Hizi hapa Aina za mapenzi

Hizi hapa Aina za mapenzi

Mstahiki Mea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
5,611
Reaction score
10,170
Kwa sasa mapenzi yanaweza kugawanywa katika makundi matatu

1. Mapenzi njiwa. Haya huwa yanawiana, wahenga husema kushibana. Aghalabu hufanywa na watu wanaokaribiana kimtazamo. Wanaokuwa katika mapenzi haya hufurahia maisha ya pamoja.

2. Mapenzi ya kuburuzwa, haya huwa yanadumu kwaajili ya kitu Fulani kinachomburuza mmojawapo na kuifanya mapenzi haya yasivunjike. Ni muhali mapenzi haya kuendelea kama kivutio kitaondoka au kuisha. Mara nyingi hapa mmoja ndiye mwenye mapenz ya kweli na hapo huwa hayajakaa sawia. Ikitoke huyo mwenye mapenz yakweli akachoka basi pia nisababu ya kuvunjika kwa mapenzi haya.

3. Mapenzi Sukulie, sukulie linatokana na mfinyazo wa sukuma liende. Haya huweza kuwa yalianza vizuri na baadaye kukosa mwelekeo. Wote wawili hakuna anayetamani kuyaendeleza. Kwa ukubwa mapenzi haya huunganishwa na watoto ingawa kiuhalisia hayamtamanishi miongoni mwa wenye nayo.

4. Mapenzi kipupwe na mapenzi ya kudonoa bado yangali yakitafutiwa data
#mawazohuru

Neno mapenzi linaweza kurejelea mahusiano ama ndoa katika muktadhaa huu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom