Hivi watanzania tumerogwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi watanzania tumerogwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by gollocko, Jan 27, 2012.

 1. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,827
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  Hivi jamani watanzania tumerogwa? Tu wapole mpaka sasa ni kama tumekuwa wajinga,Hapa nazungumzia suala la uwajibikaji, maana kiongozi wa umma aweza kusema uongo hata mara mia au kutudanganya na ahadi hewa nasi tumezubaa tu! Hebu fuatilia porojo za waziri huyu kuhusu suala nyeti la umeme na ujionee tunavyoburuzwa kama magunia ya mashudu, porojo..porojo..porojo......

  Porojo hizo zimeanza kupamba moto tangu Rais Jakaya Kikwete alipomteua mbunge wa Sengerema, William Ngeleja kuwa waziri wa nishati na madini mwaka 2008. Akizungumza bungeni, Julai 2008, Ngeleja alisema, "Tatizo la umeme litakuwa historia." Kauli yake iliungwa mkono na Aloyce Massanja, kaimu mkurugenzi wa miradi ya Mamlaka ya Uendelezaji Bonde la Mto Rufiji (Rubada), 29 Desemba 2009 pale aliposema, "Tatizo la umeme nchini litasahaulika ifikapo 2012." Aliahidi kukamilika mradi wa Stiegler's Gorge wa Rufiji wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,100 za umeme. Kiasi cha juu cha uzalishaji ni megawati 2,750.

  Tarehe 24 Desemba 2010 Ngeleja akasema mgawo wa umeme utakuwa historia ifikapo 2013. Alikuwa akikagua mradi wa kuzalisha gesi wa Songosongo, Kilwa Kisiwani. Alijitapa katika miaka mitatu ijayo, kutakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 900 katika vyanzo mbalimbali.

  Tarehe 15 Februari 2011, Ngeleja akisoma taarifa ya serikali kuhusu mwisho wa tatizo la umeme nchini, alionyesha ufumbuzi uko mbali mno. Alisema serikali inahitaji Sh. 300 bilioni kukamilisha miradi ya muda mfupi na mrefu kufikia mwaka 2033. Aidha, alibainisha uwezo halisi wa mitambo yote ya kuzalisha umeme katika gridi ya taifa kuwa ni megawati 1,006 ambapo mitambo ya maji ina uwezo wa megawati 561 na mitambo ya gesi asili na mafuta mazito ina uwezo wa kutoa megawati 445.

  Tarehe 26 Machi 2011 akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kabita wilayani Magu mkoa wa Mwanza, Makamu wa rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akaongeza kibwagizo kwa kusema kero ya umeme inamalizika mwaka 2015.

  Tarehe 25 Mei 2011, Ngeleja anampiga vijembe Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba. Alisema watu wanapita mitaani kudai yeye ni mzigo. Ngeleja alikuwa akimjibu Makamba aliyedai waziri huyo ni mzigo. Makamba alifikia hatua hiyo baada ya kumuona Ngeleja amedanganya pale aliposema serikali imedhamiria kukodi mitambo ya kufua umeme wa megawati 260 kabla ya Julai 2011. Akasema serikali imedhamiria kununua mtambo wake mpya mwaka huu wenye uwezo wa kuzalisha megawati 150. Mpaka sasa mtambo huo haujanunuliwa.

