All in all there is something wrong like any other industry in Tanzania and due to sensitivity of this area measures should be taken.
  Asante kwa thread hii japo mwanzo ni mgumu
   
 14. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nakuunga mkono,huu ni wizi wa hadharani, ila kwa wenye upeo kama wa kwako ndo watajua huu ni wizi
   
 15. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #15
  Aug 15, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ngeleji ni legelege ameulizwa swali inakuweje kwa stock iliyopo akasema mpaka waende wakaangalie sasa iweje bei ipande ikiwa fika hajui stock ya mafuta ikoje? Hawa ndio mawaziri wetu.
   
 16. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Tanzania na watz wote ni wanafiki,hatuwezi kuthubutu hata kidogo, shida yetu ni mikelele tuuu!

  Leaders wanatuburuza,wanatuchuna, wanadharau,wanatu *** kama wanavyotaka...aaah! i hate peole of this country for being cheap,untough......

  JK na familia yake + friends wanaenjoy maisha whereas the rest of watz kupongezana na kutoa lawama tuuu!
   
 17. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Shegaboy,

  Big up kwa mchango wako.
  Umezungumza kama vile tuko pamoja. Hii inathibitisha kuwa Watanzania tuna uchungu sana kwa jinsi Serikali ya Magamba inavyotuhujumu na kutufanya tuishi maisha ya kubahatisha wakti viongozi wetu wako mjengoni wanakula kuku kwa mrija: Tshs.150,000/= per diem. Saa ngapi wataona uchungu wa bei ya mafuta??? Hakika inasikitisha sana.

  Ni dhahiri kabisa hawa jamaa hawa-feel hii hali ambayo wananchi tunaipitia. Tatizo kubwa tulilonalo ni kuwa wengi wa viongozi wetu wa SERIKALI WANAFANYA BIASHARA HII YA MAFUTA, na ndiyo maana hawajali chochote. Wao wanafikiria kupata FAIDA KUBWA KUPITIA MIGONGO YA WATANZANIA MASKINI.

  Ndiyo maana mimi nasema kila siku ya kwamba Tanzania HATUNA SERIKALI,hatuna BUNGE, hatuna RAIS,hatuna MAWAZIRI na hatuna WABUNGE labda Wabunge wa CDM tu. Ukimsikiliza Gavana wa Central Bank Bw. Ndulu ANASEMA UCHUMI UNAKUWA KWA KASI SIJUI YA 7% LAKINI WAKTI HUOHUO SHILINGI INAZIDI KUPOROMOKA. This is a naked contradiction ambayo kila mtu anaweza kuiona lakini Viongozi wetu wanajifanya hawaioni.

  Bila shaka kila mtu anajua kabisa kuwa KILA MBUNGE(MP) ANALIPWA POSHO YA MAFUTA KILA MWEZI KWA RATE YA TSHS.2,500/=BILA KUJALI WHETHER NI PETROL OR DIESEL. That's why hata bei ikipanda namna gani nobody cares. PENGINE WATACHACHAMAA PALE BEI ITAKAPOFIKIA KILE KIWANGO CHAO CHA TSHS.2,500.!!!!!

  Eeh Mungu naomba utusaidie Wadanganyika ili tusiendelee KUDANGANYWA NA SERIKALI HII YA CHAMA CHA MAGAMBA-CCM. Ameeeeen!
   
 18. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #18
  Aug 15, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Watu wanaongea issue za maana wanakuja mabarubaru na magabachori kuanza kuharibu.

  Back to topic:
  Hivi zile tambo za Mkulo kupunguza kodi na tozo mbali-mbali ili kupunguza bei za mafuta zimeishia wapi? au ilikuwa ni danganya toto ili bajeti ipite?, mafuta ndio yanazidi kupaa, Tanzania bana, tunadanganywa eti shilingi imeshuka thamani, may be kweli, lakini kwa nini shilingi yetu inazidi kuporomoka wakati hatuna vita, hatuna njaa na tunaambiwa 'uchumi unakuwa'?.

  Mheshimiwa JK mwezi huu nao utatuchinjia baharini tena kwa hotuba zako za mwisho wa mwezi?, tunapenda kusikia kiongozi wa nchi unasema nini kuhusu haya matatizo au J. Makamba yuko bize siku hizi na huna mtu wa kukuandikia hotuba?

  Tunahitaji kuchukua hatua.
   
 19. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #19
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />

  lizi 1 kamaliza kirakitu mliuliza kafata nini mjengoni alienda kusawazisha mambo siku 2 jibu limepatikana alicho kifuata huko bungeni tusipo kumbuka wenyewe kuingia barabarani tutaibiwa hadi nguo za ndani
   
 20. HT

  HT JF-Expert Member

  #20
  Aug 15, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  maliza ya Oman.
  Ya Tanzania tuachie watanzania, hayakuhusu. Si ulikana sio Mtz weye? Sasa mbona kila siku busy na mambo ya kwetu? Leta hadithi za Muscat na mambo ya tende na halua. Ya Tanzania tuachie wenyewe!
   
Loading...