Hizi ndizo shughuli zinazowapeleka Wachagga Kilimanjaro kila mwaka

Natumai wote wazima.

Huu ni mwezi wa mwisho wa mwaka
Mwezi ambao unapilika nyingi sana za kumalizia dk za mwisho.

Kuna makabila mengi sana yanayopenda kuumalizia mwezi huu kwa kwenda makwao yaani sehemu walikozaliwa.
Nitazungumzia Wachagga sababu mi mwenyewe natokea huko.

Sababu za kwenda makwao December
1. Kupumzika,hii ni baada ya kufanya kazi kwa mwaka mzima,bila kwenda.
2. Kuchinja mbu zi, hapa kuna za matambiko na za kawaida. Matambiko haya ni kushukuru wazee wao kwa baraka walizopata kwa kipindi chote.
3. Sherehe mbalimbali. Komunuo, kipaimara, ubatizo, Xmas na mwaka mpya wenyewe.
4. Utambulisho mbalimbali kama mke, mchumba,gari jipya,nyumba mpya n.k
5. Kukutana na watu mbalimbali ambao hamuonani baada ya kipindi hicho kama, classmates, majirani,ndugu na jamaa.
6. Utekelezaji wa miradi mbalimbali kama ujenzi wa nyumba, ukarabati wa nyumba, njia mashamba n.k

Kutokana na sababu hizo wanaokwenda ni watu wote wa dini zote

Ukienda tofauti na kipindi hiki huwezi kukuta watu wengi sana. Kipindi hiki hakuna kaya utakayokuta haina furaha.

CHANGAMOTO
Kama umeenda na huna chochote kitu,utakumbana na ubaguzi na manyanyaso makubwa sana labda usiwe mzawa wa hapo.
Vijana wenzako wanawajengea wazazi wao nyumba ww huna kitu,wameenda na magari ww huna kitu. Umeshindwa hata kujenga choo hapo nyumbani?

Maswali fikirishi
Utaulizwa mjini ulifata nini? Bora ungelima hata huku shambani tu tujue kabisa kweli huna kazi?

Kama ni Dar, utaulizwa kwani Daslama unayokaa wewe ni hiyo hiyo anakaa mtoto wa Massawe? Utajibu nini hapo?

Kipindi hicho wenye vitu,mali pesa ndio wenye akili na maamuzi. Una vyeti vyako,una elimu kubwa lakini kama hujafanya chochote au hauko vizuri na wazazi wewe ni takataka tu.

Kwa sababu tajwa hapo juu kumbuka sio wote wanakwenda kwa sababu zote bali lazma sababu mojawapo ihusike.
Ni kipindi chenye shangwe na furaha sana.

Karibuni watu wa maeneo mengine mtupe sababu za kwenda na changamoto zake. Ruksa kujazia pia hapo.
Waambie kabisa yaani ukitaka kujua ile maana ya Christimas basi usisite kujongea Moshi kuna tofauti kubwa sana utakayo iona kwanza kuanzia tarehe 18 december ni mwendo wa mapochopocho mpaka january ushindwe mwenyewe na kule hakunaga kadi ni wewe tu na guu lako
 
Ila kuzaliwa Moshi gharama sana kiongozi

1. Harusi ya gharama
2.Shughuli za watoto gharama
3. Mwisho wa mwaka gharama
4.Ujenge nyumba ya wazazi, ya familia na ya kwako binafsi Moshi ( kama wewe ndio mwenye uwezo)
5. Usomeshe ndugu wa karibu
6. Ufanye sherehe za hapa na pale.. na ushiriki za wenzako..
7.Misiba ya gharama
Wakati wengine wakitoka ndio wametoka na nyumbani hawarud tena wala hawataki kujuana.

Hongereni wachagga...