  Hadithi ni ndefu. 27 Juni 2011 Ngeleja akaibuka na kusema, "umeme ni janga la taifa." Ametaka wananchi wavumilie. Alikuwa akizungumza katika semina ya wabunge mjini Dodoma. Baadaye 3 Julai 2011 Ngeleja taarifa zikavuja; maofisa katika wizara yake wamehonga baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya nishati na madini ili kupitisha bajeti ya wizara yake. Je, tatizo ni nini? Serikali haijawekeza katika eneo hili. Mabwawa ya maji yana uwezo wa kuzalisha megawati 773, lakini sasa yanazalisha umeme usiozidi megawati 400. Mitambo inayotumia gesi ina uwezo wa kuzalisha megawati 225. Kutokana na uchakavu wa mitambo ya kusafirisha na kuzalisha gesi kutoka Songosongo, mitambo ya umeme ya Songas yenye uwezo wa kuzalisha megawati 180, sasa inazalisha nusu ya megawati. Ni kati ya megawati 80-100. Tegeta wenye uwezo wa kuzalisha megawati 45, sasa unazalisha megawati 25, Symbion wenye uwezo wa kuazalisha megawati 100, sasa unazalisha megawati 60. Mitambo ya IPTL ina uwezo wa kuzalisha 100, lakini inazalisha chini ya megawati 50. Nani alaumiwe?

  Hebu wanajamvi nielezeni ni nchi gani ambayo waziri angekuwa anapeta mpaka sasa kama hapa kwetu?
  source; mwanahalisi 31 july 2011
   
 2. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwani ulikuwa hujui kwamba tumelogwa na kile kifimbo cha nyerere na mwenge wake? wenzio tumeshashituka. we endelea kubaki hapohapo. hivi wewe unatoka jimbo la nani vile? la geleja? bila shaka unautaka ubunge wake. work hard.
   
 3. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,827
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  umetoka uko wapi sasa? We utakuwa umerogwa tu
   
 4. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Tumerogwa, na aliyeturoga keshakufa.
   
 5. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  labda tuseme yeyote aliepigia kura magamba party amerogwa
  ndio washtuka sasa kujifunika shuka wakati kumeshakucha?
   
 6. Voice of Voices

  Voice of Voices Member

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ebu tunaone tunavyo lalamika maisha magumu, magumu CCM haijafanya kitu tunasema, lakini ikifika 2015, tukapewa tisheti na kanga za kijani tunasahu yote, hivi tunataka nini lakini?

  Sio siri kuna haja ya kuwa makini sana katika uchaguzi mkuu ujao sivyo tutalia na kusaga,sio katika kuchagu kiongozi anayefaa la asha. hata katika kulinda wizi wa kura mchezo mchafu umetawala sana,

  Angalizo mimi sio mfuasi wa chama chochote kile lakini kuweni makini na misemo ya wagombea wanapojinadi, kwa nini nasema hivi basi? msipelekwe kama upepo, mara chama hiki hakifai unahamia huku mara hiki hakifahi mnahamia huku, sasa nawambia na kaeni chini mnitegee masikio, msimomo wetu ni bora usimame kwa mtu mwenyewe na sio chama.

  Nageukia kwenu nyie CHADEMA , sawa mnato mapungufu mengi kwa CCM, lakini mjue kuwa pia nyie ni wanadam, tamaa zipo palepale, mnaweza kupewa madalaka na mkawa wezi zaidi hata kama sio wote, kwa hiyo kuweni makini mnapobainisha mapungufu hayo mtakuja kusutwa.

  • :yawn:
  /
   
 7. A

  Aaron JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2014
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 2,121
  Likes Received: 2,721
  Trophy Points: 280
  Ninachojiuliza inawezekanaje chama tawala kinahodhi matengeneza ya katiba ya wananchi ambao wanatakiwa ndio watengeneze katiba na kuwakabidhi watawala ili waifuate katiba hiyo.. Bado tunawapigia makofi na kuwaachia wajitengenezee katiba yao itakayo tumika kutuongoza sisi.. Ni kama unampa mwanafunzi ajitungie mtihani na utegemee ajitungie maswali rahisi..au mfungwa ajichagulie adhabu si atajiachia huru.. Wanasema uwazi na uwajibikaji hawajauzoea ivyo haiwezekani kuwekwa katika tunu za taifa na bado tunawapigia makofi..
   
