Hizi Home theatre zinatengenezwa kwa teknolojia gani?

INSIDER MAN

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
1,736
15,858
Mambo vipi wadau, jumamos nilikua na ki event hapa home basi kuna jamaa angu ana HT ya sony akaileta ili isaidie kwa masuala ya mziki. Hii sony ina spika ndefu 2 na zingine fupi 3 tukatandaza sebule yote.

Before haijaja Sony nilikuwa naplay muziki kwa buffa langu seapiano, ila kwa masaa 3 tu ilikuwa imepata moto sana na spika zilianza koroma. Sasa tumeanza tumia sony kuanzia saa 7 mchana mpaka saa 6 usiku lakini ngoma haijapata moto na mziki unaotoka ni hatari. Hapa nimebaki na maswali kwanini isipate hata moto kdg? Yani ya baridi na muziki tuliweka sauti mpaka mwisho.

Kwenu wataalamu nisaidieni hili, nimejikuta navutiwa na Sony.
 

Shukran kwa elimu
 

Hizo motherboards za Mi Sabufa ya kichina hata haina haja ya kuagiza. Unaweza kutengeneza mwenyewe tu. Zinafanana almost zote na hazina technolojia ya ajabu. Very Basic circuits . Ndio maana hata inaweza kuungua kila mwezi bila sababu ya msingi. 🙆
 
mchina anatumia malighafi ya hali ya chini kuundia vifaa
matokeo IC ina kua kimeo, haweki heat sink/heat compound ya kutosha (au haweki kabisa) ,
michina mingi ukipiga sauti ya juu zinakufa taratib maana ICs zinachemka uko ndani

Zile IC wanazotumiaga hata hazina specific power input wala haina specific power output. Unakuta sabufa ina PMPO 20,000W halafu RMS 40W sijui wanaandikaga tu au wanapima kweli maana hata haviendani.
 
kuna jamaa nilimuona anachezea chezea hii kitu youtube,anaunga unga kupata sub woofer analotaka.

si nikaitamani na mimi!!!kuulizia bei nakuta ni $1400 nilihisi utumbo unajisokota
.View attachment 1675555View attachment 1675554
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…