Hizi ndio hekima 50 nilizojifunza nyikani

Hizi ndio hekima 50 nilizojifunza nyikani

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,778
Reaction score
8,212
01. Kukalia kiti kikubwa hakukufanyi kuwa mfalme.

02. Tunasubiri vitu vingi na kwa bahati mbaya vitu hivyo huwa havitokei.

03. Kumbuka baada ya kimbuga kupita kifuatacho ni upinde wa mvua.

04. Uovu huingia kama sindano lakini hukua kama Oak tree.

05. Thamani ya wazo ipo kwenye kulitumia.

06. Kuwa wewe muda wote kwa sababu kila mtu ameshachukuliwa.

07. Dakika moja tu ya ushindi ni malipo ya miaka mingi uliyoshindwa.

08. Ili ukue kubali udogo wako.

09. Usijaribu kumdanganya anayekuamini na usimuamini anayekudanya.

10. Kipofu ni binadamu asiye na kitabu.

11. Unavyokula tunda la mti mkumbuke mpandaji.

12. Hakuna moto unaoweza kukuunguza zaidi ya ule unaomuwashia adui yako.

13. Hakuna dini kuu zaidi ya ukweli.

14. Mjinga huchekelea anguko la mwingine mwerevu hupata onyo.

15. Walioshindwa huendelea kutoa sababu washindi hutengeneza historia.

16. Majivuno ni tabia ambayo humilikiwa na majitu felia.

17. Ukimuona nyoka anakunywa sumu hapo hakuna cha kufikiri wala kutenda ni kumtazama tu.

18. Hofu juu ya kesho hutokana na tabia zetu za kuipoteza leo.

19. Hakuna kitu kinaleta kifo kwa haraka kama kuishi kwa hofu.

20. Matatizo makubwa duniani yamesababishwa na binadamu wanaotaka kuwa muhimu zaidi.

21. Hofu inatabia ya kuvifanya vitu vidogo kuonekana vikubwa.

22. Uaminifu ni sura ya kwanza kwenye kitabu cha hekima.

23. Ubora wa fikra zako ni kielelezo cha Ubora wa maisha yako.

24. Kadri unavyojua ndivyo unavyoonekana umechanganyikiwa.

25. Uzoefu ni Mwalimu wa yote.

26. Chochote kinachogharimu fedha ni rahisi sana.

27. Kinachokupa maumivu leo ndicho kinakuimarisha kwa kesho yako.

28. Kama hakuna adui wa ndani basi adui wa nje hawezi kukudhuru.

29. Ukitaka kujua mwisho wa kitu tazama mwanzo wake.

30. Ni kheri uhuru hatarishi kuliko amani ya kitumwa.

31. Mwenye hekima hutengeneza fursa nyingi zaidi kuliko kukimbilia zilizopo.

32. Mawazo makubwa ni yale madogo.

33. Umasikini uingiapo malangoni upendo hutorokea dirishani.

34. Dunia itakuuliza wewe ni nani? Usijijua basi dunia itakuambia wewe ni nani na hautaweza kukataa.

35. Utaanza kuwa na hekima pale tu utakapoacha kufukuzia fedha.

36. Chochote unachokihofia unakipa nguvu.

37. Ushuhuda wa jicho moja ni bora kuliko Ushuhuda wa masikio mawili.

38. Ushauri wa wazee hauwezi kukupoteza.

39. Hakuna mfalme ataweza kutawala pasipo msaada wa wazee.

40. Kuna kina kirefu cha bahari katikati ya kuongea na kutenda.

41. Kama huwezi kufanya mambo makubwa basi fanya mambo madogo kwa ukubwa zaidi.

42. Mwandishi anayewaandikia wapumbavu anauhakika wa kupata hadhira kubwa.

43. Kwenye hali ya ukandamizaji kusimama katikati ni kuchagua kuwa upande wa mkandamizaji.

44. Maisha ni mchakato wa mabadiliko.

45. Anayefikiri anaweza kuinunua starehe/anasa ajue yeye ndiye anajiuza huko.

46. Usimsumbue mtu kwa kile unaweza kukifanya mwenyewe.

47. Sisi ni kile tunakirudia kila siku, ubora siyo tendo bali tabia.

48. Unapofanya jambo chukulia dunia nzima inakuangalia.

49. Watu wengi ni wengine.

50. Kama kuna kitu unakitaka ambacho haujawahi kuwa nacho lazima uwe tayari kufanya jambo ambalo haujawahi kufanya.

Inatosha kwa leo,
 
Back
Top Bottom