 8. A

  Aaron JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2014
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 2,121
  Likes Received: 2,721
  Trophy Points: 280
  Ninachojiuliza inawezekanaje chama tawala kinahodhi matengeneza ya katiba ya wananchi ambao wanatakiwa ndio watengeneze katiba na kuwakabidhi watawala ili waifuate katiba hiyo.. Bado tunawapigia makofi na kuwaachia wajitengenezee katiba yao itakayo tumika kutuongoza sisi.. Ni kama unampa mwanafunzi ajitungie mtihani na utegemee ajitungie maswali magumu..au mfungwa ajichagulie adhabu si atajiachia huru.. Wanasema uwazi na uwajibikaji hawajauzoea ivyo haiwezekani kuwekwa katika tunu za taifa na bado tunawapigia makofi..
   
 9. mkute

  mkute Member

  #9
  Apr 19, 2014
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kabla na baada ya kupata uhuru mpaka mwanzoni mwa miaka ya tisini watanzania tuliheshimika sana kitaifa na hata kimataifa,ilikuwa ni jambo jema kujitambulisha kama mtanzania unapokutana na iwe mgeni kutoka afrika ama ulaya na asia,ilikuwwa ni heshima kubwa kipindi hicho,wahenga walisema mgema akisifiwa tembo hulitia maji.Bila ubishi ccm wameharibu heshima yetu kama watanzania tunadharaulika na sio mfano tena hata kwa Afrika mashariki! tunadharauliwa mpaka na wanyarwanda! watu tuliowapa hifadhi kwa miongo kadhaa kama wakimbidhi, sitaki kuongelea wakenya wala waganda kwanini basi wanatudharau sio jambo jingine bali ni IGNORANCE itokanayo na kuliwa ubongo na mdudu ajulikanae kama CCMSISM! Watu wamesoma ni maprofesa, madokta wanasheria n.k lakini kwa sababu ya U CCMSISM wanachoshauri,hoja zao,uwezo wao wa ku reason ni afadhari hata ya mtoto wa chekechea!Niulize ivi kuwa mwana ccm ni kuweka akili pembeni? mbona mnatushushia heshima yetu nyie? nakubaliana na Meya Ma------ Mfumo wenu wa kufikiri mmeubadilisha?
   
 10. G

  G4N Senior Member

  #10
  Apr 19, 2014
  Joined: Apr 6, 2014
  Messages: 126
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Mazingira yaliyojengwa na ccm ya ujinga wa watz walio wengi pamoja na njaa za wtz walio wengi wakiwemo wasomi ndiyo turufu ya interahamwe. Kama tumelogwa basi mchawi wetu ni ujinga na umasikini.
   
 11. k

  kabindi JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2014
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 334
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  umelaaniwa wewe ambaye hueleweki na huelewi unachokizungumzia!
   
 12. N

  Nyamanoro JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2014
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60
  Mswahili hawezi kutengeneza katiba hata siku moja, we are not of that type. sisi tumezoea vijiwe vya kahawa tu.
   
 13. mwa 4

  mwa 4 JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2014
  Joined: Oct 8, 2013
  Messages: 3,395
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Tatizo lako lile lile ambalo linawakumba bavicha wote huwezi kutuhu chama kwa kitu ambacho hata hakihusiani lakini pia hayo unayosema yamekuwa yakifanywa na chama chako cha chadema kwa kiasi kikubwa kweli.
   
 14. mwa 4

  mwa 4 JF-Expert Member

  #14
  Apr 19, 2014
  Joined: Oct 8, 2013
  Messages: 3,395
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Lala kwanza ukae sawa naona kichwa chako hakiko sawa au hujitambui kabisa kama ungekuwa unajitambua ungefanya mambo ya maana ukaachana na umbea na uzushi huu.
   
 15. Dr.Mo

  Dr.Mo JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2014
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 3,815
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Na wajinga wenyewe ni km ww mfano maana badala ya kuchambua mada una mwita jamaa bavicha..nchi imekuwa km ya watu wenye nazi vichwani badala ya akili
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Apr 19, 2014
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kwakuwa ameshafutwa kazi iliyobaki ni kung'oa mizizi yake 2015

  Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
   
Loading...