Ndo akili inakukaa vizur mkuu ya kupambana unadhan hapa dunian tumeumbwa tuje tushangaeshangae kama mashangazi
 
Ni wale wachaga waliolowea mjini wakaa miaka mingi bila kurudi kwao hawana kitu wanaogopa kurudi makwao watachekwa na wazazi ndo nasikia kwao wamepewa jina kyasaka
Mkuu upo sahihi 100% ukiona mchaga anakwambia mimi sipandi mwaka huu...sababu kuu anaona aibu(hana kitu yani). Mchaga akifeli maisha Dar hawez rudi Moshi kirahisi (labda arudi na wa mee sana) lazma atakimbilia mikoa mingine ili kuficha aibu.

Wakati mwingine kuzaliwa mchaga ni kama mzigo yani...ole wako ushindwe maisha...unaweza tolewa sadaka wewe(jokes)
 
Kweli Mkuu, kwa hayo maswali wanayoulizwa nimeeelewa kwanini hawa Wenzetu wamekuwa Wahanga wa Ufisadi na Upigaji mkubwa Serikalini na matukio makubwa ya Uporaji. Hizo Showoff kumbe ndio chanzo kikuuu. Pole rafiki yangu Mangi kipenzi unayesota kwa kesi ya Uhujumu Uchumi. Kesho naelekea Keko kukupa pole kumbe siyo akili zako bali ni msukumo wa jamii yako daaaah.

Hiv kwa akili yko ilioko hko nyuma nan kakwambia wachaga wanataka vyeo vya Serikalini au kwa kipind chote cha miaka 5 cha jiwe cha kubambikiza mikesi ya uhujum uchum kwa kila mtu kutoka kila eneo unataka kunambia imewatikisa nini hyo yote n inferiority complex yko tu hta km mambo yawe magum kama MOTONI watarudi Makwao na watafanya Spending za kufuru mpka watu kama nyie wenye roho ya korosho na mfalme wenu mjibebe mgongon Kama ipo ipo tu.
 
Yuko kamili idara zote mkuu, jikoni swafi kabisa, chumbani sijuti kabisa na pia kwenye swala la adabu na heshima kwangu na wazazi wangu na hata ndugu zangu, najisifu na ni mkwe mpendwa wa mama malume

Mwanzo nilikua nasikia hizo habari kwamba ukioa mchaga utajuta, lakini huyu wangu ni wa mfano, nikiwahi kudate demu wa kitanga sikuona zile sifa zinazosimuliwa mitandaoni ni bure kabisa zaidi ya kupiga vizinga kila siku, demu alikua na maneno huyo unaweza usilale, anakusema mpaka unahisi kutapika

Niliwahi date msukuma, very rigid yaani, ana vimisimamo ambavyo hanina mashiko na siku zote yeye anahisi yupo perfect hata kama amekosea na hawezi jishusha

Nilidate demu mmoja wa mrwara huko, shida yake hakua mwaminifu na alikua mvivu balaa, mchafu, huwezi kumkuta anajishughulisha na chochote na amerizika kabisa

Nilipokutana na huyu dada wakichaga, nilisema hapa nabuy time tu, lakini siku zilivyozidi kwenda nikawa namwona wa tofauti na mademu wote ambao nimewahi kuwa nao

Kwanza ana akili ya maisha, na anapenda kujishughulisha, amesoma ndio lakini akili yake haijabweteka, pili ana adabu, mcha Mungu, ana upendo na heshima kwa kila mtu bila kujali ni mkubwa au mdogo, halafu chumbani, sio mtu wa kunifanya nijute, pia ni mvumilivu nina mapungufu mengi, yaani mimi najiona kama mkosaji sana kwake lakini she still loves me, heshima yake haijapungua kwangu

