Hoja 18 kesi ya lema tutegemee nini??

Hoja 18 kesi ya lema tutegemee nini??

dotto

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2010
Posts
1,725
Reaction score
257
WanaJF hapa chini ni baadhi tu ya hoja zilizowasilishwa kama rufaa kupinga kilichofanywa na jaji katika kumvua ubunge. Je, tutegemee nini hasa.

"[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Monday, 07 May 2012 10:00 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Lema awasilisha rufaa ya kurasa 985

Peter Saramba, Arusha

....................Pamoja na hoja za rufaa, kitabu hicho cha rufaa chenye kurasa 985 ina mwenendo mzima wa shauri, vielelezo na viambatanisho vyote vilivyowasilishwa Mahakama Kuu.

“Kimsingi ni rai yangu kuwa mtukufu Jaji Rwakibarila (Gabriel) hakutolea uamuzi mambo na hoja za msingi zinazofanya hukumu yake kukosa hadhi kisheria, kuitwa hukumu, hayo ni miongoni mwa hoja za msingi nilizoanisha kwenye rufaa niyowasilisha mahakamani juzi,” alisema Wakili Kimomogoro.

Kwa mujibu wa hati ya rufaa hiyo, hoja ya kwanza hadi nne zinapinga uamuzi wa Jaji Aloyce Mjulizi aliyesikiliza shauri hilo katika hatua za awali kwa kutupa pingamizi za awali zilizowasilishwa na upande wa utetezi kwenye kesi ya madai namba 13 iliyofunguliwa na wapiga kura watatu waliopinga ushindi wa Lema.

Miongoni mwahoja hizo ni kuwa wadai, Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo hawakuwa na haki kisheria kufungua shauri hilo kwa sababu hakuna haki yao iliyovunjwa kisheria kama wapiga kura.

Wakili Kimomogoro aliyemwakilisha Lema na mawakili wa Serikali, Timon Vitalis na Juma Masanja walidai aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Batilda Burian ndiye alikuwa na haki kisheria
kulalamikia ushindi na maneno ya kashfa yanayodaiwa kutolewa dhidi
yake na Lema.

Hoja ya tano hadi 18 zinapinga hukumu ya Jaji Rwakibarila ambapo katika suala la hukumu yake kukosa hadhi kisheria, wakili Kimomogoro anadai hakutolea maamuzi athari za wadai kushindwa kuwasilisha mahakamani CD zinazomwonyesha Lema akitoa maneno ya kashfa na udhalilishaji walizodai kuwa nazo katika hati yao ya madai.

Kimomogoro anadai Jaji alikosea kwa kutotumia hata kesi moja kama rejea kati ya kesi kadhaa zilizotajwa na mawakili wa pande zote mbili za wadai na wadaiwa.

Jaji Rwakibarila ambaye ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga pia anadaiwa kukosea kisheria kwa kukubali na kuegemea ushahidi wa mdomo pekee katika hukumu yake bila kuwepo ushahidi wa mazingira, Video wala maandishi kuunga mkono ushahidi wa mdomo.

Mrufani pia anadai Jaji alikosea kwa kutumia viwango na vigezo tofauti kwa mashahidi wa upande wa wadai na utetezi kwa kukataa ushahidi wa Leman na mashahidi wake kwa madai kuwa walikuwa na maslahi kwa sababu ni wanachama na viongozi wa Chadema lakini akakubali ushahidi wa wanachama na viongozi wa CCM kutengua matokeo.

Hoja nyingine ni kuwa hata kama Lema angetiwa hatiani kwa madai yaliwasilishwa mahakamani, bado Jaji hakustahili kutumia kifungu cha 114 cha sheria za uchaguzi kuripoti uamuzi wake kwa Mkurugenzi wa uchaguzi kwani makosa hayo hayahusiani na vitendo vya rushwa wala jinai ambavyo humzua aliyehukumiwa kupiga kura wala kugombea uongozi kwa miaka mitano.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Tusubiri October 2 sio mbali. Na sisi wapiga ramri tunasema Lema atashinda hii rufaaa kwani hapo inahitaji kuafikiwa japo hoja moja tu kati ya zote hizo 14. Na hasa hii ya kudhalilishwa bila mhusika kufika mahakamani na kuihakikishia mahakama ni madhara gani alipata kutokana na udhalilishwaji huo imetulia.
 
Wameikimbizia Dar sababu ya ile pressure walioiona jana pale Arusha ni hatari sana kama haki haitatendeka na umati ule,damu itamwagika hakika.Heri wakimbizie Dar kama wanataka kuchakachua kumlinda JK!maana alishasema Arusha sasa imetulia!!
 
WanaJF hapa chini ni baadhi tu ya hoja zilizowasilishwa kama rufaa kupinga kilichofanywa na jaji katika kumvua ubunge. Je, tutegemee nini hasa.

"[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Monday, 07 May 2012 10:00 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Lema awasilisha rufaa ya kurasa 985

Peter Saramba, Arusha

....................Pamoja na hoja za rufaa, kitabu hicho cha rufaa chenye kurasa 985 ina mwenendo mzima wa shauri, vielelezo na viambatanisho vyote vilivyowasilishwa Mahakama Kuu.

"Kimsingi ni rai yangu kuwa mtukufu Jaji Rwakibarila (Gabriel) hakutolea uamuzi mambo na hoja za msingi zinazofanya hukumu yake kukosa hadhi kisheria, kuitwa hukumu, hayo ni miongoni mwa hoja za msingi nilizoanisha kwenye rufaa niyowasilisha mahakamani juzi," alisema Wakili Kimomogoro.

