Hofu ya Kuzeeka Wasichana Huolewa na Yeyote

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Hivi sasa watafiti wengi wameonyesha kukubaliana na jambo hilo. Wanasema kwamba, wasichana wengi hubabaika na kufanya mambo yenye kuwaumiza kutokana na hofu kwamba, muda unakwenda haraka na watazeeka. Lakini pia huamini kwamba, starehe zitaisha.

Watafiti hao wanasema, kutokana na maumbile ya wanawake, ambapo miili yao hupevuka haraka, wengi huhofia sana umri. Wamebaini kwamba, mwanamke anachukia sana kuambiwa amezeeka au hujihami zaidi kuliko mwanaume asionekane kwamba, amezeeka. Kuzeeka kwa wanawake walio wengi kuna maana ya kuchusha na kutokupendwa tena.

Mwanamke anapofikia umri wa miaka 25 huanza kujiuliza kuhusu kuolewa, lakini pia huanza kujiuliza kuhusu watoto. Kama hajaolewa, hana mchumba au anahisi kutokupata mtu anayeamini atamfaa, huanza kuhofia. Anapofikia umri huo huanza kujiuliza pia kuhusu watoto.

Hofu za maisha ya upweke ya baadaye humjaa na kumfanya kuanza kubabaika. Ni katika kubabaika huko, ndipo ambapo huweza kufanya mambo ambayo watu wengine hujiuliza ni kitu gani kimemsibu.

Kwa kuhofia kuchelewa kuolewa au kutoolewa kabisa, anaweza kumkubali mtu ambaye vinginevyo asingekubali kuwa naye kama mume. Kwa hofu ya kuingia kwenye umri mkubwa akiwa hana mume, humbeba yeyote.

Katika mazingira kama haya ndipo ambapo unakutana na wale ambao huolewa kwa madai ya kuondoa mkosi. Anachotaka ni kuolewa na mwanaume yeyote, ili mradi ionekane kwamba, maishani mwake naye alishawahi kuolewa.

Kuna wengine ambao huamua kuzaa na mwanaume ambaye anajua hataweza kumwoa. Hapa wengi huzaa na waume za watu. Inazidi kuelezwa kwamba, kubabaika huku huweza kumsababishia mwanamke kuingia kwenye kusongeka sana au kumwingiza kwenye kujichukia kunakopindukia mipaka.

Kwa sababu ya kutoolewa, mwanamke anakuwa mkali sana, mkorofi sana na mwenye kuwaona wengine wote kama adui zake.

Lakini wasichokijua wanawake wengi ni kwamba, kupata mume au mtoto siyo jambo ambalo linampa ukamilifu. Hata mwanaume hawezi kukamilishwa na mke na watoto, bali hukamilika mwenyewe kwanza.

Imani kwamba, mtu asipokuwa na ndoa haheshimiwi au asipokuwa na watotohajakamilika, ni ya zamani sana.

Kuna walio kwenye ndoa ambao maisha yao ni magumu na mabaya kiasi kwamba, wanajiuliza ni kitu gani kiliwaingiza huko. Kuna wenye watoto ambao watoto hao wamechukua maisha yao kwa mikono yao.

Mifano ni mingi sana hapa nchini ambapo kuna watoto wamewauwa mama zao kwa sababu mbalimbali.

Mwananchi
Photo_1682478577197.jpg
 
Mwanamke anapofikia umri wa miaka 25 huanza kujiuliza kuhusu kuolewa, lakini pia huanza kujiuliza kuhusu watoto. Kama hajaolewa, hana mchumba au anahisi kutokupata mtu anayeamini atamfaa, huanza kuhofia. Anapofikia umri huo huanza kujiuliza pia kuhusu watoto.
Mambo kwa ground hayako hivi. Njoo huku nje utakutana na sie wenye early 3rd floor na hatujawahi waza hayo 😁
 
Kuna wengine ambao huamua kuzaa na mwanaume ambaye anajua hataweza kumwoa. Hapa wengi huzaa na waume za watu. Inazidi kuelezwa kwamba, kubabaika huku huweza kumsababishia mwanamke kuingia kwenye kusongeka sana au kumwingiza kwenye kujichukia kunakopindukia mipaka.
😂😂
Hamna mtu anayetaka kuwa singo mama. Na kama yupo basi atajilengesha kwa mkaka/ mbaba mzuriii, ili apate katoto kacute.
 
Ulimwengu unawahangaisha sana wanawake mpaka wanasahau kusoma alama za nyakati.......

Stara pekeee ya mwanamke na heshima ya mwanamke kwenye jamii ni ndoa...... mwanamke anatakiwa kipindi kile ambacho anawaka usichana atafute na achague mtu sahihi wa kumuoa na sio kuutumia mwili wake kuendesha maisha.......
 
asiye na bahati, habahatishi.
Wangapi waliolewa at their mid 20s, wakafika 30s ndoa chali.
 
Ulimwengu unawahangaisha sana wanawake mpaka wanasahau kusoma alama za nyakati.......

Stara pekeee ya mwanamke na heshima ya mwanamke kwenye jamii ni ndoa...... mwanamke anatakiwa kipindi kile ambacho anawaka usichana atafute na achague mtu sahihi wa kumuoa na sio kuutumia mwili wake kuendesha maisha.......
.......kweli kabisa ktk umri mdogo wanakuwa na advantage ya kumfanyia screening kila mwanaume anaejitokeza, Sasa wao huwa wanageuza kuwa kipindi cha kukusanya fedha na kuleta pozi Kwa wanaume, tena huwaletea pozi hata wale walio serious, ukizungumzia ndoa tu, hapo ndo anakuona we hamnazo kabisa ie old fashion.........
 
ubaya ni kuwa wanafikiriaga wana muda.
 
Back
Top Bottom