Mdogo wangu amekuwa akifuatilia madai yake tangu mwanzoni mwa mwezi wa pili pale NSSF Ilala. Alipojaza fomu aliambiwa arudi baada ya wiki mbili tu kila kitu kitakuwa tayari! Hivi ninavyoandika hapa ni mwezi wa pili kilasiku anapigwa kalenda na kinadada wa pale mapokezi, kila akifika pale ni ama bosi hayupo na hajasign cheque au mtandao uko chini. Naomba waandishi wa habari watembelee pale japo kwa mahojiano na wateja wowote mtakao wakuta ili mjue usumbufu na manyanyaso wayoyapata watanzania hawa wa hali ya chini baada ya kupoteza kazi kwa zaidi ya miezi sita na maisha yenyewe haya ya Dar es Salaam. Kutokana na usumbufu alioupata ndugu yangu mimi binafsi na workmate wenzangu tumeamua kuconvert to PPF japo siijui vizuri sana ila tu sitaki kusikia kitu kinaitwa NSSF tena maana mimi mwenyewe nimeshamsindikiza pale 3 times anaenda kuambulia story utadhani kaenda kuomba mkopo au msaada. Mbaya zaidi nasikia mkurugenzi wake yuko busy na harakati za kutaka ubunge huko kwao mafia huku shirika linadoda kwa utendaji mbovu!
Mkuu unaweza kunipa msaada jinsi ya kufanya the needful hapo kwenye red. NSSF is behind PPF for Everything. kama PPF unapata mafao yako Ndani ya siku tisini iweje hawa NSSF washindwe.? Eti mpaka baada ya miezi 6 ndio u Claim. huu ni unyanyasaji Live live. halafu baaada ya miezi sita bado m2 anasumbuliwa.
Nafikiri hili suala tuliongeze pale kwenye uzi wa marhemu Regia Mtema kuhusu Kero zetu tunazohitaji zizungumziwe Bungeni.
Kuna mdau alituambia kuwa PPF huduma zao kwa sasa ni angalau nafuu maana unapata kilicho chako ndani ya wiki tatu hadi nne hivyo nikaona ni bora wao kuliko hawa jamaa wa NSSF maana tayari nimejionea mapungufu yao, kuna kinadada pale NSSF ILALA wanamajibu ambayo yalinitia shaka ueledi wa kazi zao, sijui ndio watoto wa wajomba na shangazi, i wish wangekuwa wanapewa training za customer care maana hawajui kuwa mtu anayekuja pale tayari anamatatizo kibao nyuma yake ila wao wanakutreat kama umepotea njia na wala hukupaswa kuwa pale! Kuna mdau alisema Mr. Crescentius Magoli yuko NSSF na ninavyomjua ni mpambanaji na asingependa kuona huu ujinga, tulijaribu hata kutafuta namba yake but hatukufanikiwa maana walioko juu sometime huwa hawajui uozo ulioko chini hasa kama wanotendewa hawasemi na kuendelea kuumia kimoyo moyo!
Nadhani kuhamisha haiwezekani ila mimi nimeamua kusitisha michango yangu kwenda kule kuanzia mwezi huu na baada ya miezi sita lazima wanipe changu! Kama ni barua ya kujifukuza kazi nitawapelekea maana wamemtesa sana yule bwanamdogo so sina hamu nao hata chembe! Lakini wakati wanakuja kutushawishi tujiunge nao miaka 5 iliyopita walikuwa wapole na wataratibu kuliko kawaida, tukawa tunaahidiwa hata kuuziwa nyumba mpaka leo sina ninayemjua mimi aliyewahi kanunua nyumba NSSF!hivi inawezekana kuhamisha michango kutoka NSSF kwenda PPF?