Hivi Watanzania tunajua tunachokitaka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Watanzania tunajua tunachokitaka?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mama kubwa, Oct 18, 2011.

 1. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,408
  Likes Received: 1,965
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nikijiuliza sana sisi watanzania na hasa wanamageuzi nini hasa tunachokitaka nikakosa jibu. Tumeshuhudia kwa mara ya kwanza Bunge lililopita likiwa na mvuto wa hali ya juu pale ambapo kinyume na mategemeo ya wengi bunge lileta majibu ya faraja kuhusu mkataba wenye utata wa richmond.japokuwa mwisho wake haukuwa mzuri lakini angalau Watanzania walipunguziwa kiu ya kujua sual hilo.
  kilichonifanya nitoe hoja hii ni pale nilipoona juhudi za wabunge wale kutufumbua macho kwenye mkataba wa richmond kuonekana ni unafiki bila kujali jambo hili limesaidia kiasi gani wananchi kuifahamu serekali yao inayowakebehi kuleta maisha bora kumbe inawanyonya kupitia mkataba huu na mingine feki.
  Limejitokeza suala la mheshimiwa sitta kuonekana mnafiki anapozungumzia masuala la dowans eti kwa sababu anasemekana anatafuta uraisi 2015 na kufanya kuwaacha vita hiyo apigane peke yake na Mwakyembe aliyeko hospitalini ambapo wengine wanadiriki kusema unafiki wa kuficha uovu umemfikisha hapo.
  Inawezekana ni kweli sitta anataka urais na je ni kosa? hivi yuko peke yake ? .Sitta huyu anatujulisha kwamba hizo hela za dowans ndizo zitakazotuchagulia rais 2015 sisi tunamjibu, mnafiki wewe! sitta huyohuyo anasema hizo hela tunalipa kundi dogo la wajanja sisi tunamjibu mnafiki wewe!.hivi wanamageuzi wenzagu kwa maneno hayo sitta anaisaidia ccm? au anatusaidia sisi ? si ndio jambo tulilokua tunalitaka? au tunataka nini?.walichokifanya pale bungeni ni kutupa mwanga (tip) ili sisi tuendelee mbele ilikuwa sio rahisi kwa tume ile kusema yote maana walikuwemo na bado wamo kwenye chama.
  Maoni yangu tukiendelea kuwakatisha tamaa hivi hata waliozidiwa na joto la kwenye magamba watashindwa kuja huku maana wanaona vita anayopigana sitta isivyokuwa na wanaoiunga mkono.Tupigane vita hii kama sisi ni wana mageuzi kweli maana hicho naamini ndicho tunachokitaka
   
 2. m

  mharakati JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
   
 3. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,408
  Likes Received: 1,965
  Trophy Points: 280
  ndugu yangu mharakati ukitaka kujua sisi sio great thinkers hebu angalia ukurasa wa kwanza wa jukwaa la siasa ni habari za nape tu watu wanapumbazwa wanakalia kumjadili mtu mmoja na kuacha masuala muhimu ya ya Taifa hili inasikitisha sana.Tunasubiri sitta na wengine waanze kuvimba ngozi tuseme tulishajua kitatokea.Alichohofu mwakyembe na kamati yake ndio hicho kinachompata sasa hivi. Kama watanzania tulifurahi tuliposomewa uchunguzi ule wa tume na sasa tunawakebehi ni wanafiki mie naona si sawa kabisa.
   
 4. d

  daniel_mollel Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Unafiki ni jambo la wazi tena rahisi kulitambua hasa kwa kuzingatia maneno na vitendo vya mnafiki husika. Haiwezi kuingia akilini kwa mtu asiye mvivu kufikiri kwamba hao jamaa siyo wanafiki. Kwanza swala la kushinikiza mkataba wa dowans uvunjwe wao wakiwa wanaufahamu fika tena wanafahamu na madhara ya kuuvunja alafu leo wanasimama mstari wa mbele kudai dowans wasilipwe, ni unafiki wa kiwango cha juu sana. Wangeweza kushinikiza badala ya kuvunjwa urekebishwe kama ilivyo mikataba ya madini. Pili kushinikiza tanesco wasinunue mitambo ya dowans alafu leo tanesco inanunua umeme unaozalishwa na mitambo hiyo hiyo kupitia symbion ni unafiki mkubwa zaidi. Sitta pia alikiri kuifahamu richmond na kuileta nchini kwa madai kwamba wakati huo ilikuwa safi, alafu hapo hapo anasahau kwamba alilitangazia bunge na watanzania kwamba richmond ni kampuni hewa, huoni kwamba mtu huyu ni hatari sana? Wewe unataka unafiki upi tena? Sitta huyu huyu anayepinga ufisadi EL akiwa PM aligoma asijengewe ofisi ya spika Urambo, baada tu ya kujiuzulu ikajengwa, huko Urambo inafanya kazi gani? Huo nao siyo ufisadi?
   
