Hizi ndio tabia za watu ambao hawapendeki

Jitu la kienyeji

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,446
Reaction score
7,990
Watu wenye tabia hii ya Avoidance behavior utawagundua kwa viashiria vifuatavyo

Huwa hawataki mahusiano yenye kudumu na hawawezi kabisa kudumu katika mahusiano yao na watu wengine.

Ukitaka kuwa nae karibu sana mtumie muda mwingi pamoja mkiongea kwa furaha ataanza kukukwepa na kuwa na visingizio kibao...

Ukionyesha lugha ya mahaba kwake atakujibu kwa mkato .Ukiandika sms ya kuonyesha kuwa unampenda sana na kuhitaji kudumu nae maishani mwako atakujibu kwa mkato kama vile "Ok,sawa, nimekuelewa, Ahsante,hakuna tatizo,"

Katika Kipindi ambacho ana huzuni ukitaka kumpa faraja atakukwepa na ataonyesha hasira dhidi yako .Akiwa na tatizo ukimpa ushauri mzuri atapunguza mazoea na wewe....

Ukionyesha kumjali sana anajitenga na wewe.Kama upo nae kwenye ndoa utakuta hataki mahaba na wewe,hataki umsogelee,hataki uongee nae kwa lugha ya mapenzi zaidi...

Ukionyesha kumpenda sana atakujibu kua yeye anakupuuzia Tena kwa kukujibu kwa mkato. Hawezi kumfurahisha mwenza wake kwasababu ya hofu ya kujenga mahusiano yenye ukaribu sana...

Ataonyesha usiri sana ,ukitaka kuongea nae kuhusu siri zake anakukwepa. Na wala hataki mzungumzie..

Ukituma sms kwake huku unataka mtumie muda huo kuchati katika mtindo wa lugha ya mahaba zaidi anakaa kimya sana au anajibu tofauti na ujumbe wako unaoutuma...

Unaweza kumuandikia sms yenye kuonyesha hisia zako kwake anajibu "sawa ,ok, hakuna tatizo".....

Ukianza kumlaumu kwa sababu haonyeshi ushirikiano kwako anakulaumu kuwa unakuwa king'ang'anizi sana....

Kama ukichukua simu yake ukajipost kinachofuata ni kipigo au kuambiwa maneno yenye aibu....

Kama ni mwanamke na kuna mwanaume ameonyesha nia ya kutaka kuolewa naye utaona anakuwa anamzungusha sana kumpa majibu...

Ukileta habari za kutaka kumpost kwenye mitandao atakujibu vibaya sana na kuonyesha hataki mazoea ya namna hiyo....

Huwa hawawezi kudumu na mtu katika mahusiano yao.akiona unataka kujenga mahusiano ya kudumu anakukwepa..

Ukionyesha upo romantic atakujibu vibaya mpaka utajiona hustahili kupata upendo au kujiona upo na dosari kibao katika mwili wako na hustahili kupata upendo..

Huwa wanawakataa watu wenye kuwapenda sana na kuwajali sana .huwa niwenye tabia ya bandika bandua, toka mtu ingia mtu hawahitaji kudumu na mtu katika mahusiano.....

Huwa hataki umletee habari za mahaba zaidi, kumkisi, wala kumkumbatia kwa hofu yake aliyonayo ya kuogopa kujenga mahusiano yenye ukaribu sana....

Ukiwa na tatizo anaweza kukusaidia lakini ukionyesha kumpenda kwa wema wake aliokufanyia anaanza kukukwepa....

Huwa hawaonyeshi ushirikiano mzuri katika mahusiano yao.....

Sababu ya wao kuwa hivyo ni (KUKATALIWA) au KUPUUZWA kutokana na malezi yao ya utotoni.Kupigwa sana na wazazi au walezi au marafiki zake utotoni...

Kunyimwa mahitaji kutoka kwa watu aliokuwa anawategemea sana....

