Mulhat Mpunga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 27,650
- 16,731
1. Utakuta mtu anatembea barabarani huku anavuta sigara hajali kuwa moshi wa hiyo sigara yake unakera watu
2. Mtu anatembea barabarani anatema mate au anapenga kamasi hovyo hovyo kila mahali bila ustaarabu
3. Mtu anakupa business card siku unamtafuta ukipiga namba za simu zilizoko kwenye card hapatikani
4. Hawa wamachinga wanaouza vitu wakitumia kispika saa zote kikisema 'dawa ya mende, mchwa, mba na mapunye inapatikana hapa' kinarudiarudia kwa kweli kinaleta kero
Na mengine mengi yenye kero katika jamii yetu, Hii inakera sana
5. Inakera sana msomi anakula kwenye basi na kutupa mifuko na chupa dirishani!
6. Inakera sana mtu anaongea na simu kwa sauti ya juu kwenye public!
7. Inakera sana dada mrembo anatupa ovyo maganda ya chocolate!
8. Inakera sana mtu ameomba simu ya mtu apige anaanza kuangalia salio!
Lol..huyu ni wa kuzaba kibao kabisa maana hana 'adabu'!
12. Inakeresha sana kwa mara yakwanza unapomwambia demu achague sehemu ya date na anakupeleka kwenye kiota cha bei chafu ambacho yeye na familia yake mzima hawajawahi kukanyaga
13. Inakeresha sana mbu, paka, mbwa, na nzi wanapovamia kituo cha raha chini ya mti nyakati za jioni
14. Inakeresha na kutapisha wauza samaki, mchicha, DVD, sidiria, vinyago n.k wanapovamia meza ya makulaji kwenye bar za chini ya mti
15.bodaboda inapowekewa honi ya lori na kupigwa hovyohovyo inakerasana.
Hiyo namba 10 imenikuta, kwa mama mwenye nyumba wangu, ni mwezi wa 3 sasa na mbaya zaidi anaingia mpaka chumbani ninakolala, si ndo mwanzo wa kutonilipa huo jamani maana duh!!!!!9. Dereva anaona mko mnasota kwenye foleni anatoka nyuma anataka aje akae mbele yako kama vile ana haraka kuliko watu wengine
10. Mtu anakujia ana shida anaomba umkopeshe pesa kwa ahadi ya kukurudishia kesho, hiyo kesho unasubiri haifiki mpaka unajuta kumkopesha
11. Mtu anakuahidi kitu na kukuomba umpigi baadae, hiyo baadae kila unapopiga hapokei simu wala hajibu meseji
aaaa umegusa ikulu!inakera sana wanao pandisha bei ya bia ovyo ovyo wkt kwenye kizibo pameandikwa 1400/=
asa wauze nini?club soda ili upunguze kilevi? Na wakikosa wateja wa hizo spana wanaenda kvnjia nyumba za watu usiku huo alaaainakera machinga kuuza vitabu na spana saa nane usiku bar watu wamelewa chakari.