 5. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ah mi nadhani hatari itakuwa mbaya zaidi kama tutakuwa watu ambao tupo carried away na hisia tu kwa kila kitu cha mwanasiasa haijalishi anajipambanua vipi!
  Lile kundi lililojitambulisha kuwa linapinga ufisadi likiongozwa na Sitta na Mwakyembe ni lazima lichambuliwe sana sababu hyo vita wanayopigana inaacha mianya kibao inayopelekea ukakasi katika matamshi.
  Watanzania hawataki mtu wa uvuguvugu, ni ama uwe baridi au moto kitu ambacho makamanda hawa wa mwituni wa vita ndani ya chama chao "ccm" hakipo!
  Kwa wachambuzi wa hotuba watupe uchambuzi wa hotuba ya Lowasa wakati anajiuzulu, anazungumzia vita ya "uwaziri mkuu"....
  Hii inaweza kutupeleka mbele sana katika kuwaangalia hawa "makamanda".
  Pia jiulize, kama hii mikwaruzano yao ya "uwaziri mkuu" wangeimaliza kwa heri kwa kuelewana huko "ndani" je tungekuwa na Richmond sagga ??
  Itakuwa ajali ya kitaifa kutaka kurusu migongano binafsi iwape watu nafasi ya ushujaa.
  Mi ningewasamehe hawa jamaa kama wangesema ukweli wote katika ile ripoti yao pale bungeni, ila kwa unafiki (samahani hamna lugha mbadala hapa ule ulikuwa unafiki) eti wakajifanya kuficha baadhi ya vitu kwa kuhofia kusambaratisha serikali. Lakini wameiokoa serikali kwa gharama gani? Wameokoa nini wakati Dowans inalipwa? Nani shujaa hapo?
  Nakubali watz tunapingana sana kisiasa ila kwa hili hapana. Mzee Sitta siwezi kumkubali wala Mwakyembe (ila Mungu ampe afya apone)! Hapo hatujajadili kukwama kwa CCJ yao, nalo linaweza kutupa picha hawa ni wapambanaji wa namna gani...
   
 6. a

  alkon Member

  #6
  Oct 19, 2011
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umeongea vema. Suala la Mhe. Sitta kubadili kauli nyakati fulani mimi huwa nalichukulia kama mbinu yake kisiasa. Pamoja na kwamba yeye ni mpiganaji, lakini tusisahau kwamba bado yuko ndnai ya chama, kwa hiyo kuna nyakati anaweza kulegeza kidogo msimamo ili kujitafutia uhalali ndani ya chama. Hata hivyo, mimi bado namkubali sana walau kwa yale machache anayomudu kuyasimamia na kuyatoa hadharani. Ujue hiyo si kazi rahisi, na mpaka hapo amekubali kubeba risk kubwa sana.

  Hoja ambayo bado inanipa shida ni ule uamuzi wake wa kujenga ofisi ya spika Urambo. Kwa kweli hilo haliniingii akilinipaka leo. Hilo wala halina mjadala, ila ni matumizi mabaya ya madaraka.
   
 7. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,408
  Likes Received: 1,965
  Trophy Points: 280
  sikatai ushujaa wao wa leo unaleta mashaka lakini si ndilo Watanzania tunachokitaka ? tumejua ukweli ambao unampa nguvu kila mwananchi kuikataa Dowans? makundi yao ndio yanatupa faida kujua kipi mchele na kipi ni pumba, hii ni faida kwetu na ndilo jambo tunalotakiwa kufanyia kazi.
   
 8. m

  mharakati JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Hivi ndiyo EL anataka tuamini kuwa ni tatizo binafsi chuki binafsi kati yake na 6. tatizo hapa ni itikadi tofauti, kumbuka 6 alikaa nje ya bunge na cabinet kwa miaka 10 (95-2005) kaitka muda huu akabadilisha itikadi kwa kua alikua anaona mapungufu ya serikali ya awamu ya 3. Ukiwa nje ya kitu lazima uone mapungufu yake. 6 spika angekua vile vile kama angekua PM, na mwisho wake angetolewa tu baada ya miaka mi5 kwa sababu itikadi yake ya uongozi haifanani ni itikadi tawala ya CCM na viongozi wake kama EL. 6 alitaka tumia nafasi yake kuboresha uongozi na kujaribu kuyapunguza mabaya ya awamu ya Mkapa, wenzake walikua wanataka status-quo iendelee. Kuhusu Richmond hata angekua Pinda 6 angefanya kazi ile ile
  Nakushauri ndugu yangu uchambuzi wa siasa unafuata kanuni chache sana na hauwezi kua emotional coz politics is neither rational nor emotional
   
 9. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  kila siku najiuliza sijui aje malaika gaaani ndo atuambi ekua tunapelekwa shimoni ndo tuamini
   
 10. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Siaminishwi kitu na Mtu yeyote, ni mtazamo wangu huru kama zilivyo fikra zangu!
  El ni fisadi, wala hyo haiwezi kumfanya 6 aonekane kinara.
  Sawa mi sio mchambuzi wa siasa, ila we uliye hebu niambie utamtafsiri vipi mtu ambaye anakaa na kundi ambalo anatofautiana nalo kiitikadi na mtazamo? Na pia unajua gharama za ukweli uliofichwa kuhusu Richmond??
  Ushujaa wa 6 ni nini hasa? Kuropoka?
   
Loading...