Huwa anaamini kuwa watu wakimzoea sana watamuumiza . Huwa haonyeshi huruma kwa watu wengine....

Haijalishi utakuwa unataka kumpenda kwa kiwango gani, yeye hawezi kukuamini wala kukupenda hata umfanyie Nini...

Ukianza kumwambia kuwa wewe huwezi kumuumiza katika mahusiano yeye haelewi chochote utaona anazidi kujitenga na wewe kabisa....

Kama upo na tabia ya kutoa sana pesa ili akupende hizo pesa,zawadi na maneno mazuri unayompatia unapoteza muda wako bure tuu....

Utapoteza pesa nyingi sana na muda wako mwngi kwa ajili yake ili kumuonyesha kuwa unampenda, Lakini ipo siku atakuacha ghafla tuu...

Ukijitoa sana kwake kwa kuonyesha kumjali kwa lengo upate upendo wake utaona anakupa maumivu zaidi.....

Aina hii ya watu, Hawapendeki hata ufanye juhudi kiasi gani. Usiombe kukutana nao...

Kama unaona huwezi kuishi bila yeye utaishi kwa maumivu kila siku wala hajali maumivu yako. Kwake haimshitui hata...
 
Ila mambo ya kupost kwenye mitandao hapana.Hili ni jambo la mtu binafsi mwenyewe
 
  • Thanks
Reactions: THT
Hao watu ndio wanapatikana pande zipi za nchi Mira mbane
 
Si useme wazi tu mkuu unawazungumzia watu wa kigoma
 
Hayana formula hayo mambo utakutana na bongo movie ataku actia mpaka unashangaa.
 
Suluhu ni Hassan 😂

Suluhu ni kama unampenda mtu naamini una feel anavyojiskia, fanya yale ambayo upendo unakufanya ufanye kwa ajili ya huyo mtu na usiweke matarajio yoyote juu yake...Fanya kwa sababu unampenda! Na ukiyafanya kwa utulivu bila matarajio hayatakuumiza na wala hutaona kama unaji- sacrifice 😊 Pale utakapohisi umechoka au vipi ujue hukumpenda kama unavyodhani.

Sikuzote upendo hushinda!
aaaaa wewe huko ni mwendelezo wa kumvimbisha bichwa.

napeleka milembe mimi.
 
Watu wenye tabia hii ya Avoidance behavior utawagundua kwa viashiria vifuatavyo

Huwa hawataki mahusiano yenye kudumu na hawawezi kabisa kudumu katika mahusiano yao na watu wengine.

Ukitaka kuwa nae karibu sana mtumie muda mwingi pamoja mkiongea kwa furaha ataanza kukukwepa na kuwa na visingizio kibao...

Ukionyesha lugha ya mahaba kwake atakujibu kwa mkato .Ukiandika sms ya kuonyesha kuwa unampenda sana na kuhitaji kudumu nae maishani mwako atakujibu kwa mkato kama vile "Ok,sawa, nimekuelewa, Ahsante,hakuna tatizo,"

Katika Kipindi ambacho ana huzuni ukitaka kumpa faraja atakukwepa na ataonyesha hasira dhidi yako .Akiwa na tatizo ukimpa ushauri mzuri atapunguza mazoea na wewe....

Ukionyesha kumjali sana anajitenga na wewe.Kama upo nae kwenye ndoa utakuta hataki mahaba na wewe,hataki umsogelee,hataki uongee nae kwa lugha ya mapenzi zaidi...

Ukionyesha kumpenda sana atakujibu kua yeye anakupuuzia Tena kwa kukujibu kwa mkato. Hawezi kumfurahisha mwenza wake kwasababu ya hofu ya kujenga mahusiano yenye ukaribu sana...

Ataonyesha usiri sana ,ukitaka kuongea nae kuhusu siri zake anakukwepa. Na wala hataki mzungumzie..

