Hizi hotuba za kisiasa za Rais Magufuli zitatuponza. Tuchague mambo ya kusema hadharani

Tunaweza tukasikilizwa au hapana, ukweli ni kwamba rais anatakiwa kusaidiwa jinsi ya kuchagua maneno ktk majukwaa ya kisiasa. Tunaona jinsi Rais anavyotumia jukwaa na kujisahau kwamba maneno ya rais hutafsiriwa na ofisi zote nchini na kuvuka mipaka.

Ni vibaya kwa rais kutoonesha imani na chanjo ya COVID-19 hadharani. Baadhi ya wasiwasi aliyonayo rais alistahili ibaki moyoni mwake na vyombo husika na siyo kulitangazia taifa. Yaweza kuwa yuko sahihi lakini ni vibaya kuweka uhakika mkubwa kiasi hicho kwa wananchi. Siyo wa kwanza, maana Afrika yupo rais wa Gambia aliwahi jidai kuoteshwa dawa ya UKIMWI, lakini ilikuwa ni gumzo la dunia juu ya kituko hicho.

Kwa nini Tanzania tuwe kituko cha Dunia kwa kukataa mawazo ya wanasayansi waliotangulia mbele yetu? Tutakapozidiwa tutakwenda wapi? Ni vibaya kumiliki sifa. Kama mwanzo tumebahatisha, tusizidishe imani kwamba Tanzania ni kiboko. Wengine wakiizuia wakati sisi tunabeza mbinu zao, tutakwisha.

Washauri munaosikilizwa na rais, jipangeni. Tunakoelekea miaka hii mitano ya kujiamini ni pabaya sana. Rais aandikiwe hotuba na kupunguza michapo ya pembeni na utani majukwaani, mengine yanatia aibu taifa. Siyo vizuri pia kuendelea na mifano ya ndoa, wanawake weupe, sijui nini tena.
Vipi mitano tena? Kwanza mlisema huyu sio mwanasiasa na mkamvimbisha kichwa kuwa nchi nyingine wanamhitaji au nasema uongo ndugu zangu.
 
Uzuri wa Magu sio mnafiki. Ni vizuri ukaonesha your true colour na msimamo iwe upo sawa au umekosea. Watu design ya magu wanawavuruga sana wazungu kwani huwa hawakwepeshi maneno.
Magu on trend#, mwanaume msimamo siyo kumtetemekea mtu
 
Tunaweza tukasikilizwa au hapana, ukweli ni kwamba rais anatakiwa kusaidiwa jinsi ya kuchagua maneno ktk majukwaa ya kisiasa. Tunaona jinsi Rais anavyotumia jukwaa na kujisahau kwamba maneno ya rais hutafsiriwa na ofisi zote nchini na kuvuka mipaka.

Ni vibaya kwa rais kutoonesha imani na chanjo ya COVID-19 hadharani. Baadhi ya wasiwasi aliyonayo rais alistahili ibaki moyoni mwake na vyombo husika na siyo kulitangazia taifa. Yaweza kuwa yuko sahihi lakini ni vibaya kuweka uhakika mkubwa kiasi hicho kwa wananchi. Siyo wa kwanza, maana Afrika yupo rais wa Gambia aliwahi jidai kuoteshwa dawa ya UKIMWI, lakini ilikuwa ni gumzo la dunia juu ya kituko hicho.

Kwa nini Tanzania tuwe kituko cha Dunia kwa kukataa mawazo ya wanasayansi waliotangulia mbele yetu? Tutakapozidiwa tutakwenda wapi? Ni vibaya kumiliki sifa. Kama mwanzo tumebahatisha, tusizidishe imani kwamba Tanzania ni kiboko. Wengine wakiizuia wakati sisi tunabeza mbinu zao, tutakwisha.

Washauri munaosikilizwa na rais, jipangeni. Tunakoelekea miaka hii mitano ya kujiamini ni pabaya sana. Rais aandikiwe hotuba na kupunguza michapo ya pembeni na utani majukwaani, mengine yanatia aibu taifa. Siyo vizuri pia kuendelea na mifano ya ndoa, wanawake weupe, sijui nini tena.
Tukifail tutanunua chanjo coz tutakuw na pesa, tukifaulu tutakuw yumepiga step kubwa kiuchumi💪
 
Kina Emanuel buhohela wako wapi mbn tulisikiaga Ni wahandiashi was hotuba za rais
 
Back
Top Bottom