Hofu yatanda Ukerewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hofu yatanda Ukerewe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]KUMEZUKA KUNDI Hatari linalojiita “Makhirikhiri” katika visiwa vya Ukerewe huko Ziwa Viktoria ambalo linahatarisha maisha ya watu kwa kuwachinja na kisha kuchukua viungo.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Kundi hilo linawateka watu umbali mrefu na kisha kuwachinja na hatimaye kuchukua viungo wanavyohitaji katika mwili huo

  Imedaiwa kuwa, hali ni mbaya kwa kuzuka kwa watu ambapo sasa wakazi wa maeneno hayo kupatwa na hofu ya uhai wao kutokana na utekwaji hovyo wa watu kiunyama

  Imedaiwa kundi hilo hutumia mbinu mbalimbali ikiwemo kuteka mabasi, pikipiki ya abiria na kisha kuamrisha vyombo hivyo kwenda wanapopahitaji na kisha kuchinja watu kinguvu na kujipatia viungo

  Tayari watu kadhaa wameshatekwa na kuuawa na kundi hilo na kujipatia viungo na kudaiwa kundi hilo hata mchana wa jua kali hutembea na kuteka watu huku wakiwa na silaha

  Moja ya viungo vinavyohitajika mara baada ya kuchinja mtu kikiwemo kichwa,Mikoni pamoja na sehemu za siri ndio viungo vikubwa wanavyohitaji watu hao[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Hofu yatanda Ukerewe
   
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kinachotusumbua watanzania ni ukosefu wa elimu pamoja na umaskini uliopindukia. Watu wanashindwa kuwa wabunifu wa shughuli za kiuchumi wanaishia kwenye imani hizi za kishirikina, za kuamini kwamba kichwa cha mtu kitampa utajiri nk. Viongozi wajao wajaribu sana kuona ni kwa namna gani watapunguza hali ya umasikini kwa watanzania, maana Kikwete kashindwa kabisa.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mkuu Lukolo lakini

  Sio hapo tu Tanzania mimi niliwahi kuwepo nchini Zambia mnamo mwaka 1980 huko Zambia kuna watu waliambia

  kuwa kama unaweza kumleta Mtu mwenye kipara wataweza kunipatia pesa nyingi sana yuko mzee mmoja huko

  Zambia nikamuuliza kwanini unahitaji mtu mwenye kipara akasema mtu mwenye upara kichwa chake ni dawa ya

  kupata utajiri nikamuogopa huyo Mzee mmoja wa ki Zambia na ukiangalia kwa makini hakuna kitu kama hicho

  kwenye kutafuta huo utajiri ni imani mbovu za watu. Ni ujinga fulani wa hao wanaotafuta Utajiri kwa njia ya

  haraka haraka hakuna kabisa Eti umkate mtu albino kichwa au miguu upate utajiri kwenda zako nani

  kakwambia umdhulumu mtu nafsi yake eti wewe uwe tajiri hakuna kitu kama hicho haikubaliki kabisa. Ni

  Ukosefu wa elimu, Umasikini na ajira ndio unaochangia watu wachache kufanya ujinga kama huo.
   
 4. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mbona eneo la ukerewe ni dogo sana kiulinzi?
   
 5. S

  Simba Yuda Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hamieni visiwa vya Ukara huenda mkasarimika:target:

   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hiyo imani ya kipara lazima itakuwa ilianzia Mbeya. Maana Mbeya ndiyo kitovu cha uchawi africa mashariki kusini na kati. Yaani hizi habari za vipara vina utajiri mimi nimezisikia tangu nikiwa mdogo na tangu wakati huo watu wenye vipara walikuwa hawaonyeshi kabisa. Ninachodhani hapa tatizo ni elimu tu. Hakuna kingine ujinga ukishakuwa mwingi utajikuta unaamini hata vitu ambavyo havipo katika dunia hii.
   
 7. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Nchi hii haina polisi, ina sungu sungu! Period! Pole kwa victims.
   
 8. q

  querauk Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ushirikina ukerewe ni moja ya sifa za kabila hilo.
   
Loading...