Hodi hodi

BENGA FELIX

New Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3
Reaction score
0
HODIIIIIIIIIII! Mimi ni mdau mpya katika hii forum ya jamii.Kwanza ninayo furaha kubwa sana kujiunga na hii kitu na najua kupitia hii kitu naweza kulonga vitu vingi sana bila msirimkali kunifungia kwa muda usiojulikana kama gazeti la mwanahalisi. Ninatamani ningekuwa nimejiunga tangu zamani ningekuwa nilishasema mambo mbalimbali yenye uhalisi, kusimulia mastori mbalimbali na kuburudisha hadhira yangu kwa vichekesho mbalimbali vyenye kuburudisha hebu kwa kuanza tu naomba nitoe hivi hapa:

1)kuna jamaa alikamatwa na police jamii akikojoa kwenye eneo lililoandikwa usikojoe hapa,yule police akamwambia jamaa kuwa faini ya kosa lake ni shilling 5000,jamaa akaamua kulipa faini na akatoa noti ya shiling elfu kumi 10000 lakini polisi akamwambia kuwa alikuwa hana chenji kwahiyo akojoe tena ili wamalizane. MWISHO. Unaionaje stori hii.

2)jamaa mwingine alimpa pregnancy mtoto wa watu na baba mtoto akasema atauwa mtu kutokana na kitindo hicho, lakini jamaa akachonga na baba yake yule msicha kwamba atampa shilling 1000,000,000 kama mtoto atakuwa ni mvulana na atampa shilling 6o,ooo,000 na gari endapo mtoto atakuwa msichana. basi jamaa akamhoji kuwa itakuwaje endapo mtoto atakufa wakati wa kujifungua, basi baba yake yule msichana akasema kuwa kama itatokea hivyo Basi itabidi jamaa ampe mimba nyingine.MWISHO.


NOTE. WAKATI NAJIUNGA NA HII JAMII FOROM NILITUMIA PROFILE NAME AMBAYO SIKUTAKA ITUMIKE LAKINI SIJUI JINSI YA KUBADILISHA HIVYO PLEASE NAOMBA KAMA KUNA MDAU ANAJUA JINSI YA KUIBADILI JINA ANISAIDIE.ASANTE
 
Da kaaaaaaaazi kweli kweli, karibu sana japo nami bado kamba haijanitoka mguuni.. subiri wataalam hawako mbali, sasa ivi wataingia kukusaidia
 
Karibu sana inaonyesha umeingia ukiwa mcheshi. Tahadhari Vigezo na masharti kuzingatiwa.
 
Karibu...umeingia na ku copy na ku paste story mbili...kwa mwendo huu angalia usije kula ma ban ya kufa mtu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…