Michael Uledi
Senior Member
- Mar 29, 2023
- 132
- 323
Nimemsikia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan na kupata ngumu faraja sana ndani ya kipindi cha mwezi mmoja nyuma! Kuna kitu nimejifunza na kuanza kutamani sana kufanya kazi na Serikali yake ya Awamu ya Sita.
Tamaa yangu imeongezeka sana baada ya mara ya kwanza kumsikia akikerwa kwa dhati kabisa na report ya CAG na kwa mara ya kwanza kutamka maneno magumu kwake yaani pumbavu, stupid na zaidi kuhoji kama Wezi wa Mali za Umma je, watazikwa na hizo fedha wanazowaibia Watanzania?
Kwangu kauli ile ya kizalendo imenipa picha kwamba labda viongozi wanawake ndani ya Nchi hii inawezekana wakawa na "Kauoga'' fulani katika kulinda maslahi ya Taifa. Jana tena katika baraza la Kitaifa la Idd nimemsikia akilia na malezi ya watoto wetu hasa watoto wa kiume kwa kuwataka Wazazi "Wakomae" katika malezi ya watoto kwa ajili ya maslahi ya baadae ya Taifa.
Naona dhamira njema ya Mh. Rais ya kutaka kulinda Uadilifu na kujenga Taifa la watu wenye hofu ya Mungu. Ukishakuwa na Rais mwenye hofu ya Mungu Taifa linapona na mengi.
Umebakiza sadaka moja kwa Mungu baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan Mh. Rais, kamilisha sala yako kwa Mungu wako.
Nenda kawachukulie hatua wahuni wote ambao wamekuchafua sana kupitia Report ya CAG. Hakuna njia bora ya kuipa heshima Serikali yako na kupunguza maneno ya huku mtaani zaidi ya kudeal angalau kwa kuwaondoa ofisini wale wote wanataka kuivua nguo Serikali yako.
Naona sasa naanza kuwa mmoja wa vijana ambao naanza kutamani kufanya kazi na Serikali yako ya Awamu Sita. Naona nia yako njema na naona nina wajibu wa kukusaidia kufikia malengo ya Taifa lako mpaka mwaka 2030.
Mpaka hapa, tayari 2025 count my vote. Ntazitafuta kura zao asubuhi mchana na usiku.
Kazi Iendelee sasa!
Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app