Hizi #KATIBA zitaeleweka kweli!?

Hizi #KATIBA zitaeleweka kweli!?

Te te..te.....mzee kala kiroba huyo..
 
Kama ndiyo, basi hakuna tena sababu ya Tanzania kuwa na wanasheria maalumu. Kila mtu atakuwa na uwezo wa kuelewa na kutafsiri sheria kwa kuisoma yeye mwenyewe.

Vinginevyo, ninasisitza watawala na viongozi wa ccm ni mumiani!.

Wanataka kunywa damu ya watanzania kupitia zoezi la katiba yao.

Ikiwa wanafunzi wa wanasoma miaka 4 shuleni, wanafundishwa na walimu lakini mwisho wa mwaka wa nne 60% hawajui walichokuwa wakifundishwa na hivyo kufeli.

inauwaje serikali hii hiii ambayo inaujua ukweli wa failures hizi na ambavyo imekuwa ikichakachua matokeo ili kuongeza ushindi kwalengo la kuficha aibu ya serikali, ijidai kusahau hili na itake kulazimisha kwamba kwa muda wa mwezi mmoja, watanzania wasome katiba wao wenyewe waielewe na la ajabu wanawalazimisha kupiga kura za ndiyo?

Watu wanaseoma degree za sheria miaka na bado wanafail. Wanasheria wanakutana mahakamani wanabishana katika sheria zile hadi kesi zinaahirishwa. Mahakimu wasomi wanahukumu kesi na baadaye tena hukumu zinabatilishwa kwa sheria zile zile, na hawa ni wasomi.

Leo inakuwaje serikali iwafanye Watanzania wapumbavu kwa kuzuia kwanza makongamano yaliyokuwa yakifanywa juu ya hii katiba, kuwanyima watu kupata elimu ya katiba, na halafu leo wanafiki kama kikwete, kina pinda na wahuni wenzao wanasema, Watanzania wasome katiba wao wenyewe waielewe na wakaipigie kura za ndio. Watanzania wangapi wanauwezo wa kuelwa katiba kwa mazingira ya kiwango cha elimu ya Tanzania?

La ajabu kuliko yote, mnawalazimisha wasome katiba ambayo haipo!. Hawajwahi hata kuiona. Huwezi mtu na akili zako ukaprint katiba 2m, halafu unataka watu 50m wote wasome hiyo katiba na kuielewa na unajua fika kwamba hata ungetoa makala 50m, ni less than 10% ndio wanaweza kuisoma na kuielewa correctly bila kuhitaji facilitation. Huu ni wendawazimu wa serikali.

Huu siyo mwanzo wa vurugu na umwagaji damu za watanzania unaoasisiwa na umafia , hila na urafi wa madaraka unalindwa na maslahi fisadi ya viongozi wa ccm?

Ccm iacheni Tanzania kwa sababu Watanzania tuna akili sasa. Hatutakubali kuangamizana kabla ninyi mnaotupeleka kwenye dimbwi la damu hamjaangamia. Na bahati nzuri tunawafahamu kwa majina, sura na mnakopatikana. Msitegemee usalama na amani katikati ya watu wenye mateso na uchungu!.
 
Maskini weeee mbaba wa watu katiba yenyewe kaigeuza yani shida kweli kweli
 
Ha ha haaa hii itakuwa ni katiba pendekezwa ila ingekuwa ya wananchi asingeshika upside down!
 
Back
Top Bottom