Hizi ndio ndoa za kibongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi ndio ndoa za kibongo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 4, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  BI. SADYA OTHUMAN [37] amejikuta akipata aibu ya mwaka baada ya kutukanwa matusi ya nguoni mbele ya hadhara ya watu kwa kile kilichodaiwa kutumia fedha ya mume wake isivyo halali
  Tukio hilo limetokea juzi mishale ya saa 11 jioni huko maeneo ya Yombo Vituka jijini Dar es Salaam katika eneo wanakoishi wanandoa hao

  Katika kile ambacho hakikutarajiwa mume wa mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina moja la Kibwana[ 54] alianza kwa kumpa kichapo mke wake huyo na kuanza kusikika kwa mayowe ya mwanamke huyo kuomba msaada kwa majirani ili aweze kuokolewa katika kipigo kinachomkabili ndani kwake

  Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio walidai kuwa, mwanamke huyo alipata mkongĀ’oto kutoka kwa mume wake huyo kutokana na kutumia kiasi cha fedha cha shilingi elfu themanini bila kutoa taarifa kwa mume wake huyo

  Imedaiwa kuwa kiasi hicho cha fedha alichotumia alikipata kutoka katika kodi ya pango ya mpangaji wao aliyelipa pango la nyumba na kumkabidhi mwanamke huyo

  Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alikabidhiwa kiasi cha fedha cha shilingi laki moja na elfu arobaini na kuchapua kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya matumizi yake binafsi bila kutoa taarifa kutoka kwa mume wake ambaye alikuwa safarini

  Imedaiwa kuwa, juzi majira ya asubuhi mume huyo alirudi kutoka safari yake ambayo haikufahamika ilikuwa ya kikazi au la na ndipo jioni varangati hilo lilipoanza la kumuadhiridha mke wake hadharani ambapo ilidaiwa mwanamke huyo alipokea pango hilo siku tano nyuma kabla ya jana

  Mume huyo aliona kwa kuwa mwanamke huyo alichoropoka ndani na kukimbia nje ndipo alipoanza mvua ya matusi kummwagia mke wake huyo hadharani hali iliyofanya kujaza umati wa watu waishi karibu na eneo hilo kufika karibu na kushuhudia tukio hilo huku mwanamke huyo kushikwa na aibu ya mwaka kutokana na fedheha hiyo

  Hata hivyo baadhi ya majirani wa wanandoa hao walijaribu kumsihi mwanamme huyo kuacha jazba na kumtaka amsamehe mke wake hata hivyo hakukubalina na msamaha huo na kumtaka mwanamke huyo asiingie ndani na kumuamuru aende ukweni kwake na kumtupia mmoja wa mikoba yake nje iliyoambatana na shilingi elfu tano kwa ajili ya nauli

  Hadi nifahamnikshe inaondoka eneo la tukio majira ya saa 12:30 jioni iliacha mwanamke huyo akiwa maeneo hayo na baadhi ya majirani wakijaribu kumstiri katika moja ya nyumba iliyokuwa karibu na nyumba yake.
   
Loading...