Kwa mujibu wa hati ya rufaa hiyo, hoja ya kwanza hadi nne zinapinga uamuzi wa Jaji Aloyce Mjulizi aliyesikiliza shauri hilo katika hatua za awali kwa kutupa pingamizi za awali zilizowasilishwa na upande wa utetezi kwenye kesi ya madai namba 13 iliyofunguliwa na wapiga kura watatu waliopinga ushindi wa Lema.

Miongoni mwahoja hizo ni kuwa wadai, Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo hawakuwa na haki kisheria kufungua shauri hilo kwa sababu hakuna haki yao iliyovunjwa kisheria kama wapiga kura.

Wakili Kimomogoro aliyemwakilisha Lema na mawakili wa Serikali, Timon Vitalis na Juma Masanja walidai aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Batilda Burian ndiye alikuwa na haki kisheria
kulalamikia ushindi na maneno ya kashfa yanayodaiwa kutolewa dhidi
yake na Lema.

Hoja ya tano hadi 18 zinapinga hukumu ya Jaji Rwakibarila ambapo katika suala la hukumu yake kukosa hadhi kisheria, wakili Kimomogoro anadai hakutolea maamuzi athari za wadai kushindwa kuwasilisha mahakamani CD zinazomwonyesha Lema akitoa maneno ya kashfa na udhalilishaji walizodai kuwa nazo katika hati yao ya madai.

Kimomogoro anadai Jaji alikosea kwa kutotumia hata kesi moja kama rejea kati ya kesi kadhaa zilizotajwa na mawakili wa pande zote mbili za wadai na wadaiwa.

Jaji Rwakibarila ambaye ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga pia anadaiwa kukosea kisheria kwa kukubali na kuegemea ushahidi wa mdomo pekee katika hukumu yake bila kuwepo ushahidi wa mazingira, Video wala maandishi kuunga mkono ushahidi wa mdomo.

Mrufani pia anadai Jaji alikosea kwa kutumia viwango na vigezo tofauti kwa mashahidi wa upande wa wadai na utetezi kwa kukataa ushahidi wa Leman na mashahidi wake kwa madai kuwa walikuwa na maslahi kwa sababu ni wanachama na viongozi wa Chadema lakini akakubali ushahidi wa wanachama na viongozi wa CCM kutengua matokeo.

Hoja nyingine ni kuwa hata kama Lema angetiwa hatiani kwa madai yaliwasilishwa mahakamani, bado Jaji hakustahili kutumia kifungu cha 114 cha sheria za uchaguzi kuripoti uamuzi wake kwa Mkurugenzi wa uchaguzi kwani makosa hayo hayahusiani na vitendo vya rushwa wala jinai ambavyo humzua aliyehukumiwa kupiga kura wala kugombea uongozi kwa miaka mitano.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

1. Jaji Mkuu kajiingiza kwenye UAMUZI

2. Wamehamishia KESI, DAR ES SALAAM

Ina Maana LEMA ameanguka... Kwa Manufaa ya KIKWETE CLAN - CCM!!!
 
Kisheria ni wazi Lema ameshinda kesi.
 
1. Jaji Mkuu kajiingiza kwenye UAMUZI

2. Wamehamishia KESI, DAR ES SALAAM

Ina Maana LEMA ameanguka... Kwa Manufaa ya KIKWETE CLAN - CCM!!!

Mkuu hata mimi nalihisi ilo,wameona Arusha ni maafa,ila Dar waliosinzia wengi!ukweli kulikua hakuna sababu ya msingi kuhamishia rufaha hiyo Dar es salaam!sababu alizotoa CJ ni dhaifu na hazina mashiko hata kidogo!
 
Kama alishindwa kesi ya msingi hataweza kushinda rufaa.bora mara mia tusingekata rufaa ili tuingie kwenye uchaguzi
 
Huoni kuwa sababu ya kukata rufaa ni kupinga hiyo hukumu ya mwanzo. Kwani rufaa huwa si kutenda haki mkuu?
 
Kijani imekalia kuti kavu la mnazi wa mita mia kwenda juu!!! Likikatika hili litaleta balaa kupita lile bomu mliloulia mwandishi aiyekuwa na hatia halafu hadi leo mko kimya tu sijasikia jinsi gani serikali itasaidia ile familia. Kuleni raha kufa kwaja 2015.
 
Huoni kuwa sababu ya kukata rufaa ni kupinga hiyo hukumu ya mwanzo. Kwani rufaa huwa si kutenda haki mkuu?

Hawa kina mohamed, zomba, tume ya katiba e.t.c unadhani unaweza waelewesha??? Inataka moyo sana kujadili na hawa.
 
Haihitaji ramli kujua ushindi wa Lema!
Mkanga na wenzake wajiandae kulipa gharama za kesi
 
Hawa kina mohamed, zomba, tume ya katiba e.t.c unadhani unaweza waelewesha??? Inataka moyo sana kujadili na hawa.
Leo walikuwa kwenye maandamano ya kupinga ile filamu ya Mmarekani ndio maana mchana hawajaonekana hapa. Hawa wana vichwa vigumu sana
 
huoni kuwa sababu ya kukata rufaa ni kupinga hiyo hukumu ya mwanzo. Kwani rufaa huwa si kutenda haki mkuu?

achana na muhamed huyo ni mshabiki atakuumiza kichwa, baba yake ni mjumbe wa nyumba kumi ccm
 
Back
Top Bottom