Hivi watanzania tunaweza kitu gani?

Hivi watanzania tunaweza kitu gani?

Huo ni mwanzo. Hata kilimo unaanza kwa ajili kula nyumbani kisha unaongeza kwa ajili ya kuuza kwa wengine.


Hata 2099 itakuwa haijauzwa hata moja si nje ya nchi tu, hata ndani. Tanzania hatuko serious na mambo ya kitaalam hata kidogo. Tunajali siasa na ufisadi tu.

Na kilimo cha maana chenye tija ya kibiashara mtu analima kwa malengo ya biashara. Hicho unachosema mtu analima chakula kikibaki anauza ni kdunduliza na kuganga njaa tu, wala hakiwezi kumtoa mtu.
 
Watanzaniaaa tunauwezaaa umbeaaa na kusutana only hiii tu ivyooo vingne tuwaaachie wenyewee
 
Wewe unaweza nini zaidi ya kubwabwaja na kuhororoja?

At least nimetoa mwongozo kuwa ili tubadilike na tuwe na chetu basi nini kifanyike. Kagame aliamua kuwekeza kwenye IT na soon Rwanda itakuwa hub ya Africa kwenye mambo ya IT nami nikasema kwanini tusiamue kuifanya Tanzania centre ya utabibu kwa mfano.

Haya wewe FaizaFoxy umefanya nini maana badala ya kujenga juu ya hoja unabomoa
 
Tunao uwezo wa kuongea kwa hisia na uchungu mkubwa sana juu ya uozo wa nchi hii, tunaweza majukwaani, kwenye Tv na hapa Jf, tukisha post kwa uchungu mwingi tunasubiri tuone tutapata 'LIKES' ngapi

Angalau umeonyesha uwezo wa watanzania. Haya basi tuubadilishe kwenye maendeleo kina Obama watuletee pesa za kigeni wakija kujifunza
 
Tunaweza ufisadi , umbeya, uongo na maneno mengi vitendo 0
 
Mitambo ya Gongo, maana gongo itaruhusiwa kuanzia 2015. Kwa sasa mitambo mingi iko mafichoni.
 
Watanzania wanaweza sana kujamiiana ... Thanks to tiba za nguvu za kiume kila kona ya nchi... !!! Chanjo na zile sindano za ndui zimetuharibu ubongo kiasi cha kushindwa kuhoji wizi wa maliasili zetu... Wote tumeishia kuwa Mazombie ...
Nimekuwa nikifuatilia ukosoaji wa wananchi kwa wenye nchi juu ya mambo mbalimbali. Ukosoaji huu umekwenda mbali mpaka kwenye matibabu ya mkuu wa nchi. Hapa imebidi niweke pozi na badala ya kubebwa na hoja za ukosoaji na wanaojitoa muhanga kutetea, imebidi nianze kujiuliza maswali hivi sisi watanzania tunaweza nini hasa tunachoweza kujivunia. Nikasafiri mpaka North Korea ambapo kuna kila aina ya vikwazo toka kwenye mataifa yenye nguvu lakini hatuingii hata chembe kwenye maendeleo yao. Nikafika Switzerland ambako hakuna mali asili yoyote lakini ndiyo mabingwa wa kutengeneza chocolate duniani wakati hata hawalimi. Kufika hapa nikakubali kubebwa na upepo wa wakosoaji wa matibabu ya Rais na kujiuliza hivi ni nchi gani zinazojitambua viongozi wao wanaumwa na wanakwenda kutibiwa nchi nyingine. Zinazofanya hivyo mara nyingi viongozi wake hawadumu sana.

Sasa najiuliza hivi sisi watanzania tunaweza nini jamani tukipigie chepuo kitutoe kama huko mbele kwa wenzetu? Hapo kale tuliwacheka wachina kwa kugeza vitu vya nchi nyingine, kupitia kugeza huko leo wanatisha duniani na tumebaki tu kusema miaka hiyo China ilikuwa sawa na Tanzania. We need visioned leaders who have mission to transform lives of Tanzanians, a leader who thinks about today and 200 years to come... Aagh naanza kupata hasira na najihisi kuanza kutoka nje ya msitari. Haya wanajamvi toeni mawazo ya kuijenga hii nchi
 
Kama huu ndiyo uelewa wa viongozi wetu jua hoja niliyotoa tumekwisha...
 
At least nimetoa mwongozo kuwa ili tubadilike na tuwe na chetu basi nini kifanyike. Kagame aliamua kuwekeza kwenye IT na soon Rwanda itakuwa hub ya Africa kwenye mambo ya IT nami nikasema kwanini tusiamue kuifanya Tanzania centre ya utabibu kwa mfano.

Haya wewe FaizaFoxy umefanya nini maana badala ya kujenga juu ya hoja unabomoa

Humu humu JF nawapa darsa Watanzania kila kukicha. Dogo hilo?
 
Wewe unaweza nini zaidi ya kubwabwaja na kuhororoja?

we kimdada si lazma somtim kama una cha kuandika unakausha2 mana kwa jinsi unavyoshinda na kukesha humu sis wagen tunakuheshm sna kama celbrt.wa jukwaa sasa usitak tukuone huwez chochote wkt uwezo wako wa kupost ovyovyo humu uko ju sana may.
 
Huo ni mwanzo. Hata kilimo unaanza kwa ajili kula nyumbani kisha unaongeza kwa ajili ya kuuza kwa wengine.


Malengo mhimim ya ccm kwenye bajeti zake za ndugu Wasira lipo hilo wazo?
Mkiambiwa ukweli hamtaki kuukubali ili mbadirike kwa ajiri ya manufaa ya nchi.

Mmekariri kutoa majibu hata kwa mambo yanayohtaji utekelezaji ama utafiti.
Kila jambo mnatoa majibu ya kujihamiiiiii......

Ndivyo tunavyofunzwa lakini hata huku majumbani ukihoji jambo utasikia, 'SIJAMPIGA MIMI'
 
Back
Top Bottom