Hofu ya ushirikina....waalimu waendelea kugoma.................. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hofu ya ushirikina....waalimu waendelea kugoma..................

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 17, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,461
  Likes Received: 418,969
  Trophy Points: 280
  Walimu wagoma kurejea kazini


  na Moses Ng'wat, Mbeya


  [​IMG] WANAFUNZI wa shule ya msingi Chindi, wilayani hapa wameshindwa kuanza masomo kutokana na walimu wao 12 kugoma kuendelea na kazi shuleni hapo licha ya kuhakikishiwa usalama.
  Mwishoni mwa mwaka jana, walimu 12 wa shule hiyo iliyoko Kata ya Msangano, walikimbia shule hiyo kwa madai ya kufanyiwa ushirikina. Hata hivyo serikali ya wilaya kwa kushirikiana na viongozi wa kimila waliingilia kati sakata hilo na kutangaza kulimaliza huku wakiwaomba walimu hao kurejea kazini.
  Baadhi ya walimu hao walipohojiwa na Tanzania Daima, walisema hawako tayari kurudi kufanya kazi katika mazingira ya shule hiyo kwa kuwa yanahatarisha usalama wao licha ya serikali kutoa agizo la kuwataka warudi.
  Katika mahojiano hayo, walimu hao walisema msimamo wao ni kumtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuwapangia vituo vingine vya kazi badala ya kuwalazimisha kuendelea kufanya kazi katika mazingira ambayo tayari yamewaathiri kisaikolojia.
  Hata hivyo, walieleza kuwa endapo uongozi wa wilaya hiyo hautasikiliza hoja yao ya kutafutiwa vituo wapo radhi kuacha kazi.
  Mratibu elimu kata wa Msangano, Osia Mwanyamba, alithibitisha shule hiyo kushindwa kuanza kazi kutokana na kukosa walimu baada ya walimu wote 12 waliokuwa wakifundisha kugoma kurejea shuleni hapo.
  Mkuu wa wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo, alipohojiwa kuhusiana na suala hilo alisema hajapata taarifa ya walimu hao kutoripoti katika kituo chao cha kazi na kuahidi kulifuatilia.
  Desemba mwaka jana, walimu walianza kuanguka na kupoteza fahamu, wengine kuona giza wanapokuwa wakifundisha darasani, na wakati mwingine kujikuta wamelala nje ilihali walilala ndani vitendo ambayo viliripotiwa kuwa ni vya kishirikina.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,461
  Likes Received: 418,969
  Trophy Points: 280
  Anayeogopa ushirikina ni dhahiri uhusiano wake na Mwenyezi Mungu ni dhaifu..................................
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,461
  Likes Received: 418,969
  Trophy Points: 280

  Walimu waliorogwa wagoma kurejea shule

  Imeandikwa na Joachim Nyambo, Mbozi; Tarehe: 17th January 2011 @ 09:04 Imesomwa na watu: 11; Jumla ya maoni: 0


  WALIMU 12 walioacha kazi katika Shule ya Msingi Chindi iliyopo wilayani hapa kwa madai ya kurogwa na mwenzao, hawajarejea shuleni hapo kuendelea na kazi hata baada ya viongozi wa dini wakishirikiana na Serikali pamoja na waganga wa jadi kusafisha hali hiyo.

  Shule hiyo ilifunguliwa mwanzoni mwa wiki iliyopita sambamba na shule nyingine mkoani hapa na ilitarajiwa angalau katikati ya wiki, walimu hao wangeanza kurejea kutekeleza mwito wa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo.

  Kimolo hivi karibuni alilazimika kushiriki katika ibada maalumu ya kukemea mapepo katika shule hiyo ili kuweka mazingira mazuri kwa walimu hao kurejea.

  Ibada hiyo ilifanyika kwa wakati mmoja na shughuli za waganga wa jadi za kufukua baadhi ya vitu walivyodai kuwa vilifukiwa na wachawi, akiwemo mmoja wa walimu hao (jina limehifadhiwa), ili wenzake washindwe kufanya kazi yao.

  Baada ya kumalizika kwa ibada hiyo na shughuli ya waganga hao, viongozi hao wa dini na jadi, kila mmoja alitoa kauli ya kuondoa hatari iliyokuwepo katika eneo hilo la shule.

  Kutokana na uhakika huo, Kimolo alitoa mwito kwa walimu waliokimbia kurogwa kurejea na kuagiza mwalimu anayetuhumiwa kuwaroga wenzake ahamishwe shuleni hapo.

  Hata hivyo mpaka Ijumaa wiki iliyopita, zikiwa ni siku tano zimepita tangu kufunguliwa kwa shule hiyo, hakuna mwalimu hata mmoja kati ya waliokimbia aliyekuwa amerejea shuleni hapo.

  Gazeti hili lilifika shuleni hapo na kuwakuta wanafunzi peke yao, ambao walilalamika kuwa tangu wafungue shule, walimu hao hawajafika na wamelazimika kujisomea wenyewe na kuiomba Halmashauri iangalie uwezekano wa kuwasaidia.

  "Tunalazimika kujisomea wenyewe kwakuwa walimu walioondoka baada ya kurogwa hawajarudi.Tunaomba Serikali kupitia halmashauri itusaidie kuwarejesha walimu wetu ili tuendelee na masomo," alisema mmoja wa wanafunzi shuleni hapo aliyeomba kutotajwa jina.

  Baadhi ya walimu hao hivi karibuni walinukuliwa wakisema hawako tayari kurejea kijijini hapo kwakuwa hawana imani kuwa matatizo hayo yameisha.

  Walimu hao ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao, walisema wapo tayari kuendelea na kazi iwapo watahamishwa kijijini hapo na kupangiwa kazi katika shule zilizo mbali na kijiji hicho.

  Walionesha kuendeleza msimamo wa kuacha kazi iwapo mamlaka husika hazitashughulikia ombi lao la kuhamishwa, wakidai hawako tayari kuvumilia kwa yale yaliyowasibu katika Kijiji cha Chindi.

  Mratibu wa Elimu wa Kata ya Msangano kilipo kijiji hicho, Osia Mwanyamba alisema amelazimika kwenda kufundisha yeye mwenyewe huku akitarajia kuazima walimu wengine wanne kutoka shule ya jirani.

  Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo alipohojiwa kuhusu suala hilo alisema hajapata taarifa ya walimu hao kutoripoti katika kituo chao cha kazi na kuahidi kulifuatilia suala hilo.
   
Loading...