Hivi wasomi wetu wana utambuo?

mamushkabrain

New Member
Jun 16, 2010
2
0
Hodi hodi naingia, mara ya kwanza nachangia
roho yangu yafurahia , jamii forum kunukia
ila naumia kwa mada hii nachangia.

tunawaita wasomi, na macho yetu yapo kwao
tunajisisifu nao, kumbe tunajidanganya
si vyema nikizunguka, ngoja yangu hoja niitoe

Raisi kawatembelea, kutaka yao kura
kaenda wapamba vichwa, nao wajione bora
wakasahau shida zao, kumtwika ende nazo
juzi juzi katugomea, mishahara kuongozewa
na haha hao wasomi, ajirani waelekea
wasahau serikalini , ndipo vilio vilipo

wangeamua kulia, vilio vyao kusikika
wao wajitia kucheka, raisi kushangilia
lini Tanzania tutapata sauti?
vijana ndio nyie , macho mwayafunga
mnasahau ya mjomba, nyimbo awaimbia?

ingewapasa kusema, yale yote mlonayo
kwani ujio wake hamkuujua,mseme kawavamia?
mngeyaandika yakwenu, nanyi nafuu kujipatia
nyie si ndo viongozi , baadae kutuongoza?
kwa nini mwajinyamazia, nafasi mmepatiwa
ongeeni kwa niaba, jamii kuiokoa

ni kura kajawaomba, si hali kuwajulia
mkadanganyika na hilo, kura mkampatia
ni lipi alolitenda, kwa wenzenu walomaliza
ajira katuahidi, na maisha bora
yapo wapi hayo yote, kam asi utapelei
nawashangaa sana vijana, vigelegele mwamwagia
mmesahau ahadi, zote alowaambia

na mengi yakuyaandika, basi tu staki wachosha
ila jukwaani nitasimama
mengi nipate taamka
wana JF mpoooooooo?
 
Wasomi walio wa UDOM ni kwamba ndio kwaaanza bado wanasoma sasa hivi, kwa maana ya continuous verb, hivo bado hawajaelimika wala kuhitimu. Tusiwalaumu sana.
 
Wasomi walio wa UDOM ni kwamba ndio kwaaanza bado wanasoma sasa hivi, kwa maana ya continuous verb, hivo bado hawajaelimika wala kuhitimu. Tusiwalaumu sana.

Wanastahili sana kulaumiwa!...Kuna brodas na sistos zangu huku Mbulu hawajaenda hata darasa, lakini unapoongelea haki za raia wanaelewa kama njaa!..na huwaambii kitu cha kijinga, na walishakataa vya ma vya siasa vya JADI!
 
Wanastahili sana kulaumiwa!...Kuna brodas na sistos zangu huku Mbulu hawajaenda hata darasa, lakini unapoongelea haki za raia wanaelewa kama njaa!..na huwaambii kitu cha kijinga, na walishakataa vya ma vya siasa vya JADI!
Watu wanashindwa kuelewa: kumtambua kiongozi mbovun hakuhitaji kwenda shule, ni kama kuutambua mkono wako wa kushoto ni upi kati ya mikono miwili uliyonayo! Kiongozi alisema atafanya haya na haya, hakufanya, kwanini? Hana sababu za msingi eti ni kwa nini alishindwa, unahitaji kuwa na shahada ya chuo kikuu ili kujua huyu hakufai? binafsi sidhani!
 
Mara zote watu hupenda kuona wanachotaka kuona! Husikia wanachotaka kusikia! Lakini kuna mambo bayana ambayo hayahitaji macho wala masikio ya kiroho kuyaona na kuyatafakari. Kama huwezi kuhoji mapungufu, uzembe rushwa na ufisadi unaofanywa na serikali ya cc em bila shaka kama ni mgojwa utakuwa ICU.

Nisicho kifahamu mimi ni huu utiifu wa kinafiki usio weza hata kuhoji hata kama unaumizwa. Baada ya miaka yote hiyo ya uhuru ccm wamefanya nini cha kujivunia! Bado tunaendelea kuwa masikini wa kutupwa na hakuna hata dalili ya mwelekeo, serikali zote zimekuwa typical and ordinary wanaingia na kutoka, vipaumbele sifuri, malengo hakuna ndio maana leo utawasikia wanaanza kujiganyaga "UDOM likiuwa wazo letu ila halikuwa kwenye ilani yetu, bunch of ******" yaani mambo shagalabaghala tu! Kama ndio mwenendo huu bado safari haijaanza
 
Msishangae sana kuhusu UDOM;

Hamjui kwamba UDOM ni chuo cha kata?
 
Wanastahili sana kulaumiwa!...Kuna brodas na sistos zangu huku Mbulu hawajaenda hata darasa, lakini unapoongelea haki za raia wanaelewa kama njaa!..na huwaambii kitu cha kijinga, na walishakataa vya ma vya siasa vya JADI!
U probably missed the sarcasm.
 
Wapo wengi wanaokariri na hata kupata Phd lakini common sense hawana.
Elimu zao hazina manufaa kwa jamii na ndiyo maana maamuzi ya kidudu dudu yanazidi kuongezeka!
 
elimu ni tofauti na hekima nadhani vijana na wasomi wa sasa ni wanafiki na wamepungukiwa hekima
 
UDOM=Unalitambua Deal! Ona Mimi.

Kweli kabisa mzee JK, tumeliona deal,......... kesho tutachanganya na za kwetu.
 
Back
Top Bottom