Hizi ahadi! yupi ni Muongo?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi ahadi! yupi ni Muongo??

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by LoyalTzCitizen, Oct 25, 2010.

 1. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  [FONT=&quot]Ahadi za Profesa Lipumba na Maalimu Seif(CUF)[/FONT][FONT=&quot]
  1.Elimu ya bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu
  2.Kubana matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri
  3.Kuunda serikali shirikishi
  4.Kusimamia rasilimali
  5.Kuimarisha miundombinu
  6. Kusimamia na kuboresha afya
  7. Kuboresha kilimo, viwanda na uwekezaji
  8. Kurudisha chakula cha bure mahospitalini

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Ahadi za Dk Slaa(CHADEMA)[/FONT][FONT=&quot]
  1.Kujenga nchi isiyo na ufisadi
  2.Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
  3.Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
  4.Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais
  5.Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15
  6. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
  7. Kutoa huduma bora za afya bure
  8. kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi
  9. Kuwalipa wazee wa EAC fedha zao ndani ya siku 100
  10. Kubana matuzi Ikula (Yuko tayari kula mihogo[/FONT]

  [FONT=&quot]Maalimu Seif Sharif Hamad(CUF) [/FONT][FONT=&quot]
  1. Zanzibar kuwa kama Hong Kong – Unguja
  2.Kuendeleza mashamba ya Karume- Kibanda maiti
  3. Kubadilisha katiba na kuunda katiba mpya ya muungano na Zanzibar- Pemba
  4.Kubadilisha mfumo wa uteuzi makamishna wa tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC)- Unguja
  5. Kuwaunganisha wazanzibari ili kujenga umoja, udugu na ushirikiano-Pemba
  6. Kuwasilisha hoja ya kubadili katiba ya Zanzibar na ya Muungano-Viwanja vya Kibanda Maiti
  7. Kuondoa bajeti ya ZEC isiwe chini ya waziri kiongozi na badala yake kuwa inajitegemea yenyewe- Pemba
  8. Kuondoa ulazima wa mwenyekiti wa tume kuwa jaji na badala yake awe mtu anayejua sheria-Unguja
  9. Serikali kuundwa na vyama vyote vilivyopata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi- Unguja
  10.Kujenga jamii yenye maelewano na umoja -Pemba
  11.Kutokochagua kiongozi kwa urafiki bali kwa uwajibikaji na uadilifu -Unguja na pemba
  12.Kudhibiti vyombo vya dola vinavyofanya kazi kwa matakwa ya watu binafsi -Kibanda maiti
  13.Kukomesha rushwa-Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba
  14.Kuhakikisha ununuzi wa zabuni unakuwa wazi na wananchi kuruhusiwa kuhoji kuhusu zabuni-Jimbo la ole Pemba
  15.Kuongeza kima cha chini cha mshahara hadi Sh150,000-Mkanyageni Pemba
  16.Kubadili vikosi vyote vya usalama na kulipwa mishahara kima cha chini kulipwa Sh180,000-Chakechake Pemba
  17.Kubadilisha kikosi cha KMKM kuwa kikosi cha mwambao-Wawi
  18.Wazee kupanda daladala bure na wale wasiokuwa na watoto kulelewa bure-Majimbo ya Chakechake
  19.Kufuta michango yote ya shule za msingi na sekondari, kila mwanafunzi kuwa na kompyuta na badala ya kuishia darasa la saba sasa kuishia kidato cha sita-Hoteli ya Bwawani
  20.Kutoa kitambulisho cha kila Uzanzibari na kufuta cha Mzanzibari mkaazi- Uwanja wa Hospitali ya Mnazi Mmoja
  21.Kila mzanzibar kupata pasi ya kusafiria- Hoteli ya bwawani Zanzibar
  22.Kuanzisha shirika la ndege Zanzibar -Viwanja vya Kibanda maiti
  23.Kupandisha uchumi wa Zanzibar kutoka 6.8 hadi 15 kila mwaka kwa Zanzibar -Unguja
  24.Kutoa uhuru zaidi kwa vyombo vya habari pamoja na kusaidia uanzishwaji wa Baraza la Habari Zanzibar-Unguja na Pemba
  25. Kuweka hadharani nambari yake ya simu - Viwanja vya Kibanda miti
  26. Kubadili sheria ya uwekezwaji-Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar
  27.Kila mwanafunzi kuwa na komputa yake-Viwanja vya Kibanda maiti
  28.Akiwa rais hata waziri au mkewe atafungwa akiwa ametenda kosa-Viwanja vya Tibirizi Kisiwani Pemba
  29.Kujenga bandari ya Mkokoto na Pemba ili kuweka usafiri wa haraka wa boti ziendazo kasi-Tibirizi Kisiwani Pemba
  30. Ahadi kudhibiti kuvuja kwa mitihani- Unguja

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Ahadi za Kikwete(CCM)[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora [/FONT]

