Hizi biashara zimevamiwa

Hizi biashara zimevamiwa

Vibanda Vya Chipsi....
Vijiwe Vya Maafisa Usafirishaji(Boda*2)...
Vimatawi Vya Mikopo(Kausha Damu)…...
 
Wanafungua fremu 10....wanao survival ndani ya miezi 6 wanabaki 4 tu... ahahaa
 
Sasa hivi naona Tanzania imekuwa nchi ya fremu za biashara .
Leo nimekwenda kariakoo majengo yote yanajengwa vifrem. Unakuta mtu ana kifrem chake chembachemba anauza zake chupi fresh maisha yanaenda analipa kodi anafanya mambo yake.
Kuna nchi za Asia Kuna mitaa ina mashopping malls tupu unatoka kwenye shopping mall moja unaingia jengine hapo tena unakodi gari kwenda kwenye shopping mall inayofuata jinsi yalivyokuwa yamechukua nafasi Kubwa.
Mimi pale kkoo sijaona shopping mall ni majengo tu ya ghorofa yamebananishwa chini kuna fremu juu appartment au hotel.
Mlimani City yenyewe ile huwezi ita ni shopping mall ila atilist panaelewekaeleweka
DDC pale napo wanajenga frem tupu, mtaani huku ndio usiseme watu hadi wanataka kuzibia majirani njia kwa kujenga frem.
Eti hadi JWTZ nao wanafanya biashara ya frem.
Kuna kipindi Dodoma halmashauri ilipiga marufuku ujenzi wa frem manake waliona zimezidi sana.
Tubadili mtazamo tungetakiwa kama kule kkko kuwe na mashopping mall ziwe na kila kitu.
Yaani nchi inakuwa ya mafrem tu hata kama hatuproduce sana tufikirie kiupana kidogo kko imeharibuwa sana na mafrem wajukuu zetu watapata shida sana kuibadili ile kko manake wengi watakuwa na maexposure ya nje ule uchafu wa pale kko watakuwa wanashangaa hawa wazee walifanya nini
Serikali ulitaka ikupe wazo la biashara ama ikuambie usiwe wakala?? Mtu kaamua kwa akili zake timamu afungue fremu wewe unakasirika nini?? Au ulitaka serikali ndio ikenge shopping malls??
 
Kila frem duka kila jengo frem Hadi tunashindwa kwenda kununua kima muuzaji unajuana nae tunajiendea pembezoni...ndio kilichobaki...hizi copy and paste NI hatari nilikuwa na biashara yangu nimeijenga kwa kuchanganya maujuzi kutoka inchi mbalimbali...mshikaji kaja kunisoma kamufua jengo Hilo Hilo ...mfanya kazi wangu nae kapest kafungua jirani alafu kanihama...zimebakia kazi ngumu wasizijua yaani NI hatari
 
Back
Top Bottom