Kuna wakati biashara zangu ziliyumba kwa muda wa miaka miwili sikua na nyuma wala mbele, nikasema ukisikia kuachwa na mchaga ndio huku, cha kushangaza sio ndugu zangu wala ndugu zake walinotice kwamba mambo yangu ni mabaya, maisha yaliendelea kama kawaida, heshima.yake kwangu haikupungua sansana alijitahidi sana kunitia moyo na kunipa ideas pamoja na mawazo mapya ya biashara, kikubwa ambacho sikuregemea ni kwamba nilikua nasomesha wadogo zangu wawili na bi mkubwa wangu ananitegemea, alipofika kipindi cha ada alinipa full ada za wadogo zangu na pia kila mwezi alihakikisha ile support tuliyokua tunapeleka kwa bi mkubwa haikwami, na aliniambia haya ni maisha yetu na ni sirinyetu, sio lazima kila mtu ajue kwamba for now mke ndio anasupport

Kwa kuwa ameajiriwa, na alikua na biashara ya duka na sehemu ya uwakala wa gesi, mpesa,tigo pesa, crdb na pia alikua anauza vifaa vingine, akaniambia kwamba nisimamie ile biashara na kila faida itakayopatikana kule niingize kwenye mtaji wa kuinua biashara yangu mpaka ntakapoweza kusimama ndio nirudishe usimamizi kwake

Liukweli nilipambana na ndani ya miaka miwili biashara zangu zilisimama tena na maisha yakasonga

Ni mwanamke wa.mfano kwenyw familia yetu, huwa nasikitika kila rafiki zangu wanaponiambia wake zao wanawasumbua, mara hawana support yoyote ndani ya nyumba ni nikiuliza makabila ya wake zao wala sio wachaga ni makabila tanayosifika kwa mapenzi

Niseme tu, haya manenonyanayosemwa mitandaoni yanaweza kuwa kweli lakini uhalisia ni tofauti, kila kabila lina watu wabaya na wazuri kwa hiyo tusiwahukumu watu
Ndiye yule unaemuimbiaga?
 
2643660_FB_IMG_16083679040201854.jpg
 
Uchagani hata kama ni jambazi lakini ukiionekana unaleta maendeleo kwa wazazi na kwako unaonekana una akili sana.
Ukweli wengi hawaendi kwa uliyosema ila moja wapo ni kwenda kutambiana basi hakuna zaid hasa wamarangu warombo poa sana.
Ila mwaka huu tabia hiyo iliwaponza kidogo na covid ombi langu kwa mwaka huu kama hakuna ulazima bakini mlipo tusubiri ili gonjwa lipite kama ni hela ya kujenga tuma MTATUMALIZA KWA MISIFA YENU
 
Uchagani hata kama ni jambazi lakini ukiionekana unaleta maendeleo kwa wazazi na kwako unaonekana una akili sana.
Ukweli wengi hawaendi kwa uliyosema ila moja wapo ni kwenda kutambiana basi hakuna zaid hasa wamarangu warombo poa sana.
Ila mwaka huu tabia hiyo iliwaponza kidogo na covid ombi langu kwa mwaka huu kama hakuna ulazima bakini mlipo tusubiri ili gonjwa lipite kama ni hela ya kujenga tuma MTATUMALIZA KWA MISIFA YENU
Wewe hujui chochote nyamaza.
 
Uchagani hata kama ni jambazi lakini ukiionekana unaleta maendeleo kwa wazazi na kwako unaonekana una akili sana.
Ukweli wengi hawaendi kwa uliyosema ila moja wapo ni kwenda kutambiana basi hakuna zaid hasa wamarangu warombo poa sana.
Ila mwaka huu tabia hiyo iliwaponza kidogo na covid ombi langu kwa mwaka huu kama hakuna ulazima bakini mlipo tusubiri ili gonjwa lipite kama ni hela ya kujenga tuma MTATUMALIZA KWA MISIFA YENU
Mbona mm sifanyi mila wala kutambika? Wa Kutambika wapo lakini sio kila anaeenda anafanya hapo makitu
 
Hapo namba 2 hilo la mbuzi wa matambiko, acha kuwafariji makabila ambayo bado yapo gizani. Ni asilimia ndogo sana ya wachaga bado wanafanya huo ushirikina.
 
Back
Top Bottom