  1. [FONT=&quot]Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini[/FONT]
  2. [FONT=&quot]Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga[/FONT]
  3. [FONT=&quot]Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga [/FONT]
  4. [FONT=&quot]Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma[/FONT]
  5. [FONT=&quot]Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini [/FONT]
  6. [FONT=&quot]Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma [/FONT]
  7. [FONT=&quot]Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera [/FONT]
  8. [FONT=&quot]Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera[/FONT]
  9. [FONT=&quot]Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini [/FONT]
  10. [FONT=&quot]Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini [/FONT]
  11. [FONT=&quot]Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera [/FONT]
  12. [FONT=&quot]Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera [/FONT]
  13. [FONT=&quot]Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera [/FONT]
  14. [FONT=&quot]Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya [/FONT]
  15. [FONT=&quot]Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera [/FONT]
  16. [FONT=&quot]Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali[/FONT]
  17. [FONT=&quot]Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza [/FONT]
  18. [FONT=&quot]Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza[/FONT]
  19. [FONT=&quot]Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita [/FONT]
  20. [FONT=&quot]Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba [/FONT]
  21. [FONT=&quot]Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro [/FONT]
  22. [FONT=&quot]Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini [/FONT]
  23. [FONT=&quot]Kujenga bandari Kasanga –Rukwa [/FONT]
  24. [FONT=&quot]Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea [/FONT]
  25. [FONT=&quot]Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya [/FONT]
  26. [FONT=&quot]Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga [/FONT]
  27. [FONT=&quot]Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa [/FONT]
  28. [FONT=&quot]Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro [/FONT]
  29. [FONT=&quot]Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini [/FONT]
  30. [FONT=&quot]Kuboresha barabara za Igunga -Tabora [/FONT]
  31. [FONT=&quot]Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu [/FONT]
  32. [FONT=&quot]Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini [/FONT]
  33. [FONT=&quot]Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara [/FONT]
  34. [FONT=&quot]Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma [/FONT]
  35. [FONT=&quot]Kulinda haki za walemavu- Makete [/FONT]
  36. [FONT=&quot]Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini [/FONT]
  37. [FONT=&quot]Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha [/FONT]
  38. [FONT=&quot]Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini[/FONT]
  39. [FONT=&quot]Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora [/FONT]
  40. [FONT=&quot]Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini [/FONT]
  41. [FONT=&quot]Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma [/FONT]
  42. [FONT=&quot]Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga [/FONT]
  43. [FONT=&quot]Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini [/FONT]
  44. [FONT=&quot]Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, . [/FONT]
  45. [FONT=&quot]Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido [/FONT]
  46. [FONT=&quot]Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro [/FONT]
  47. [FONT=&quot]Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara [/FONT]
  48. [FONT=&quot]Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini [/FONT]
  49. [FONT=&quot]Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa [/FONT]
  50. [FONT=&quot]Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa [/FONT]
  51. [FONT=&quot]Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa [/FONT]
  52. [FONT=&quot]Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda [/FONT]
  53. [FONT=&quot]kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara [/FONT]
  54. [FONT=&quot]kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa [/FONT]
  55. [FONT=&quot]ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar [/FONT]
  56. [FONT=&quot]Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar [/FONT]
  57. [FONT=&quot]Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti [/FONT]
  58. [FONT=&quot]Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma [/FONT]
  59. [FONT=&quot]Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma [/FONT]
  60. [FONT=&quot]kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma [/FONT]
  61. [FONT=&quot]Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma [/FONT]
  62. [FONT=&quot]Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam [/FONT]
  63. [FONT=&quot]Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara [/FONT]
  64. [FONT=&quot]Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha [/FONT]
  65. [FONT=&quot]Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha [/FONT]
  66. [FONT=&quot]Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha[/FONT]

  Hivi hawa CCM wanavokuja na ahadi..... hayo mambo hapo juu hawaoni haya jamani!! hivi wamefanya wananchi kuwa ni wapumbavu hinyo!? kipi wameshakifanikisha kati ya walivyoaidi 2005 na sasa wanaongezea ahadi! hiki ni kigezo tosha kuwa ni wababaishaji!:peep:
   
 2. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,861
  Likes Received: 2,786
  Trophy Points: 280
  Jamani sisiem wagonjwa wa akili hao!! Ahadi zote hizo zinawezekana kwa kipindi cha miaka mitano? wasitufanye mazezeta bwana!!! Watanzania amkeni jamani kiama hicho! Jamaa anaahidi tu kwa vile hana cha kupoteza bwana anamaliza yake mitano anajiondokea kwa hiyo ndugu zangu akili kichwani!!!!
   
 3. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Ahadi za Slaa na Lipumba zinawezekana kabisa tena kwa kutumia nguvu ndogo tu ya usimamizi mzuri wa mali ya umma. Za JK Mmhh!!! Tena umesahau za Kigoma kuwa Dubai na Mwanza kuwa Califonia.....!!!
   
 4. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  katika hayo 66 kweli sioni hata moja kutimizwa! trust me! Mungu atusaidie jamaa akaishie kwenda kucheza kiduku kule Lugoba!!!:rip::rip:
   
Loading...