Hivi Wilaya ya Rorya imewakosea nini CHADEMA?

Hivi Wilaya ya Rorya imewakosea nini CHADEMA?

Joined
Jun 30, 2013
Posts
21
Reaction score
14
Ikumbukwe kuwa viongozi wa ngazi za juu wa CHADEMA kwa mara ya kwanza walifika wilayani Rorya katika Operation Sangara mwaka 2008 nami nikiwa mmoja kati ya wana Rorya waliojiunga na CHADEMA katika operation hiyo wilayani hapa.Baadaye viongozi wetu walionekana tena Rorya mwaka 2010 wakati wa kampeni za Urais ambapo Katibu Mkuu Dr.W.P.Slaa alifika katika miji midogo ya Shirati na Utegi tu.

Tangu 2010 hadi sasa hakuna kiongozi yeyote wa juu aliyewahi kufanya ziara ya kichama Rorya.Kufuatia hatua hiyo Rorya imeachwa kisiwani katika siasa za mageuzi nchi hii.Jambo la kusikitisha ni pale viongozi wetu wanapopata fursa ya kufika Mkoani Mara hufika katika wilaya za Musoma mjini na Bunda tu.Dr Slaa,Mhe Mbowe,Mwana wa Haki Godbless Lema,John Mnyika,Kamanda Heche na wengine tunawaambia kuwa huku pia kuna watanzania waliochoka,tunawahitaji..njooni mseme neno nasi,nasi tutasikia kwani tuko tayari! Kama kuna mahala wana rorya tuliikosea CHADEMA,nasi ni binadamu kama mlivyo ninyi,nasi tunafanya makosa.Njooni Rorya!
 
boniface makene chukua huu ujumbe P Aweda
 
Kama kuna uongozi wa wilaya fanyeni kazi... Ukombozi
utakuja kwa kuhitambua.. Kuja kwao watakuja ila kumbuka nchi ni kubwa sana..hivyo wwatakuja
 
Kama kuna uongozi wa wilaya fanyeni kazi... Ukombozi
utakuja kwa kuhitambua.. Kuja kwao watakuja ila kumbuka nchi ni kubwa sana..hivyo wwatakuja

Uongozi wa wilaya upo lakini pengine ni kutokana na kutotembelewa na viongozi wao wakuu na operation za chama nao wamepoteza uwezo wao wa kisiasa,wamejisahau.
 
Ni kweli Chadema kimewekeza nguvu nyingi katika majimbo walipo wabunge wa chadema tu,wameyatelekeza majimbo ambayo ccm walishinda.Mfano,baada ya ccm kushinda Tarime CDM wamelipa kisogo jimbo hilo ambalo lilikuwa ngome ya kuaminika.Viongozi msipuuze kilio hicho cha wanarorya! Nendeni!
 
Back
Top Bottom