Hivi watanzania tunaweza kitu gani?

Hivi watanzania tunaweza kitu gani?

Maendeleo tu

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2010
Posts
347
Reaction score
107
Nimekuwa nikifuatilia ukosoaji wa wananchi kwa wenye nchi juu ya mambo mbalimbali. Ukosoaji huu umekwenda mbali mpaka kwenye matibabu ya mkuu wa nchi. Hapa imebidi niweke pozi na badala ya kubebwa na hoja za ukosoaji na wanaojitoa muhanga kutetea, imebidi nianze kujiuliza maswali hivi sisi watanzania tunaweza nini hasa tunachoweza kujivunia. Nikasafiri mpaka North Korea ambapo kuna kila aina ya vikwazo toka kwenye mataifa yenye nguvu lakini hatuingii hata chembe kwenye maendeleo yao. Nikafika Switzerland ambako hakuna mali asili yoyote lakini ndiyo mabingwa wa kutengeneza chocolate duniani wakati hata hawalimi. Kufika hapa nikakubali kubebwa na upepo wa wakosoaji wa matibabu ya Rais na kujiuliza hivi ni nchi gani zinazojitambua viongozi wao wanaumwa na wanakwenda kutibiwa nchi nyingine. Zinazofanya hivyo mara nyingi viongozi wake hawadumu sana.

Sasa najiuliza hivi sisi watanzania tunaweza nini jamani tukipigie chepuo kitutoe kama huko mbele kwa wenzetu? Hapo kale tuliwacheka wachina kwa kugeza vitu vya nchi nyingine, kupitia kugeza huko leo wanatisha duniani na tumebaki tu kusema miaka hiyo China ilikuwa sawa na Tanzania. We need visioned leaders who have mission to transform lives of Tanzanians, a leader who thinks about today and 200 years to come... Aagh naanza kupata hasira na najihisi kuanza kutoka nje ya msitari. Haya wanajamvi toeni mawazo ya kuijenga hii nchi
 
Kujenga nchi yetu na kuwa na mipango endelevu.
 
Hatuna akili hivyo hatuwezi chochote
 
Tunaweza taarabu na mipasho......mara EPA, ESCROW, IPTL, RICHMOND, MADAWA YA KULEVYA wakati hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa na mamlaka husika kutatua swala husika.
 
Nimekuwa nikifuatilia ukosoaji wa wananchi kwa wenye nchi juu ya mambo mbalimbali. Ukosoaji huu umekwenda mbali mpaka kwenye matibabu ya mkuu wa nchi. Hapa imebidi niweke pozi na badala ya kubebwa na hoja za ukosoaji na wanaojitoa muhanga kutetea, imebidi nianze kujiuliza maswali hivi sisi watanzania tunaweza nini hasa tunachoweza kujivunia. Nikasafiri mpaka North Korea ambapo kuna kila aina ya vikwazo toka kwenye mataifa yenye nguvu lakini hatuingii hata chembe kwenye maendeleo yao. Nikafika Switzerland ambako hakuna mali asili yoyote lakini ndiyo mabingwa wa kutengeneza chocolate duniani wakati hata hawalimi. Kufika hapa nikakubali kubebwa na upepo wa wakosoaji wa matibabu ya Rais na kujiuliza hivi ni nchi gani zinazojitambua viongozi wao wanaumwa na wanakwenda kutibiwa nchi nyingine. Zinazofanya hivyo mara nyingi viongozi wake hawadumu sana.

Sasa najiuliza hivi sisi watanzania tunaweza nini jamani tukipigie chepuo kitutoe kama huko mbele kwa wenzetu? Hapo kale tuliwacheka wachina kwa kugeza vitu vya nchi nyingine, kupitia kugeza huko leo wanatisha duniani na tumebaki tu kusema miaka hiyo China ilikuwa sawa na Tanzania. We need visioned leaders who have mission to transform lives of Tanzanians, a leader who thinks about today and 200 years to come... Aagh naanza kupata hasira na najihisi kuanza kutoka nje ya msitari. Haya wanajamvi toeni mawazo ya kuijenga hii nchi

Ukileta ujuaji na uvumbuzi wa mambo tz unachekwa na kubezwa.
Tazama na fikiri wananchi wa kipato cha chini wanavyofikiri kila jambo na kuwaza mitambo ya kuboresha utengenezaji wa gongo ili iuzwe nje kama wine zingine znavyotoka mataifa mengine kama south africa, ila ccm na akina nape ambao ndio wanasikilizwa umewasikia na utawasikia kila kukicha.

Unamkumbuka yule mlemavu wa macho aliyevumbua mtambo wa kuvumbua mafuta?
Nani amejari?

Kaka, ili kutoka hapa tulipo ni lazima kuung'oa mtandao wooote wa panya ulioingia madarakani kwa ofa na rushwa.
Vinginevyo tutaongea sanan na mambo hayataenda kabisaaaaaa
 
Tunao uwezo wa kuongea kwa hisia na uchungu mkubwa sana juu ya uozo wa nchi hii, tunaweza majukwaani, kwenye Tv na hapa Jf, tukisha post kwa uchungu mwingi tunasubiri tuone tutapata 'LIKES' ngapi
 
Wewe unaweza nini zaidi ya kubwabwaja na kuhororoja?
 
Hii gari imetengenezwa na kikosi JWTZ Nyumbu.

Haya pia ni matunda yetu wenyewe.

Zinauzwawapi sasa? au ndo ukitengeneza kufikirii kuongeza uzarishaji ili utengenezaji upanuke? au ni ujanja kuviunda na kukaa navyo kuvienzi wakati vinaweza kuuzwa hapa nchini na hata kwa nchi jirani ili kujipatia kpato? au uwekezaji ndo mambo yote kwa ccm? basi mpeni mchina ama Rostam maana ndio mnaowaamini kuendesha uchumi wa nchi hii.
 
Huo ni mwanzo. Hata kilimo unaanza kwa ajili kula nyumbani kisha unaongeza kwa ajili ya kuuza kwa wengine.

Back
Top Bottom