Hizi Adhabu kumbe bado zipo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi Adhabu kumbe bado zipo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Power G, Oct 13, 2011.

 1. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Wana JF, kuna adhabu ambazo kwa muda nimekuwa nikizisikia katika msimulizi ya watu kama vile za kukatwa mikono, kukatwa vichwa na kupigwa mawe hadi kufa. Mara zote nimekuwa nikizichukuliwa kama hadithi, kumbe ni kweli zipo mpaka leo na kesho. Tafadhali fuatana nami nikuhabarishe.

  Jana tarehe 12/10/2011 nilikuwa shughuli kidogo katika mji wa Jeddah nchini Saudia. Mnamo saa 5 asubuhi nikiwa kwenye gari nikielekea wizara ya mambo ya nchi za njema wakati tunakaribia eneo moja linaloitwa Balad (historic town) magari yote yalisimamishwa kukawa kunapita msafara mkubwa sana wa magari ya polisi yakiwa na vimulimuli na ving'ora na moja lililoonekana kama la kiraia aina ya Jeep nyekundu. Kwa mawazo yangu nilidhani ule msafara ungekuwa wa "kikwete" wa nchi hii. Msafara ulitangulia na siye tukawa kwenye msululu wa magari kwa nyuma.

  Msafara uliishia kwenye Msikiti mkubwa sana ambao uko opposite na wizara ya mambo ya nje. Watu maelfu kwa maelfu toka pande zote walikuwa wakimiminika kuelekea kwenye eneo hilo huku kukiwa na ulinzi mkali wa magari mengine yakiwa mounted na machine guns. Katika ile Jeep nyekundu alishuka askari mmoja mwenye nyota 3 akiandamana na kijana mmoja mwenye umri kama wa miaka 30 hivi akiwa amevaa kanzu. Kijana alipelekwa moja kwa moja mpaka kwenye kijukwaa ambacho kinaonekana kipo siku zote kwa ajili ya shughuli maalum.

  Saa 5 na dk 5, yule askari alimfunga kitambaa yule kijana kwenye macho kisha akaamuliwa apige magoti. Baada kama ya dak 2 aliongezeka mtu mwingine kwenye jukwaa ambaye anaonekana ana umbo la kushiba hasa naye akiwa amevaa kanzu nyeupe. Askari mwingine alitokea akiwa na jambia lenye umbo la mwezi mchanga lililokuwa kwenye ala nyeupe akamkabidhi yule jamaa mwenye kanzu aliyekuwa jukwaani. Huyu jamaa alichomoa jambia akalinyanyua kwa mkono wake wa kushoto na kulishusha mara moja sawia katika shingo ya huyo kijana na kichwa kikaruka mbali na kiwiliwili huku watu wakishangilia ikiwamo na watoto wadogo. Kutokana na ulinzi uliokuwapo sikuweza hata kuweza kupiga picha walao kwa simu.

  Katika mazungumzo niliwasikia watu wakisema ni mharifu, lakini sikuweza hata kufuatilia kosa lake lilikuwa lipi. Ila adhabu ndiyo niliyoishuhudia. Kwa kweli hiyo picha imenisumbua sana kwenye mawazo hadi sasa.
   
 2. i

  issenye JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,146
  Likes Received: 989
  Trophy Points: 280
  Hicho ndicho kitu wenzetu wanakililia kwenye mahakama ya kadhi.
   
 3. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,482
  Likes Received: 12,745
  Trophy Points: 280
  Utapata athari za kisaikolojia
  wahi hosp
   
 4. wijei

  wijei JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Ndo kadhi hiyo! Thubutu muone
   
 5. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Adhabu kama hizo zinamfaa Rostam na kundi lake.

  Nataman tungekuwa na mahakama ya kadhi.
   
 6. N

  Nasine New Member

  #6
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  mnh so bad.
   
 7. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2011
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ni sawa na adhabu nyengine za kifo,,

  Hata US si wanafanya kila siku!??
   
 8. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Makama ya kadhi inahukumu wanyonge, mtu kama Rostam hutamwona huko kwa kadhi hata siku moja.
   
 9. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hizo adhabu nyingine za kifo zinazofanywa katika nchi nyingine, sidhani kama zinatolewa hadharani hata mbele ya macho ya watoto wadogo.
   
 10. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  hakuna aliye juu ya sharia.
   
Loading...