Ukituma sms kwake huku unataka mtumie muda huo kuchati katika mtindo wa lugha ya mahaba zaidi anakaa kimya sana au anajibu tofauti na ujumbe wako unaoutuma...

Unaweza kumuandikia sms yenye kuonyesha hisia zako kwake anajibu "sawa ,ok, hakuna tatizo".....

Ukianza kumlaumu kwa sababu haonyeshi ushirikiano kwako anakulaumu kuwa unakuwa king'ang'anizi sana....

Kama ukichukua simu yake ukajipost kinachofuata ni kipigo au kuambiwa maneno yenye aibu....

Kama ni mwanamke na kuna mwanaume ameonyesha nia ya kutaka kuolewa naye utaona anakuwa anamzungusha sana kumpa majibu...

Ukileta habari za kutaka kumpost kwenye mitandao atakujibu vibaya sana na kuonyesha hataki mazoea ya namna hiyo....

Huwa hawawezi kudumu na mtu katika mahusiano yao.akiona unataka kujenga mahusiano ya kudumu anakukwepa..

Ukionyesha upo romantic atakujibu vibaya mpaka utajiona hustahili kupata upendo au kujiona upo na dosari kibao katika mwili wako na hustahili kupata upendo..

Huwa wanawakataa watu wenye kuwapenda sana na kuwajali sana .huwa niwenye tabia ya bandika bandua, toka mtu ingia mtu hawahitaji kudumu na mtu katika mahusiano.....

Huwa hataki umletee habari za mahaba zaidi, kumkisi, wala kumkumbatia kwa hofu yake aliyonayo ya kuogopa kujenga mahusiano yenye ukaribu sana....

Ukiwa na tatizo anaweza kukusaidia lakini ukionyesha kumpenda kwa wema wake aliokufanyia anaanza kukukwepa....

Huwa hawaonyeshi ushirikiano mzuri katika mahusiano yao.....

Sababu ya wao kuwa hivyo ni (KUKATALIWA) au KUPUUZWA kutokana na malezi yao ya utotoni.Kupigwa sana na wazazi au walezi au marafiki zake utotoni...

Kunyimwa mahitaji kutoka kwa watu aliokuwa anawategemea sana....

Huwa anaamini kuwa watu wakimzoea sana watamuumiza . Huwa haonyeshi huruma kwa watu wengine....

Haijalishi utakuwa unataka kumpenda kwa kiwango gani, yeye hawezi kukuamini wala kukupenda hata umfanyie Nini...

Ukianza kumwambia kuwa wewe huwezi kumuumiza katika mahusiano yeye haelewi chochote utaona anazidi kujitenga na wewe kabisa....

Kama upo na tabia ya kutoa sana pesa ili akupende hizo pesa,zawadi na maneno mazuri unayompatia unapoteza muda wako bure tuu....

Utapoteza pesa nyingi sana na muda wako mwngi kwa ajili yake ili kumuonyesha kuwa unampenda, Lakini ipo siku atakuacha ghafla tuu...

Ukijitoa sana kwake kwa kuonyesha kumjali kwa lengo upate upendo wake utaona anakupa maumivu zaidi.....

Aina hii ya watu, Hawapendeki hata ufanye juhudi kiasi gani. Usiombe kukutana nao...

Kama unaona huwezi kuishi bila yeye utaishi kwa maumivu kila siku wala hajali maumivu yako. Kwake haimshitui hata...
Jinsi ya kujinasua na hizi tabia, nahisi umenigusa mimi kila kitu, huwa sipendi kupendwa sana na msichana na pia huwa sipendi kudumu wala kuzoeana sana, tusaidie na tiba ya tatizo hili ata nikitumiwa sms najibu wakati ninaojisikia mimi, nikipigiwa simu naweza kuacha kupokea au nipokee na kumwambia"" subiri kidogo nakupigia"" Naomba msaada.
 
Back
Top Bottom