gollocko
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 2,945
- 2,275
Hivi jamani watanzania tumerogwa? Tu wapole mpaka sasa ni kama tumekuwa wajinga,Hapa nazungumzia suala la uwajibikaji, maana kiongozi wa umma aweza kusema uongo hata mara mia au kutudanganya na ahadi hewa nasi tumezubaa tu! Hebu fuatilia porojo za waziri huyu kuhusu suala nyeti la umeme na ujionee tunavyoburuzwa kama magunia ya mashudu, porojo..porojo..porojo......
Porojo hizo zimeanza kupamba moto tangu Rais Jakaya Kikwete alipomteua mbunge wa Sengerema, William Ngeleja kuwa waziri wa nishati na madini mwaka 2008. Akizungumza bungeni, Julai 2008, Ngeleja alisema, "Tatizo la umeme litakuwa historia." Kauli yake iliungwa mkono na Aloyce Massanja, kaimu mkurugenzi wa miradi ya Mamlaka ya Uendelezaji Bonde la Mto Rufiji (Rubada), 29 Desemba 2009 pale aliposema, "Tatizo la umeme nchini litasahaulika ifikapo 2012." Aliahidi kukamilika mradi wa Stiegler's Gorge wa Rufiji wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,100 za umeme. Kiasi cha juu cha uzalishaji ni megawati 2,750.
Tarehe 24 Desemba 2010 Ngeleja akasema mgawo wa umeme utakuwa historia ifikapo 2013. Alikuwa akikagua mradi wa kuzalisha gesi wa Songosongo, Kilwa Kisiwani. Alijitapa katika miaka mitatu ijayo, kutakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 900 katika vyanzo mbalimbali.
Tarehe 15 Februari 2011, Ngeleja akisoma taarifa ya serikali kuhusu mwisho wa tatizo la umeme nchini, alionyesha ufumbuzi uko mbali mno. Alisema serikali inahitaji Sh. 300 bilioni kukamilisha miradi ya muda mfupi na mrefu kufikia mwaka 2033. Aidha, alibainisha uwezo halisi wa mitambo yote ya kuzalisha umeme katika gridi ya taifa kuwa ni megawati 1,006 ambapo mitambo ya maji ina uwezo wa megawati 561 na mitambo ya gesi asili na mafuta mazito ina uwezo wa kutoa megawati 445.
Tarehe 26 Machi 2011 akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kabita wilayani Magu mkoa wa Mwanza, Makamu wa rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akaongeza kibwagizo kwa kusema kero ya umeme inamalizika mwaka 2015.
Tarehe 25 Mei 2011, Ngeleja anampiga vijembe Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba. Alisema watu wanapita mitaani kudai yeye ni mzigo. Ngeleja alikuwa akimjibu Makamba aliyedai waziri huyo ni mzigo. Makamba alifikia hatua hiyo baada ya kumuona Ngeleja amedanganya pale aliposema serikali imedhamiria kukodi mitambo ya kufua umeme wa megawati 260 kabla ya Julai 2011. Akasema serikali imedhamiria kununua mtambo wake mpya mwaka huu wenye uwezo wa kuzalisha megawati 150. Mpaka sasa mtambo huo haujanunuliwa.
Hadithi ni ndefu. 27 Juni 2011 Ngeleja akaibuka na kusema, "umeme ni janga la taifa." Ametaka wananchi wavumilie. Alikuwa akizungumza katika semina ya wabunge mjini Dodoma. Baadaye 3 Julai 2011 Ngeleja taarifa zikavuja; maofisa katika wizara yake wamehonga baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya nishati na madini ili kupitisha bajeti ya wizara yake. Je, tatizo ni nini? Serikali haijawekeza katika eneo hili. Mabwawa ya maji yana uwezo wa kuzalisha megawati 773, lakini sasa yanazalisha umeme usiozidi megawati 400. Mitambo inayotumia gesi ina uwezo wa kuzalisha megawati 225. Kutokana na uchakavu wa mitambo ya kusafirisha na kuzalisha gesi kutoka Songosongo, mitambo ya umeme ya Songas yenye uwezo wa kuzalisha megawati 180, sasa inazalisha nusu ya megawati. Ni kati ya megawati 80-100. Tegeta wenye uwezo wa kuzalisha megawati 45, sasa unazalisha megawati 25, Symbion wenye uwezo wa kuazalisha megawati 100, sasa unazalisha megawati 60. Mitambo ya IPTL ina uwezo wa kuzalisha 100, lakini inazalisha chini ya megawati 50. Nani alaumiwe?
Hebu wanajamvi nielezeni ni nchi gani ambayo waziri angekuwa anapeta mpaka sasa kama hapa kwetu?
source; mwanahalisi 31 july 2011